Tuesday, 9 September 2014
SAFARI ZIENDELEE LICHA YA EBOLA KUSAMBAA - AU
Wakuu wa Umoja wa Afrika wametoa wito wa kuondolewa kwa vizuizi vya safari vilivyotolewa kwenye nchi zilizoathirika na maradhi ya Ebola licha ya shirika la Afya Duniani WHO kuonya maelfu ya watu wengine kuathirika katika wiki chache zijazo.
“Nchi wanachama wafute vizuizi vyote vya safari ili kufungua fursa za kiuchumi,” Mkuu wa tume ya AU Nkosazana Dlamini-Zuma aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa dharura mjini Addis Ababa, Ethiopia, ulioitishwa kujadili kuhusu Ebola.
Lakini alisema “lazima mchakato thabit wa kupima uwekwe”.
Idadi ya waliofariki dunia kutokana na maradhi hayo ya Ebola – yanayoenea Afrika magharibi, huku Liberia, Guinea na Sierra Leone zikiwa zimeathirika zaidi, imefikia 2,000, huku takriban 4,000 sasa wakiwa wameambukizwa, WHO imesema.
Shirika la Umoja wa Mataifa limeionya Liberia kuwa “maelfu” ya maambukizi mapya ya Ebola yataibuka katika kipindi cha wiki tatu zijazo, ongezeko kubwa sana kutoka idadi ya 2,000 walioathirika sasa.
Katika harakati za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo, baadhi ya nchi zilizoathirika zimezuia eneo zima watu kutoka, wakati baadhi ambao hawajaathirika wamesimamisha safari za ndege.
Wataalamu wameonya kutetereka kwa uchumi ambapo kumesababishwa na vizuizi hivyo vinaongeza madhila kwenye bara hilo la Afrika, wengine wakisema kuzuia safari za ndege kumepunguza kasi ya kupeleka tiba maeneo yaliyoathirika.
Chanzo: Al Jazeera
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
MAJESHI YA AU 'YABAKA' MABINTI SOMALIA
Majeshi ya Umoja wa Afrika AU yanayodhaminiwa na mataifa ya kigeni yaliyopo Somalia yamewabaka kwa pamoja wanawake na watoto wa kike, wengine, mpaka wakiwa chini ya umri wa miaka 12 na kutumia chakula cha misaada kama biashara ya kupata ngono, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, HRW limesema.
Majeshi 22,000 ya AU, yanayoitwa AMISOM, yakiwa na wanajeshi kutoka mataifa sita, yamekuwa yakipigana sambamba na majeshi ya serikali dhidi ya kundi linalohusishwa na al-Qaeda la al-Shabab tangu mwaka 2007.
"Baadhi ya wanawake waliobakwa walisema wanajeshi hao huwapa chakula au pesa baada ya kitendo hicho katika jaribio la kutoa madai ya kufanya ngono kwa makubaliano," HRW imesema kwenye ripoti hiyo.
AMISOM imesema madai hayo ya ubakaji ni"ya nadra" na kuita ripoti hiyo "kutokuwa na uwiano na inapendelea".
Wafadhili wa AMISOM ni Umoja wa Ulaya na Marekani
Chanzo: Al Jazeera
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Monday, 8 September 2014
BUNGE LA IRAQ LAAPISHA SERIKALI YA UMOJA
Wanachama wengi wa bunge hili jipya waliapishwa siku ya Jumatatu |
Bunge la Iraq limepitisha serikali mpya ikiwa na manaibu waziri mkuu wa Ki-Sunni na Ki-Kurdi, huku ikijaribu kupambana na wapiganaji wa IS waliodhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo.
Saleh al-Mutlak na Hoshyar Zebari wamepitishwa ndani ya makubaliano ya kugawana madaraka baada ya wiki mbili za mfarakano wa kisiasa.
Waziri mkuu Haidar al-Abadi, Mshia mwenye msimamo wa kati, aliombwa kuunda serikali baada ya kujiuzulu kwa Nouri Maliki.
Hata hivyo, hawajakubaliana kuhusu waziri wa ndani na wa ulinzi.
Bw Abadi ameahidi kujaza nafasi hizo katika kipindi cha wiki moja.
Mrithi wake alilazimishwa kujiuzulu mwezi Agosti, kufuatia Waarabu wa Kisunni na jumuiya za Kikurdi kushutumu serikali yake kuweka sera za upinzani.
Marekani iliisihi Iraq kuunda serikali itakayohusisha wote wakiwemo wawakilishi wa Sunni, wakiielezea kama sharti la kuongeza nguvu za kijeshi dhidi ya IS.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
WATAWA WATATU WAUAWA BURUNDI
Olga Raschietti amekaa miaka mingi Afrika ya Kati |
Polisi nchini Burundi imesema watawa watatu,
watu wazima wamebakwa na kuuawa kwenye makazi yao nje ya mji mkuu Bujumbura.
Watawa wawili waliuawa siku ya Jumapili huku
mtawa wa tatu ambaye mwili wake uligundulika mapema siku ya Jumatatu ulikutwa
kichwa chake kikiwa kimekatwa.
Watawa hao wametajwa kuwa Lucia Pulici, mwenye umri wa
miaka 75, Olga Raschietti, miaka 82, na Bernadetta Boggian, mwenye miaka 79.
Serikali imesema anayeshukiwa kufanya mauaji
hayo katika shambulio la kwanza alionekana akikikmbia makazi ya watawa hao huku
akiwa na kisu mkononi.
Dayosisi ya Italia huko Parma imesema watawa
hao wameuawa kukiwa na jaribio la ujambazi.
Hatahivyo, polisi wa Burundi, wamesema nia
yao haijulikani ni nini, kwani hakuna pesa zozote zilizoibiwa.
Mwaka 2011, mtawa kutoka Croatia na
mfanyakazi wa kutoa misaada wa Italia waliuawa katika jaribio la wizi kaskazini
mwa Burundi.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
'KUPIMWA NGUVU' KABLA YA NDOA
Pendekezo la Mahakama Kuu ya Madras kuwataka wanaume na wanawake kufanya
vipimo kabla ya kufunga ndoa limewafurahisha wengi huko kusini mwa India na la
kushangaza wanawake wengi wameridhishwa na uamuzi huo kuliko wanaume.
"Watoto wa kike mpaka leo wanaonekana kama mzigo usio na umuhimu. Bila hata
uchunguzi wa kutosha wa bwana harusi, binti hutolewa kwenye familia zao kwa minajil ya
ndoa," Justice N Kirubakaran
ameshuhudia katika kesi moja ambapo mwanamke anadai talaka kwa madai kuwa mumewe
hana nguvu za kiume.
Uamuzi huo wa mahakama pia umewafurahisha wanasheria, watabibu na jumuiya
ya wanafunzi.
Mwanasheria T S R
Venkataramana alisema, “Pendekezo la mahakama ni sahihi na ni mabadiliko
chanya. Lakini katika hali ya uhalisia haliwezekani. Jamii yetu lazima ibadilike kulikubali hilo.”
Dr Abdul Latiff alisema,
“Siku hizi, watoto wa kike na wa kiume wana taarifa nyingi za ngono, ambazo
wanajifunza kupitia televisheni na mtandao. Hivyo vipimo kabla ya ndoa ni jambo
jema.
Hata hivyo, alisema si rahisi kutekeleza. Miaka
kadhaa iliyopita, kuonyesha cheti cha hospitali cha kupima ukimwi kabla ya ndoa
ilisistizwa, hata hivyo, lengo halikufanikiwa.
Chanzo: The Times of India
Subscribe to:
Posts (Atom)