Tuesday, 16 December 2014

THIERRY HENRY ASTAAFU SOKA



Henry



Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry ametangaza kujiuzulu soka baada ya kudumu kwenye fani hiyo kwa miaka 20 na kuingia kwenye taaluma ya habari.

Mchezaji aliyekuwa katika timu ya taifa iliyoshinda kombe la Dunia mwaka 1998, mwenye umri wa miaka 37, aliondoka New York Red Bulls mwezi huu huku kukiwa na hisia huenda akaamua kwenda kuchezea timu nyingine.

“Imekuwa safari ya kipekee,” alisema.

Henry anajiunga na Sky Sports baada ya kuwa mchambuzi wakati wa Kombe la Dunia na BBC.

Mchezaji huyo kutoka Ufaransa, ambaye pia aliichezea Juventus, Barcelona na Monaco, alifunga magoli 175 ya Ligi Kuu ya England na yuko nafasi ya nne kwa wafungaji wa magoli mengi.


Thierry Henry
Henry akisherehekea na wenzake wa Barcelona, Sylvinho na Lionel Messi after the 2009 Champions League final


Henry alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England na matatu ya Kombe la FA akiwa na the Gunners, ambapo alicheza kati ya mwaka 1999 na 2007.

Aliongeza tuzo ya Ligi ya Ulaya akiwa na Barcelona mwaka 2009 na kurejea Arsenal kwa ajili ya mechi nne kwa mkopo kutoka Red Bulls mwaka 2012.


                                                                

Monday, 15 December 2014

USO UNAPOKUWA 'SIVYO NDIVYO'



Woman recovering from plastic surgery, from the series Beauty Recovery Room

Huwezi kukwepo matangazo. Kila pahala unapopita mjini Seoul unashauriwa kubadili umbile lako kwa njia ya upasuaji.

Gangnam eneo lenye utajiri, kila ukuta unaonyesha kuwa na alama ikiashiria upasuaji

Kwenye treni na barabarani, unaambiwa unaweza “kuupa uso wako uhai”. “upasuaji wa matiti”, “kukupa ujana”. Pia kuna “kupunguza taya” (matangazo hayo hasa kwa wanaume).

Mmoja alilalalamika kwamba kidevu chake huuma wakati wa mvua. Halafu baadae ikajulikana alikwenda kufanyiwa upasuaji wa pua lakini akashawishiwa- au akajishawsihi mwenyewe – kuwa kidevu chake kilihitaji kubadilishwa.

Matokeo yake akapata kidevu alichotaka lakini chenye maumivu zaidi. Licha ya yote hayo, bado ana nia ya kuongeza ukubwa wa matiti yake.

Kim Bok-soon spent 30 million won (£17,320) for 15 surgeries on her face over the course of a day and only afterwards found out her doctor was not a plastic surgery specialist
Kim Bok-Soon alishawishiwa kutumia paundi 17,320) kwa upasuaji wa uso mara 15

Korea kusini, wazazi huwapa zawadi mabinti zao vijana, kwa kile wanachoita “upasuaji mara mbili wa kope” unaofanya macho yawake zaidi – “yasiwe macho ya Ki-Asia”. Sababu haieleweki , wakati macho ya WaKorea yanaonekana mazuri jinsi yalivyo.

Jibu linalotokana na matangazo kwenye treni ni kwamba “kujiamini kwa umbo lako kunasababisha kuwa na imani chanya ambapo huweza kuwa msingi wa furaha”. Furaha- inayopatikana kirahisi kwa upasuaji!

Isipokuwa sasa, bila shaka, sivyo inavyoaminiwa. Hali imegeuka, mfululizo wa kesi mahakamani ambapo wagonjwa au waathirika kama wanavyojulikana- wanawashtaki madaktari waliobadilisha sura zao, lakini si kwa uzuri.

Muathrika mmoja alisema ‘bandage’ zilipotolewa: “Huu si uso wa binadamu. Unatisha hata kuliko jini au watu wa sayari nyingine.”

