Tuesday, 11 November 2014
MAZISHI YA KITAIFA KWA RAIS WA ZAMBIA
Zambia imefanya mazishi ya kitaifa kwa ajili ya Rais Michael Sata, aliyefariki dunia mwezi uliopita kwenye hospitali moja nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 77.
Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi hayo katika uwanja wa taifa wa Mashujaa kwenye mji mkuu, Lusaka.
Akijulikana kama “King Cobra” kwa ulimi wake mkali, Bw Sata alichaguliwa kuwa Rais wa Zambia mwaka 2011.
Nchi hiyo kwa sasa inaendeshwa na rais anaye kaimu, na uchaguzi upya unatarajiwa kufanyika mwezi Januari.
Mwandishi wa BBC aliyopo Lusaka Dennis Okari amesema ni shughuli yenye hisia kali.
Katika wiki iliyopita, raia wa nchi hiyo wametoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kiongozi wao – wakipita pembeni ya mwili wake uliokuwa umelazwa kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano Mulungushi.
Alifariki dunia siku chache baada ya Zambia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kutoka Uingereza.
Alikuwa rais wa pili wa Zambia kufa akiwa madarakani
KAPTENI WA KOREA KUSINI MIAKA 36 JELA
Kapteni wa kivuko cha Korea kusini kilichozama mwezi Aprili amekutwa na kosa la kudharau na kuhukumiwa miaka 36 jela.
Kivuko hicho kilikuwa na abiria 476 kilipozama. Zaidi ya 300 wamefariki dunia, wengi wao wakiwa wanafunzi.
Lee Joon-seok ni miongoni mwa wafanyakazi 15 wa kivuko hicho walioshtakiwa kutokana na tukio hilo, miongoni mwa balaa kubwa kutokea majini Korea kusini.
Waendesha mashtaka wamemshatki kwa mauaji ‘homicide’ na kutaka apewe adhabu ya kifo, lakini majaji walimfutia hukumu hiyo.
Lee ana zaidi ya umri wa miaka 60, na alikubali mahakamani kuwa katika siku zake zilizobaki duniani abaki gerezani.
Majaji walisema bila shaka si yeye peke yake anayehusika na tukio hilo na wamekubali kuwa kudharau kwake hakumaanishi alikuwa na nia ya kuua.
Monday, 10 November 2014
MWANAMKE ABURUZWA UTUPU KWA PUNDA, INDIA
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 anatuhumiwa kumwuua mtoto wa ndugu yake |
Baraza la kijiji katika wilaya ya Rajsamand pia iliagiza uso wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 upakwe rangi nyeusi.
Familia ya ndugu zake inamshutumu mwanamke huyo kwa mauaji. Polisi wamewakamata watu 39.
Amri zinazotolewa na mabaraza ya vijiji- yaitwayo panchayats- hazina haki yoyote kisheria lakini yanaheshimiwa sana vijijini.
Afisa mwandamizi wa polisi Shweta Dhankhad aliiambia idhaa ya Hindi ya BBC kuwa tarehe 2 Novemba, mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 45, Vardi Singh, alijiua katika kijiji cha Thurawad.
Siku tatu baada ya maziko yake, mke wake na ndugu wengine walikwenda polisi wakidai Bw Singh aliuliwa na shangazi yake.
Siku ya Jumamosi usiku, familia hiyo ilikwenda kwa baraza la kijiji na kukubali mwanamke/shangazi huyo alikuwa na hatia ya mauaji.
Kwa amri ya baraza hilo, mwanamke huyo alikatwa kipara na uso wake kupakwa makaa, akavuliwa nguo zote na kuburuzwa kijijini hapo kwa punda.
Waandishi wanasema wanawake mara kwa mara huvuliwa nguo hadharani maeneo ya vijiji vya India kwa nia ya kuwaadhibu na kuwadhalilisha.
WANAFUNZI WA SEKONDARI WAUAWA NIGERIA
Wazazi wa watoto waliojeruhiwa wamekusanyika katika hospitali ya Potiskum |
Takriban wanafunzi 46 wameuawa na mtu mmoja aliyejitoa mhanga, wanafunzi hao walipokuwa kwenye mstari shuleni kwenye mji ulio kaskazini-mashariki mwa Nigeria uitwao Potiskum, polisi walisema.
Polisi wanapendekeza kuwa Boko Haram ndio waliofanya shambulio hilo.
Gavana wa jimbo la Yobo amefunga shule zote za umma huko Potiskum na kuikosoa serikali kwa kutotatua tatizo hilo.
