Wednesday, 3 December 2014

'MARUFUKU' KUTUMIA JINA SAWA NA LA RAIS


This undated picture released from North Korea's official Korean Central News Agency (KCNA) on January 12, 2014 shows North Korean leader Kim Jong-Un

Korea Kaskazini inaripotiwa kuamuru mtu yeyote mwenye jina sawa na la kiongozi wake Kim Jong-un, kubadili mara moja., kulingana na vyombo vya habari vya Korea kusini.

Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Korea Kusini zinasema jina hilo limezuiliwa kupewa  kwa watoto wanaozaliwa kuanzia sasa.

Mbali na hilo na wale wanaolitumia, tayari wanalazimika kubadili vyeti vyao vya kuzaliwa na nyaraka za makazi yao.

Amri hiyo ilitolewa tangu mwaka 2011 lakini ndio kwanza sasa imetolewa hadharani.

Karibu asilimia ishirini ya familia za Kikorea zina jina la Kim na Jong-un.

Japo maelekzo yamenukuliwa kuwa  hatua hiyo ni hiari, waandishi walisema wachache Korea Kaskazini wataacha kutii.

KESI INAYOMKABILI RAIS KENYATTA ITAENDELEA?


Kenya's President Uhuru Kenyatta leaves after attending the Mashujaa Day (Hero's Day) celebrations at the Nyayo National Stadium in Nairobi, on 20 October 2014.
Bw Kenyatta alichaguliwa mwaka 2013, licha ya kukabiliwa na mashtaka ICC

Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC imempa kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda muda wa wiki moja aondoe mashtaka dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Kama si hivyo ametakiwa awasilishe taarifa kuelezea ikiwa ana ushahidi wa kutosha kuendeleza kesi hiyo.
Mahakama hiyo imekataa ombi la kiongozi huyo wa mashtaka kuiahirisha kesi dhidi ya Bwana Kenyatta ili kumpa muda kutafuta ushahidi zaidi. 

Bw Kenyatta alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi kufikishwa rasmi mahakamani tangu kushtakiwa mwaka 2012 kwa uhalifu dhidi ya binadamu, jambo analokataa.

Upande wa mashtaka mara kwa mara umeomba muda zaidi kujenga hoja ya kesi hiyo.
Wamesema mashahidi wamekuwa wakihongwa na kutishwa, na serikali ya Kenya imekataa kukabidhi nyaraka muhimu zinazotakiwa.

Bw Kenyatta amekana kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wenye utata mwaka 2007 ili kuzuia ushindi wa kwa wakati ule Rais Mwai Kibaki na kusema kesi ya ICC ni ya kisiasa.

MAHOJIANO YA BBC KUHUSU HIV 'KUPUNGUA MAKALI'

     
Utafiti mkubwa wa kisayansi umesema virusi vya HIV vinapungua makali kadri muda unavyoenda. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford wamegundua hilo baada ya kuwachunguza mamia ya wanawake nchini Botswana.
Kufahamu zaidi , Jo-Angeline Kalambo, mtaalam wa afya ya jamii katika shirika la Global Fund linaloshughulikia ukimwi, malaria na kifua kikuu, alihojiwa na BBC Dira TV mwanzo akitoa maoni yake kuhusu utafiti huo.

UNAPODHANI UMELAMBA BINGO


 Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

HIV 'YAPUNGUA MAKALI'

MUHAMMAD: JINA LA KIUME LINALOTUMIKA ZAIDI UINGEREZA

AJERUHIWA KWA CHOO CHA KUIBUKA ARDHINI

Tuesday, 2 December 2014

HIV 'YAPUNGUA MAKALI'



HIV

Virusi vya HIV vinaanza kupungua makali, kulingana na utafiti mkubwa wa kisayansi.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford kinaonyesha virusi hivyo “vinafubazwa” huku vikiendana na mfumo wa kinga wa miili yetu.

Utafiti huo unasema maambukizi ya HIV yanachukua muda mrefu zaidi kusababisha Ukimwi na mabadiliko ya virusi huenda ikasaidia jitihada za kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo.

Baadhi ya wataalamu wa virusi wanapendekeza virusi hivyo mwisho “vitakuwa havina athari yoyote” kwa jinsi vinavyoendelea kuwepo.

Zaid ya watu milioni 35 duniani wameathirika na virusi vya HIV na ndani ya miili yao mapambano makali huwepo baina ya mfumo wa kinga na virusi hivyo.

AL-SHABAB YAUA TENA KENYA


Protests in Nairobi, 25 November 2014
Maandamano makubwa yalifanyika wiki iliyopita kufuatia shambulio katika basi karibu na eneo hilo hilo

Wapiganaji wa Al-Shabab wamewaua watu 36 wengi wakiwa Wakristo wanaofanya kazi kwenye machimbo karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa nchi ya Kenya.

Washambuliaji hao wenye makao makuu yao Somalia waliwatenganisha Waislamu na wasio waislamu na kuwapiga risasi za kichwa Wakristo, kulingana na wakazi wa eneo hilo.

Awali, mtu mmoja aliuawa katika baa maarufu kwa wasio Waislamu kwenye wilaya jirani.

Al-Shabab iliwaua watu 28 katika shambulio la basi lililowalenga wasio waislamu katika eneo hilo hilo wiki iliyopita.

Shambulio kwa wachimbaji hao lilifanyika siku ya Jumanne.

Walioshuhudia walisema watu hao walikamatwa saa sita za usiku, wakiwa wamelala kwenye maturubali katika machimbo hayo.

Shambulio hilo lilifanyika ormey, kilomita 15 kutoka mji wa Mandera.

Mtu mmoja aliyetembelea eneo hilo aliiambia BBC baadhi ya waliouawa inaonyesha kama walilazwa chini, na kupigwa risasi kichwani.

Wengine wanahisi maturubali ya wafanyakazi hao yalimiminiwa risasi.

Al-shabab imesema imehusika na mauaji hayo.