Saturday, 22 November 2014

KIFO CHA MTOTO KILICHOZUA HASIRA, UGANDA



Man holding the body of Ryan Ssemaganda
Mwili wa Ryan Ssemaganda (uliobebwa) ulizikwa nyumbani kwao nje kidogo ya Kampala

 Mazishi ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili yamefanyika Uganda,

Kifo chake kiliamsha hamaki kufuatia hatua ya kugongwa na gari la manispaa ya jiji la Kampala baada ya mama yake kukamatwa kwa kuuza matunda kinyme na sheria.

Familia ya Ssemaganda na wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika hadi maafisa wakiri kuhusika na kifo chake.

Mwili wa marehemu ulipelekwa bungeni siku ya Alhamis kuonyesha kupinga kwa tukio hilo.

Waganda wengi wanahisi manispaa ya jiji la Kampala linawaonea sana wachuuzi.

Mkasa mzima

Mama yake alikamatwa siku ya Jumatatu kwa kuuza matunda mitaani bila kibali.

Siku iliyofuata, bibi yake alimchukua mtoto huyo kwenye ofisi za Mamlaka za Mji Mkuu Kampala (KCCA), alipokuwa amewekwa kizuizini mama huyo, ili aweze kumnyonyesha.

Ryan Ssemaganda's mother (right)
Mama yake Ryan Ssemaganda( kulia) sasa ameachiliwa huru 

Maafisa wa KCCA inaripotiwa walimkatalia, lakini wakati majadiliano yanaendelea, alimponyoka bibi yake na kugongwa na gari la KCCA.

Siku ya Alhamis polisi walizuia mwili wa mtoto huyo kupelekwa bungeni.

"Hatutaki maiti bungeni. Nendeni mkamzike, msivuruge amani ya maiti," alisema kamanda wa polisi wa kanda hiyo James Ruhweza, kulingana na gazeti la Monitor.

Alisema dereva wa gari hilo atafunguliwa mashtaka na kuisihi familia isiruhusu wanasiasa kuwatumia kutokana na tukio hilo.

Mwanasiasa wa upinzani Erias Lukwago alitembelea familia hiyo kabla ya kuchukua mwili wa mtoto huyo bungeni, gazeti la Monitor limesema.


RAIS WA INDONESIA ASAFIRI DARAJA LA 'ECONOMY'




Rais wa Indonesia amesababisha kitahanani kwa kupanda ndege daraja la ‘Economy’ kuelekea Singapore kuhudhuria mahafali ya kidato cha sita ya mtoto wake wa kiume.

Joko Widodo na mkewe walikataa kuchukua ndege ya Rais kwasababu ilikuwa safari ya binafsi.

Wawili hao walijilipia tiketi, japo serikali imelipia gharama za walinzi waliofuatana nao.

Baadhi ya wachunguzi wamemsifu Bw Widodo, wengine wanasema ni kutaka tu kupata  umaarufu.


Indonesia President, Joko Widodo
Rais wa Indonesia, Joko Widodo, akichukua selfie na wanafunzi katika shule ya mwanawe mjini Singapore


Baba au rais?                

Rais wa Indonesia na mkewe, Iriana, walienda kwenye mahafali ya mtoto wao wa mwisho, ambapo rais huyo alipiga picha za ‘selfie’ na wanafunzi wengine.

Walisafiri na ndege ya taifa, Garuda Indonesia, siku ya Ijumaa, na kupanga foleni kusubiri nyaraka zao zikaguliwe mjini Jakarta na abiria wengine, hivyo kusababisha abiria wengi kumshangaa.

"Rais anasafiri kama baba, si mkuu wa nchi, “ alisema afisa mmoja wa Indonesia, akielezea safari hiyo ya aina yake kwa mtu kama Rais.

Joko Widodo -  anayejulikana kwa jina la Jokowi – alijijengea taswira ya mtu wa watu, kwanza kama meya wa mji wa Solo halafu kama gavana wa Jakarta.


MASANDUKU YENYE 'KELELE' YAPIGWA MARUFUKU



Grand Canal, Venice, 27 Sep 2014
Venice, mji wenye mvuto mkwabwa wa watalii  nchini Italia

Mji wa Venice unafikiria kupiga marufuku utumiaji wa masanduku yanayotumia matairi yanayopiga kelele kwa madai yanawafanya watu kuwa macho usiku mzima.