Tarehe 17 Oktoba serikali ya Nigeria ilidai imekubaliana na Boko Haram kusitisha mapigano.
Lakini wiki mbili baadae kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau alikana madai hayo na kusema kwenye video: “ Hatujasitisha mapigano na mtu yeyote. Hatujakubaliana na mtu yeyote. Ni uongo.”
CHEKI JAMAA ALIVYO MSANII!
Vimbwanga vya WhatsApp
Kwa habari nyingine:
ZITTO: NASHAMBULIWA, TUNASHAMBULIWA 'HATUTETEREKI' http://bit.ly/1zcURF0
WABIDUN WA KUWAIT 'KUPEWA URAIA' WA COMOROS http://bit.ly/1wK63K7
WABIDUN WA KUWAIT 'KUPEWA URAIA' WA COMOROS
WaBidun wamekuwa wakiomba uraia wa Kuwait kwa muda mrefu, jambo linalopingwa na serikali |
Afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya ndani aliliambia gazeti moja nchini humo kuwa watu hao wa Bidun watapewa uraia maalum wa kiuchumi kwenye visiwa hivyo.
Alisema wale watakaokubali watapewa vibali vya ukaazi nchini Kuwait.
Zaidi ya Wabidun 100,000 wanadai uraia wa Kuwait lakini huchukuliwa kama wakazi wanaokaa kinyume cha sheria na serikali hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni, wamekuwa wakiandamana wakitaka uraia wa Kuwait na polisi wamekuwa wakiwatawanya kwa nguvu. Mamia wamekamatwa.
Serikali ya Kuwait imesema ni WaBidun 34,000 wenye sifa za kufikiriwa iwapo wapate uraia wa Kuwait au la.
Wengine huchukuliwa kama raia wa nchi nyingine ambao huenda walihamia Kuwait baada ya kugunduliwa kwa mafuta miongo mitano iliyopita au vizazi vya wahamiaji hao.
Serikali ya visiwa vya Comoro hadi sasa hawajasema lolote kuhusiana na ripoti hiyo.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Sunday, 9 November 2014
ZITTO: NASHAMBULIWA, TUNASHAMBULIWA! PAC TUNASEMA “HATUTETEREKI”
'Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCO izalishe au isizalishe Umeme!
'Kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP.'
Ifuatayo ni kauli ya Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu heka heka ya uchunguzi wa akaunti ya Tegeta Escrow inayohusisha kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.
Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege). Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.
Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.
Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari “Zitto na Filikunjombe wanatumiwa na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu” zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.
Tuhuma #1 :
Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.
Majibu:
Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.
'TIKISA' KABLA YA KUTUMIA
Vimbwanga vya WhatsApp
WATOTO WA NCHI ZINAZOENDELEA WANA 'RAHA' ZAIDI http://bit.ly/1xixUjx
MISS TANZANIA AWEZA 'KUFUNGWA' MIAKA 3 http://bit.ly/1ttgpYD
MISS TANZANIA AWEZA 'KUFUNGWA' MIAKA 3 JELA
Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu (katikati) akiwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima pamoja na watatu Jihan Dimachk |
Shindano la mlimbwende wa Tanzania maarufu kama Miss Tanzania limetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, huku likiandika historia mbaya baada ya mrembo wa 2014, Sitti Mtemvu kuvua taji hilo kutokana na kashfa ya kudanganya umri.
Kutokana na uamuzi huo, nafasi ya Sitti sasa itachukuliwa na Miss Arusha, Lilian Kamazima ambaye alishika nafasi ya pili katika Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014, lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kung’oka kwa Sitti katika nafasi yake ya mlimbwende wa Tanzania ni tukio la kwanza tangu kurejeshwa kwa mashindano ya Miss Tanzania 1994.
Miss Tanzania wa 2000, Hoyce Temu akizungumzia hatua ya Sitti jana, alisema amepokea habari hizo kwa masikitiko ingawa ni kitendo ambacho kimerudisha heshima kwa tasnia ya urembo nchini.
“Baada ya hili sakata, kwa kweli tulivunjika moyo sisi warembo, kila tulipopita tulionekana kama watu tusio na maadili, tuliharibiwa jina na ilituvunja moyo, lakini kwa kuwa ameamua kurudisha taji, ameibadilisha Miss Tanzania,” alisema Hoyce.
Katika barua yake ya Novemba 5, mwaka huu kwenda kwa waandaaji wa shindano hilo ambao ni Kampuni ya Lino International Agency Ltd, Sitti alisema amechukua uamuzi huo kwa hiari bila kushawishiwa na mtu ili kulinda heshima yake pamoja na familia yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)