Sunday, 21 December 2014

MUHAMMAD ALI APELEKWA HOSPITALI



Muhammad Ali, pictured at a celebrity boxing match in 2012
Ali, aliyepigwa picha hii mwaka 2012, amekuwa na maradhi ya kutetemeka 'Parkinsons' kwa miaka 30 

Aliyekuwa bingwa mara tatu wa uzani wa juu wa masumbwi amepelekwa hospitali akiumwa mapafu ‘pneumonia’, msemaji wake alisema.

Ali, ambaye ana maradhi ya kutetemeka ‘Parkinson’, yuko katika hali nzuri, Bob Gunnell ameviambia vyombo vya habari.

"Uchunguzi unaonekana kuwa mzuri," Bw Gunnell alisema, akiongeza kuwa kukaa kwa mwanandondi huyo mwenye umri wa miaka 72 hospitalini kutakuwa kwa muda mfupi.

Hakutoa taarifa nyingine ya ziada na kutaka ombli la familia ya Ali kuachwa bila kubughudhiwa iheshimiwe.

Ali alipatikana na ugonjwa huo wa kutetemeka mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kustaafu ndondi.

Alionekana hadharani katika sherehe mwezi Septemba, eneo alipokuzwa huko Louisville kwa ajili ya Tuzo za kusaidia Binadamu za Muhammad Ali.

UCHUMI WA ZIMBABWE WAZIDI KUSUASUA



A poster showing the new 25 cent bond coin in Zimbabwe

Sarafu maalum zilizotolewa na benki kuu ya Zimbabwe zimesambazwa huku sherehe za Krismas zikikaribia.

Zimbabwe iliacha kutumia sarafu zake mwaka 2009 kutokana na kupanda sana kwa gharama za maisha na mara nyingi hutumia dola za kimarekani na randi za Afrika Kusini.

Lakini kutokana na sarafu hizi kuwa chache, wauza maduka hupewa ‘chenji’ kwa pipi au kalamu.

Gavana wa benki kuu alisema kulikuwa hakuna mpango wa kurejesha upya matumizi ya dola za Zimbabwe na sarafu hizi mpya zitaambatana na dola za kimarekani.


 A Zimbabwean looks at a Z$50bn note issued by Zimbabwe's central bank on 13 January 2009

John Mangudya alisema sarafu zenye thamani ya dola milioni 10 – kwa senti moja, senti 5, senti 10 na senti 25 – mpaka sasa zimesambazwa kwenye mabenki.

Alisema jumla ya fedha zilizosambazwa haitozidi dola milioni 50, kulingana na gazeti la taifa la Zimbabwe, Herlad.

Saturday, 20 December 2014

MTANZANIA AFUNGWA MAISHA KWA KUUA BINTI ZAKE



Indianna, miaka 3 na Savannah miaka 4




Mtanzania mmoja mwenye uraia wa Australia amefungwa maisha kwa kuua mabinti zake wawili muda mfupi baada ya kuwavalisha magauni na kuwarekodi wakicheza.

Mauaji hayo yanasadikiwa kuchochewa na chuki dhidi ya aliyekuwa mke wake, Jaji alisema.

Charles Amon Mihayo, mwenye umri wa miaka 36, lazima atumikie angalau miaka 31 jela kwa mauaji hayo.

Charles akiwasili mahakamani, mwezi Septemba



Aliwaua binti zake Savannah mwenye umri wa miaka minne na Indianna miaka mitatu kwa kuwaziba pumzi akitumia mto wakati wakicheza kombolea siku ya Jumapili Kuu,.

Mihayo baadae aliwaambia polisi ilibidi lazima afanye mauaji hayo lakini akasema hahitaji kuwapa sababu ya kwanini alifanya hivyo.

Lakini hakimu wa mahakama kuu Lex Lasry alisema uhalifu wake ulifanyika kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea na aliyekuwa mkewe.

MBEGU ZA KIUME ZA VVU ZAOSHWA NA MIMBA KUTUNGWA

Wanandoa waliopata mtoto baada ya kuosha mbegu

Hakika teknolojia inazua mengi, hata yale ambayo hayakuwahi kufikiriwa na mababu zetu karne nyingi zilizopita.

Hivi karibuni, wanasayansi wameweza kugundua namna ya kuzisafisha mbegu za kiume za mtu mwenye virusi vya Ukimwi na kuondoa virusi hivyo ili kumwezesha kutungisha mimba bila kumwathiri mwenza wake.,

Hii ni kwa wenza ambao mwanamume anaishi na VVU na mwanamke akiwa hana virusi hivyo.

Programu hiyo maalumu ijulikanayo kama SPAR, ilibuniwa ili kuwasaidia wenza hao kupata mtoto bila kumwambukiza mama na mtoto ambao mwanamume anaishi na VVU aweze kuzalisha.

Inafanyikaje?

Kisayansi, damu pekee si kipimo cha kuonyesha kuwepo kwa maambukizo ya VVU katika mwili bali hata katika majimaji ya mwilini.

Ogani zinazozalisha majimaji ya mbegu za kiume huathiriwa kwa namna ya pekee na VVU.

Daktari Bingwa wa Uchunguzi wa magonjwa, Henry Mwakyoma anasema kwa kawaida Virusi vya Ukimwi hupenda kukaa katika chembehai nyeupe(CD4).

Friday, 19 December 2014

NDEGE HII UTAPANDA KWELI?

    

Vimbwanga vya WhatsApp

UCHUNGUZI MPYA WAONYESHA EBOSSE ALIPIGWA

MMAREKANI AKAMATWA UGANDA KWA 'PESA BANDIA'

UCHUNGUZI MPYA WAONYESHA EBOSSE ALIPIGWA



 Albert Ebosse ceremony

Uchunguzi mpya wa mwili wa mcheza soka wa Cameroon Albert Ebosse unaonyesha kuwa kifo chake ni matokeo ya kupigwa badala ya taarifa ya awali kuwa alitupiwa kitu, ‘projectile’.

Mfungaji huyo wa JS Kabylie alikufa mwezi Agosti baada ya timu yake kushindwa.

Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Algeria zilisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliuawa na kitu chenye ncha kali kilichorushwa na mashabiki.

Lakini mchunguzi wa seli Andre Moune ameiambia BBC World TV: "Ukiona majeraha kwenye mabega yake, namna pekee ya kuelezea ni kuwa alishambuliwa.”

Cameroon imefanya uchunguzi huo baada ya kuombwa na familia ya Ebosse.

Aliripoti kuwa mwanasoka huyo “alipata pigo kubwa kichwani” iliyosababisha fuvu kubonyea” na kuathiri ubongo na pia alikuwa na majeraha sehemu ya juu ya mwili inayoashiria “ishara za kupambana”.

Matokeo ya uchunguzi wake yamepelekwa kwenye mamlaka za Algeria na Cameroon kwa hatua zaidi.