                                                                                                                      

YAYA WA UGANDA AHUKUMIWA





Mfanyakazi wa ndani, Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, amepewa kifungo cha miaka minne gerezani nchini Uganda kwa kumnyanyasa mtoto, katika kesi iliyozua hasira baada ya video kutolewa kwenye mitandao ya kijamii.

Alirekodiwa akiwa anampiga, akimpiga mateke mtoto huyo wa miezi 18.

Siku ya Ijumaa aliiambia mahakama kuwa kilichomchochea kumpiga mtoto huyo ni kufuatia mama wa mtoto huyo kumpiga- jambo ambalo mama wa mtoto huyo amelikataa.

Awali mashtaka ya utesaji yalifutwa baada ya waendesha mashtaka kusema si rahisi kuthibitisha hilo.

'Alinaswa na kamera'

Video ikionyesha utesaji wa mtoto huo ulizua tafrani kubwa iliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Baba yake mtoto huyo, Eric Kamanzi, aliweka kamera baada ya kugundua mtoto wake akiwa na majeraha na anaburuza mguu.

Alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwendesha mashtaka wa serikali Joyce Tushabe aliiambia mahakama kuwa mfanyakazi huyo “anajutia” na kuomba msamaha.

Video hiyo iliyochukuliwa na kamera iliyokuwa imefichwa pembezoni mwa ukumbi, inamwonyesha Tumuhirwe akimpiga mtoto huyo alipokataa kula kisha akamtupa chini kwenye sakafu, huku akimpiga na tochi kabla ya kumkanyaga na kumpiga mateke.

Baada ya kunasa ukatili huyo, baba wa mtoto huyo aliripoti tukio hilo kwa polisi Novemba 13.




Sunday, 14 December 2014

AFRIKA YANYAKUA 'MISS WORLD 2014'



Rolene Strauss wa Afrika kusini ametwaa taji la Mrembo wa Dunia ‘Miss World 2014’, akimrithi Megan Young wa Ufilipino kwa nafasi hiyo katika shughuli iliyofanyika kituo cha ExCeL Exhibition mjini  London.

Mrembo huyo mwenye umri  wa miaka 22 amekonga nyoyo za wengi kutokana pia na hali ya kuwa mwanafunzi wa udakatari kwenye nchi aliyotoka.

"Afrika Kusini hii ni kwa ajili yenu," Strauss alisema baadae.

Aliongeza pia, "Ni jukumu kubwa."

"Natumai Mrembo wa Afrika Kusini atafurahia taji hilo kwa mwaka mzima kama mie," alisema Young.
Wakati huohuo, Young alikuwa binti wa kwanza kushinda taji hilo la Mrembo wa Dunia kutoka Ufilipino mwaka jana.

Edina Kulcsar wa Hungary amekuwa wa pili, wakati Mmarekani  Elizabeth Safrit amekuwa wa tatu.


“Urembo wenye Malengo”


Kipengele cha mashindano ya Urembo wenye Malengo, “Beauty with a Purpose” ni pale washindani wanapoangaliwa kwa misingi ya mchango wao kwenye jamii.

Kwa mara ya kwanza si mmoja bali watano wametangazwa kushinda katika misingi hiyo.

Washindi hao ni Miss India, Miss Kenya, Miss Brazil, Miss Indonesia na Miss Guyana.

Mrembo wa Dunia kutoka Kenya 2014 Idah Nguma amefanya kazi ya kuwashawishi wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na ‘cleft clip’ kufanyiwa upasuaji.

Tatizo hilo ambalo linawakumba wengi Kenya, huacha mdomo wa juu wa mtoto ukiwa umekatika katikati, na kusababisha mtoto kutoweza kula wala kuongea.

Kulingana na Idah, tatizo hilo huacha watoto wakiwa wametengwa na kunyanyapaliwa na wakati mwengine hata kuuliwa.

Bahati nzuri, tatizo hilo lina tiba na linaweza kurekebishwa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo.