Friday, 5 December 2014

RAIS KENYATTA WA KENYA AFUTIWA MASHTAKA NA ICC


Uhuru Kenyatta

Waendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC mjini the Hague wamefuta mashataka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yakimkabili Rais Uhuru Kenyatta.

Akishtakiwa kwa kuhusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008 ambapo watu 1,200 walifariki dunia.

Bi Kenyatta, aliyekana mashtaka hayo, alisema alihisi “amefutiwa lawama.”

Ofisi ya waendesha mashtaka ilisema serikali ya Kenya ilikataa kukabidhi ushahidi ulio muhimu katika kesi hiyo.

Bw Kenyatta aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa alikuwa na “furaha” kufuatia kufutwa kwa mashtaka hayo.

Uhuru Kenyatta (l) and William Ruto (r)
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto

 "Nafsi yangu iko safi kabisa," alisema, akiongeza ujumbe mwengine kuwa kesi yake “iliharakizwa kupelekwa huko bila uchunguzi wa kutosha”.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohamed alisema serikali yake itaendelea kushughulikia kesi nyingine mbili kama hizo zifutwe moja ikimhusu Naibu Rais William Ruto.

Thursday, 4 December 2014

KUTOA NI MOYO USAMBE NI UTAJIRI

  

      Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

RAIS MUGABE AHAMAKI JUU YA 'JARIBIO LA KUMWUUA'

'MARUFUKU' KUTUMIA JINA SAWA NA LA RAIS

RAIS MUGABE AHAMAKI JUU YA 'JARIBIO LA KUMWUUA'



Zimbabwean President Robert Mugabe delivers his speech during the official opening of the Zanu-PF congress in Harare on 4 December 2014

Rais wa Zimbabwe amezungumzia hasira zake juu ya naibu wake walio kwenye mzozo Joyce Mujuru kwa madai ya kula njama ya kumwuua kiongozi huyo na kumtuhumu kuwa mwizi.

Akizungumza katika mkutano wa chama tawala cha Zanu-PF, Robert Mugabe alisema atawashughulikia maafisa wote mafisadi.

Kutokuwepo Bi Mujuru kwenye mkutano huo kunaashiria kuwa “anaogopa” alisema Bw Mugabe.

Siku za hivi karibuni mwanachama wa Zanu-PF aliyefurumushwa Rugare Gumbo aliiambia  BBC kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 90 amebadilisha “kabisa” chama hicho kuwa “mali yake binafsi”.

Bw Mugabe alimlenga Bi Mujuru ili ‘kumpembejea’ mke wake Grace, aliyekuwa msemaji wa Zanu-PF aliongeza.

Bi Mujuru, ambaye hivi karibuni alikana madai hayo, alikuwa ana nafasi kubwa ya kumrithi Bw Mugabe, ambaye alikuwa naye sambamba wakati wa kupigania uhuru wa Zimbabwe kutoka kwa wazungu walio wachache.

Hatahivyo, ndoto zake zilianza kuyumba baada ya Bi Mugabe kuingia kwenye siasa mwaka huu, na kumshutumu kwa kupanga jaribio la kumwuua mumewe.

Mkutano huo, unaofanyika mjini Harare, unatarajiwa kumchagua mke huyo wa rais kuwa kiongozi wa umoja wa wanawake wa Zanu-PF.

Wednesday, 3 December 2014

'MARUFUKU' KUTUMIA JINA SAWA NA LA RAIS


This undated picture released from North Korea's official Korean Central News Agency (KCNA) on January 12, 2014 shows North Korean leader Kim Jong-Un

Korea Kaskazini inaripotiwa kuamuru mtu yeyote mwenye jina sawa na la kiongozi wake Kim Jong-un, kubadili mara moja., kulingana na vyombo vya habari vya Korea kusini.

Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Korea Kusini zinasema jina hilo limezuiliwa kupewa  kwa watoto wanaozaliwa kuanzia sasa.

Mbali na hilo na wale wanaolitumia, tayari wanalazimika kubadili vyeti vyao vya kuzaliwa na nyaraka za makazi yao.

Amri hiyo ilitolewa tangu mwaka 2011 lakini ndio kwanza sasa imetolewa hadharani.

Karibu asilimia ishirini ya familia za Kikorea zina jina la Kim na Jong-un.

Japo maelekzo yamenukuliwa kuwa  hatua hiyo ni hiari, waandishi walisema wachache Korea Kaskazini wataacha kutii.

KESI INAYOMKABILI RAIS KENYATTA ITAENDELEA?


Kenya's President Uhuru Kenyatta leaves after attending the Mashujaa Day (Hero's Day) celebrations at the Nyayo National Stadium in Nairobi, on 20 October 2014.
Bw Kenyatta alichaguliwa mwaka 2013, licha ya kukabiliwa na mashtaka ICC

Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC imempa kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda muda wa wiki moja aondoe mashtaka dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Kama si hivyo ametakiwa awasilishe taarifa kuelezea ikiwa ana ushahidi wa kutosha kuendeleza kesi hiyo.
Mahakama hiyo imekataa ombi la kiongozi huyo wa mashtaka kuiahirisha kesi dhidi ya Bwana Kenyatta ili kumpa muda kutafuta ushahidi zaidi. 

Bw Kenyatta alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi kufikishwa rasmi mahakamani tangu kushtakiwa mwaka 2012 kwa uhalifu dhidi ya binadamu, jambo analokataa.

Upande wa mashtaka mara kwa mara umeomba muda zaidi kujenga hoja ya kesi hiyo.
Wamesema mashahidi wamekuwa wakihongwa na kutishwa, na serikali ya Kenya imekataa kukabidhi nyaraka muhimu zinazotakiwa.

Bw Kenyatta amekana kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wenye utata mwaka 2007 ili kuzuia ushindi wa kwa wakati ule Rais Mwai Kibaki na kusema kesi ya ICC ni ya kisiasa.

MAHOJIANO YA BBC KUHUSU HIV 'KUPUNGUA MAKALI'

     
Utafiti mkubwa wa kisayansi umesema virusi vya HIV vinapungua makali kadri muda unavyoenda. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford wamegundua hilo baada ya kuwachunguza mamia ya wanawake nchini Botswana.
Kufahamu zaidi , Jo-Angeline Kalambo, mtaalam wa afya ya jamii katika shirika la Global Fund linaloshughulikia ukimwi, malaria na kifua kikuu, alihojiwa na BBC Dira TV mwanzo akitoa maoni yake kuhusu utafiti huo.

UNAPODHANI UMELAMBA BINGO


 Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

HIV 'YAPUNGUA MAKALI'

MUHAMMAD: JINA LA KIUME LINALOTUMIKA ZAIDI UINGEREZA

AJERUHIWA KWA CHOO CHA KUIBUKA ARDHINI