Tuesday, 18 November 2014
MUUAJI WA MAREKANI ARUHUSIWA 'KUOA'
Muuaji kutoka Marekani Charles Manson, mwenye umri wa miaka 80, imeripotiwa kuwa atapewa leseni ya kumwoa mwanamke wa miaka 26 aliyekuwa akimtembelea gerezani.
Leseni ya ndoa hiyo ilitolewa siku 10 zilizopita kwa Manson na Afton Elaine Burton, shirika la habari la AP limeripoti.
Bi Burton alihamia Corcoran, California, miaka tisa iliyopita ili awe karibu na gereza la Manson.
Manson anatumikia kifungo cha maisha kwa mauaji ya watu saba na mtoto mmoja ambaye alikuwa bado kuzaliwa mjini Los Angeles mwaka 1969.
Kati ya aliyowaua ni muigizaji aliyekuwa mjamzito Sharon Tate, mke wa mtayarishaji filamu Roman Polanski.
Bi Burton, anayejiita Star, aliiambia AP kuwa yeye na Mason wataoana mwezi ujao. Leseni hiyo ina uhalali wa siku 90.
"Nampenda," aliongeza.
Monday, 17 November 2014
DK WA SIERRA LEONE AFARIKI DUNIA KWA EBOLA
Daktari kutoka Sierra Leone aliyekuwa akitibiwa kwa maradhi ya Ebola nchini Marekani amefariki dunia, hospitali ya Nebraska ilitangaza.
Martin Salia, ambaye ana uraia wa Marekani na amemwoa Mmarekani, aliwasili kupata matibabu kwenye jimbo hilo siku ya Jumamosi, akiwa katika hali mbaya sana.
Na siku ya Jumatatu asubuhi hospitali ilisema mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 44 alifariki dunia.
Zaidi ya watu 5,000 wamefariki dunia katika mlipuko wa Ebola wa hivi karibuni – karibu wote Afrika magharibi. Dk Salia ni mtu wa pili kufa Marekani.
Raia wa Liberia Thomas Eric Duncan alifariki dunia huko Dallas mwezi uliopita baada ya kupata virusi hivyo mjini Monrovia.
Hali ya hatari ya taifa iliyotangazwa nchini Liberia iliisha wiki iliyopita na siku ya Jumapili, Rais Ellen Johnson Sirleaf alisema ana matumaini nchi hiyo haitokuwa na virusi hivyo ifikapo Krismas.
MAANDAMANO KUPINGA KUVULIWA NGUO, KENYA
Takriban watu 200 wameandamana katika mji mkuu Nairobi, nchini Kenya, baada ya kundi la wanaume kurarua nguo za mwanamke mmoja kwa kuvaa sketi fupi.
Waandamanaji walipiga kelele wakisema “Ona aibu” na kuweka maua kwenye kituo cha basi ambapo shambulio hilo lilipofanyika, mwandishi wa BBC Anne Soy aliripoti.
Katika maandamano mengine ya upinzani, takriban wanaume 20 nao walipiga kelele wakisema “Vaa nguo, hatutaki haya”.
Kenya ni nchi ambayo wanaharakati hulalamika kuwa haki za wanawake aghlabu hukiukwa.
Kundi la akina mama, Kilimani Mums, liliandaa maandamano hayo baada ya video kusambazwa ikionyesha shambulio hilo katika mitandao ya jamii.
Ilizua hasira miongoni mwa Wakenya na kupitia mitandao ya kijamii #MydressMychoice na #strippingshame kwenye twitter siku ya Jumamosi na Jumapili.
Naibu rais wa Kenya William Ruto naye aliingia kwenye mjadala, akisema Kenya si jamii ya “kishamba” na wanaume waliomvua nguo mwanamke huyo lazima wakamatwe.
Wote, wanaume na wanawake, baadhi wakiwa wamevaa sketi fupi, waliandamana kwenye kituo cha basi na ofisi za mkuu wa polisi David Kimaiyo, wakitaka kusimamisha ukatili dhidi ya wanawake.
Bw Kimaiyo ametaka mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kuwasilisha malalamiko rasmi kwa polisi ili tukio hilo lifanyiwe uchunguzi.
POLIS WAVAMIA MISIKITI MOMBASA, KENYA
Polisi wa Kenya wamempiga risasi na kumwuua
mtu mmoja na kuwakamata zaidi ya wengine 250 katika uvamizi walioufanya kwenye
misikiti miwili mjini Mombasa.
Polisi wanasema misikiti hiyo imetumika
kuajiri wafuasi wa kundi la Kisomali, al.-Shabaab, ambalo limefanya mashambulio
kadhaa Kenya.
Wamesema msikiti
Musa na Shakinah zilikuwa zikitumika kuhifadhi silaha.
Magurunedi,
visu na bendera ya al-Shabab vinadaiwa kukamwatwa wakati wa uvamizi huo.
Tishio
za ghasia zimechangia sana kuyumbisha sekta ya utalii hasa upande wa pwani ya
Kenya.
Subscribe to:
Posts (Atom)