|
Waliohojiwa Afrika ndio wenye furaha zaidi |
Watu wenye furaha inaongezeka duniani, kulingana na
utafiti wa mwisho wa mwaka wa watu
64,000 katika nchi 65.
Shirika lililofanya utafiti huo
WIN/Gallup
liligundua kuwa 70% ya waliohojiwa wameridhika na maisha yao – idadi iliyoongezeka
kwa 10% kutoka mwaka jana.
Fiji ndilo taifa lenye furaha zaidi, huku 93% ya wakazi wakiwa na furaha na
kuridhika, na Iraq ikiwa la mwisho lenye furaha kwa 31%.
Utafiti huo umeonyesha kuwa Afrika ni bara lenye furaha zaidi, huku 83% ya
watu wakisema wana furaha au furaha sana.
Wakati huohuo, Ulaya ya Magharibi ilionekana eneo lenye watu wengi wasio na
furaha, huku 11%
wakisema hawana furaha
au hawana furaha hata kidogo.
Kwa takwimu za ulimwengu, 53% ya waliohojiwa walihisi mwaka 2015 utakuwa
mzuri zaidi kuliko 2014.
Robo tatu ya waliohojiwa Afrika walikuwa na matumaini makubwa ya maisha
kuimarika, ikilinganishwa na 26% ya waliopo Ulaya ya Magharibi.
Nigeria ndio nchi yenye hisia chanya kuliko zote, huku Lebanon ikiwa yenye
hisia hasi kuliko zote.