Tuesday, 3 February 2015

RUBANI WA JORDAN 'ACHOMWA AKIWA HAI'





Jordan imethibitisha kifo cha rubani Moaz al-Kasasbeh baada ya video iliyowekwa mtandaoni na Islamic State (IS) inayodaiwa kumwonyesha akichomwa moto akiwa hai.

Video hiyo inamwonyesha mtu mmoja akiwa amesimama kwenye kizimba huku akiwaka moto.

Maafisa wanahangaika kuthibitisha kama video hiyo ni ya kweli.

Mfalme Abdullah wa Jordan amemsifu Lt Kasasbeh kuwa shujaa, akisema Jordan lazima “isimame imara” wakati huu mgumu.

Rubani huyo alikamatwa baada ya ndege yake kushuka karibu na Raqqa, Syria, mwezi Desemba wakati wa harakati za mapambano dhidi ya IS.

Video iliyowekwa siku ya Jumanne ilisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter inayojulikana kuwa chanzo cha propaganda za IS.

BOBBI KRISTINA BROWN 'HALI MAHUTUTI'



Whitney Houston (left) and daughter Bobbi Kristina Brown. Photo: 2011
Whitney Houston pamoja na Kristina Brown mwaka 2011

Bobbi Kristina Brown, binti wa mwimbaji marehemu Whitney Houston, "yuko katika hali mbaya” baada ya kukutwa hana fahamu, familia yake imesema.

Bi Brown, mwenye umri wa miaka 21, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumamosi baada ya kukutwa katika hali hiyo ya kupoteza fahamu bafuni nyumbani kwake mjini Atlanta.

Mama yake, aliyekuwa aking’ara duniani kote, alikutwa amefariki dunia Februari 2012, akiwa na umri wa miaka 48, bafuni katika hoteli Los Angeles.

Hospitali haijsema lolote kuhusu hali yake ila familia yake imesema wapo naye.

Taarifa iliyotolewa, na familia ya Bi Brown: "Bobbi Kristina anapambana na amezungukwa na familia yake."

"Tunawaomba mheshimu ombi letu la kutuachia faragha wakati huu mgumu."

Siku ya Jumatatu, polisi walisema waliitwa nyumbani kwake Atlanta siku ya Jumamosi kwa minajil ya mtu “kuzama”.

Afisa mmoja wa polisi aliiambia redio moja kuwa hawakukuta dawa zozote za kulevya nyumbani kwake.

Baba yake Bobbi Kristina ni msanii maarufu wa miondoko ya hip-hop Bobby Brown.

Monday, 2 February 2015

WATOROKA JELA WAKITUMIA MASHUKA, INDIA


 India police (file picture)

Zaidi ya wahalifu vijana 90 wametoroka kutoka kizuizini katika jimbo la Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, polisi walisema.

Wahalifu hao, wote wakiwa chini ya umri wa miaka 18, walitoa vyuma vilivyopo kwenye dirisha na kufunga mashuka waliounganisha pamoja ambayo walitumia kushuka nayo.

Walitokea nyuma ya jengo mjini Meerut huku polisi wakiwa wamelinda kwa mbele.
Wafungwa thelathini na watano wamekamatwa mpaka sasa, polisi walisema.

Afisa mwanadamizi wa polisi Om Prakash ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kutoroka huko kumefanywa  "kwa utaalamu mkubwa hata hamna aliyegutuka".

Kitendo hicho cha kutoroka kiligunduliwa baada ya baadhi ya wafungwa walipokutwa barabarani, wakijaribu kusimamisha magari mapema Jumatatu asubuhi.

Bw Prakash alisema wale ambao bado wamekimbia ni pamoja na wafungwa waliotiwa hatiani kwa uhalifu kama vile mauaji, ubakaji, wizi na ujambazi.

Zaidi ya wahalifu vijana 31,000  wanashikiliwa kwenye vituo maalum India.

'KABURI' LA MUASI WA LRA UGANDA LAPATIKANA


Ugandan soldiers patrol as part of a mission to combat Lord's Resistance Army (LRA) rebels in Obo in the Central African Republic (CAR) on 11 May 2014
Majeshi ya Uganda yamekuwa yakimsaka LRA, Jamhuri ya Afrika ya Kati 

Jeshi la Uganda limesema limegundua mabaki ya kamanda mwenye cheo kikubwa katika kundi la waasi la LRA.

Okot Odhiambo alikuwa mmoja wa makamanda watano waliopatikana na hatia katika mahakama ya uhalifu wa kivita. 

Inaaminiwa kuwa kaburi lake limegunduliwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda aliiambia BBC kuwa majeshi ya Marekani yalikuwa yakifanya uchunguzi wa asidi nasaba (DNA) kujua iwapo ni mabaki ya mwili wa Bw Odhiambo au la.

Kamanda mwengine wa LRA, Dominic Ongwen, alifikishwa mahakama ya ICC wiki iliyopita.

Mkuu wa waasi hao, Joseph Kony, bado hajulikani alipo.

Mkuu wa waasi hao, Joseph Kony, bado hajulikani alipo.


AFRIKA YAMUENZI MWALIMU NYERERE

Jengo la Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Nchi za Afrika (AU), lililopewa jina la Mwalimu Julius Nyerere Hall wakati wa kikao cha ndani cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika makao makuu ya AU, Addis Ababa, Ethiopia. 

 Umoja wa Nchi za Afrika (AU) umetoa heshima na kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kuita jina lake moja ya majengo yake katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mwalimu Julius Nyerere anapewa heshima hiyo kwa mchango wake katika ukombozi na kuliondoa Bara la Afrika katika ukoloni. Uamuzi wa kuliita Jengo la Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo, Mwalimu Julius Nyerere Hall ulifikiwa juzi wakati wa kikao cha ndani cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Akizungumza baadaye kwenye kikao hicho, Rais Jakaya Kikwete aliwashukuru viongozi wenzake, wakiongozwa na Rais wa AU, Robert Mugabe kwa kutoa heshima hiyo kwa mwanzilishi wa Taifa la Tanzania.

Hoja ya kuliita jengo hilo Mwalimu Nyerere iliwasilishwa na Rais wa Namibia, Hifekepunye Phohamba katika kikao cha Baraza la Amani na Usalama na kufafanuliwa na Rais Mugabe.

Rais Mugabe alisema, “Sote tulikuwapo pale Tanzania, kila mtu akiwa na kambi yake ya kufanyia mafunzo ya kijeshi. Wengine tukagawanyika palepale, lakini shughuli za ukombozi zikaendelea.