Maafisa wanataka wageni wote kuachana na masanduku hayo au kutumia “yasiokuwa na makelele”  na mbadala uwe matairi yaliyojaa hewa au kimiminika.

Matumani ni kuwa hatua hiyo italinda pia mitaa ya kale ya mji huo.

Venice ni miongoni mwa miji mikubwa inayopata watalii wengi Italia, huku watu milioni 27 wakimiminika kila mwaka.

"Amri hiyo inatolewa kukabiliana na malalamiko mengi kutoka kwa raia mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni kwa manispaa husika kuhusu kero kubwa inayosababishwa na watu kusogeza vitu mchana na usiku," kulingana na mtandao wa manispaa ya Venice.

Lakini meneja mmoja wa hoteli aliiambia BBC anahisi amri hiyo haitotekelezeka.

Alisema kama maeneo wanaotumia wapita njia ‘pavements’ yana makelele sana, basi mji huo ubadilishe seheumu hizo badala ya masanduku.

SHAMBULIO LA BASI KENYA LAUA 28



Archive photo of al-Shabab fighters, 2011
Al-shabab limekuwa likifanya mashambulio kadhaa nchini Kenya

Wanaoshukiwa kuwa wanachama kutoka kundi la Kisomali la al-Shabab wameua takriban watu 28 katika shambulio la basi kaskazini mwa Kenya, maafisa walisema.

Basi hilo lilikuwa linaelekea mji mkuu, Nairobi, liliposimamishwa kwenye kaunti ya Mandera, karibu na mpaka wa Somalia.

Watu hao wenye silaha waliwatenganisha wale waliodhani si Waislamu kabla ya kuwaua, kulingana na maafisa walioambiwa na walioshuhudia.

Al-Shabab, ambalo limekuwa likifanya mashambulio nchini Kenya tangu mwaka 2011, limekiri kufanya shambulio hilo.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao unaohusishwa na kundi hilo limesema shambulio hilo limefanywa katika hali ya kulipiza kisasi kutokana na uvamizi wa polisi katika misikiti mjni  Mombasa mapema wiki hii.

Friday, 21 November 2014

WEMA HAUOZI

  

Vimbwanga vya WhatsApp

Habari nyingine: 

RAIS OBAMA AFANYA MABADLIKO KWA WAHAMIAJI http://bit.ly/1F7qFN1

BASI LA KWANZA KUTUMIA 'KINYESI CHA BINADAMU'

RAIS OBAMA AFANYA MABADILIKO KWA WAHAMIAJI



Undocumented immigrant Angela Navarro and her husband Ermer Fernandez (L), along with other immigrants and supporters, watch U.S. President Barack Obama speak 20 November 2014
Wahamiaji wasio na nyaraka halali wakisikiliza hotuba ya Rais Obama huko Philadelphia

Mamilioni ya wahamiaji wanaoishi kinyume naa sheria Marekani wataruhusiwa kuomba kibali cha kufanya kazi katika mtikisiko mkubwa uliotangazwa na Rais Barack Obama.

Inahusisha wahamiaji walioishi Marekani kwa miaka mitano wenye watoto wanaoishi kihalali nchini humo.

Takriban watu milioni tano wanatarajiwa kufaidika kutokana na mabadiliko hayo aliyolazimisha kutumia madaraka yake, inayomruhusu Bw Obama kuliruka bunge la Congress.

Chama cha Republican kimemshutumu rais huyo kwa “madaraka ya kunyakua kwa nguvu isivyo halali”.

Inakadiriwa kuwepo wahamiaji haramu milioni 11 Marekani.

Katika mpango wa Bw Obama, wazazi ambao hawana nyaraka halali ambao watoto wao ni raia wa Marekani au wakazi halali wataruhusiwa kuomba kibali cha kazi kitakachodumu kwa miaka mitatu.

Wazazi tu walioishi Marekani kwa miaka mitano wataruhusiwa kuomba kibali hicho – takriban watu milioni nne wanakadiriwa kuwa na sifa hizo.

Ingawa mpango huo utaruhusu mamilioni ya watu kufanya kazi, haitotoa fursa ya kupata uraia au kupata haki zote sawa kama Mmarekani, alisema.

"Kama wewe ni mhalifu, utahamishwa. Kama una mpango wa kuingia Marekani kinyume na sheria, uwezekano wa kukamatwa na kurejeshwa ndio umeongezeka," alisema.