Wednesday, 4 February 2015

BUSU LA WAPENZI WA JINSIA MOJA LAZUA UTATA


 

Watayarishaji wa kipindi kimoja maarufu cha kijamii cha televisheni nchini Angola wameomba radhi baada ya kuonyesha wapenzi wa jinsia moja wakibusiana na kusababisha hamaki miongoni mwa watazamaji.

Televisheni ya taifa ilisema imesimamisha kipindi hicho kiitwacho Jikulumessu kutokana na  "sababu za kiufundi ".

Watazamaji wengi wamehisi kipindi hicho kilivuka mipaka kwa kuonyesha wanaume wawili wakibusiana, licha ya kwamba mapenzi ya jinsia moja hayakuharamishwa Angola, waandishi walisema.

Kipindi hicho kilitayarishwa na kampuni inayomilikiwa na mtoto wa kiume wa rais wa nchi hiyo.

Jose Eduardo Paulino dos Santos, muigizaji mkuu ambaye jina lake la uigizaji ni Coreon Du, amekuwa akishutumiwa kuunga mkono wapenzi wa jinsia moja Angola, nchi ambayo wengi wana misimamo mikali ya kidini na maadili tofauti ya kijamii.

Kampuni yake, Semba Productions, ilisema ilikuwa ikitathmini upya kipindi hicho na kuomba radhi kwa lolote baya lililotokea.


KENYA KUPEWA MKOPO WA DOLA MILIONI 700



 IMF Managing Director Christine Lagarde shaking hands with Kenyan president Uhuru Kenyatta. 4 January 2014

Shirika la Fedha duniani IMF  limekubali kutoa mkopo wa takriban dola milioni 700 nchini  Kenya.

Fedha hizo zitatumika kama sera ya bima kujilinda kwa tishio lolote la uchumi wa nchi, ikizingatiwa nchi hiyo iko imara kiuchumi Afrika Mashariki.

Serikali ya Kenya iliomba pesa hizo kama njia ya tahadhari, iwapo kutatokea dharura kama vile majanga ya asili au mashambulio kutoka kwa wapiganaji.

Fedha hizo zitakuwepo kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.

Wizara ya fedha imeiambia IMF haina nia ya kutumia pesa hizo.

Badala yake itatumika kama kinga dhidi ya “mtikisiko wa kiuchumi”, IMF ilisema.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

                                                                                                        


WAPIGANAJI WAWILI WANYONGWA JORDAN



Sajida al-Rishawi in military court in Jordan. Photo: 2006
 Sajida al-Rishawi alipewa hukumu ya kifo huko Jordan kwa takriban muongo mmoja 

Jordan imewanyonga wafungwa wawili, akiwemo mpiganaji mmoja wa kike, kufuatia mauaji ya rubani wao mmoja wa kijeshi aliyeuawa na wapiganaji wa Islamic State (IS).

Mwanamke huyo, aliyekuwa amejitolea mhanga lakini hakufanikiwa Sajida al-Rishawi, na mshirika wa al-Qaeda Ziyad Karboli – wote wakiwa raia wa Iraq – walinyongwa alfajiri, maafisa walisema.

Mauji hayo kwa kunyonga yalifanyika saa chache baada ya IS kuweka video ikionyesha rubani Moaz al-Kasasbeh akichomwa moto ilhali yuko hai.

Alikamtwa baada ya kupata ajali wakati wa kupambana na IS huko Syria mwezi Desemba.

Jordan ilikuwa ikifanya jaribio la kumwokoa Lt Kasasbeh ili aachiwe huru kwa kubadilishana naye na Rishawi.

Rishawi alipewa hukumu ya kifo kwa kuhusika na mashambulio katika mji mkuu wa Jordan, Amman, ulioua watu 60 mwaka 2005.

Karboli alitiwa hatiani mwaka 2008 kwa kumwuua raia wa Jordan.

Tuesday, 3 February 2015

WABUNGE WAKUBALI MTOTO KUPITIA WATU WATATU



 An embryo

Wabunge wamepiga kura kuunga mkono utengenezaji wa watoto kwa asidi nasaba kutoka wanawake wawili na mwanamme mmoja, katika tukio la kihistoria.

Uingereza sasa itakuwa nchi ya kwanza kuanzisha sheria kuruhusu utengenezaji watoto kwa kutumia watu watatu.

Katika upigaji kura bungeni, wabunge 382 waliunga mkono huku 128 wakipinga mchakato huo unaozuia maradhi yanayohusisha asidi nasaba zinazopita kwa mama kwenda kwa mtoto.

Wakati wa mjadala, mawaziri walisema muundo huo ni “mwanga mwisho wa tanuri la kiza” kwa familia nyingi.

Kura nyingine inatakiwa kupigwa kwenye bunge la House of Lords. Kama kura ikipitishwa basi mtoto wa aina hiyo atazaliwa mwakani.

Inakadiriwa watoto 150 kutoka wazazi watatu huenda wakazaliwa kila mwaka.

RUBANI WA JORDAN 'ACHOMWA AKIWA HAI'





Jordan imethibitisha kifo cha rubani Moaz al-Kasasbeh baada ya video iliyowekwa mtandaoni na Islamic State (IS) inayodaiwa kumwonyesha akichomwa moto akiwa hai.

Video hiyo inamwonyesha mtu mmoja akiwa amesimama kwenye kizimba huku akiwaka moto.

Maafisa wanahangaika kuthibitisha kama video hiyo ni ya kweli.

Mfalme Abdullah wa Jordan amemsifu Lt Kasasbeh kuwa shujaa, akisema Jordan lazima “isimame imara” wakati huu mgumu.

Rubani huyo alikamatwa baada ya ndege yake kushuka karibu na Raqqa, Syria, mwezi Desemba wakati wa harakati za mapambano dhidi ya IS.

Video iliyowekwa siku ya Jumanne ilisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter inayojulikana kuwa chanzo cha propaganda za IS.