Thursday, 25 December 2014

BINTI ADAI WAZAZI WALIMKABIDHI KWA BOKO HARAM



Nigerian police present 13-year-old girl to reporters in Kano. 24 Dec 2014

Mtoto wa kike kutoka Nigeria mwenye umri wa miaka 13 ameelezea namna wazazi wake walipomkabidhi kwa wapiganaji wa Boko Haram ili ajitolee mhanga.

Binti huyo, akizungumza na waandishi wa habari iliyoandaliwa na polisi, alisema alipelekwa mjini Kano ambapo mabinti wengine wawili walilipua mabomu yao.

Takriban watu wanne walikufa katika shambulio la Desemba 10. Binti huyo alikamatwa, bado akiwa amevaa mabomu, polisi walisema.

Takriban watu 2,000 walikufa kutokana na mashambulio waliohusishwa nao wapiganaji hao mwaka huu.

Binti huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wazazi wake walimpeleka kwa wapiganaji hao waliojificha msituni karibu na mji wa Gidan Zana katika jimbo ka Kano kaskazini mwa nchi hiyo.

Alisema mmoja wa viongozi wa kundi hilo alimwuuliza kama anajua maana ya kujitolea mhanga kutumia bomu.

"Walisema, 'Utaenda peponi ukifanya hivyo.' Nikasema 'Hapana siwezi.' Wakasema watanipiga risasi au kunirusha kwenye gereza."

Binti huyo hatimaye alisema  alikubali kushiriki kwenye shambulio hilo lakini "hakuwahi kuwa na nia ya kufanya hivyo".

Alisema alijeruhiwa baada ya mmoja wa mabinti hao kujilipua na kuishia hospitali ambapo mabomu hayo yaligunduliwa.

Haikuwa rahisi kuthibitisha taarifa ya binti huyo. Waandishi walisema hapakuwa na wakili wowote wakati wa mkutano hao wa waandishi wa habari.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

OMBAOMBA APIMWA IMANI, KAFAULU?



Gesture ... with an agenda: YouTube star Josh Paler Lin (right) gives $100 cash to a homeless man in LA, with the intention of following the beggar afterwards

Mtu mmoja kutoka California aliyedhamiria kuona ombaomba atafanya nini akigaiwa dola 100, alipatwa na mshangao mkubwa baada ya hatua hiyo.

 Josh Paler Lin maarufu katika mtandao wa YouTube — ambaye amejulikana zaidi kwa video zake za maskhara –aliweka video hiyo siku ya Jumatatu, inayoanza akimpa ombaomba huyo pesa hizo mjini Los Angeles, halafu wakianza kumfuatilia kisiri mtu huyo huku wakimrekodi.

Ombaomba huyo, anayejulikana tu kwa jina la Thomas alipoingia kwenye duka linalouza pombe, Paler Lin aliamini kashapata jibu alilolitaka.

Hatahivyo, Thomas aliingia humo kununua chakula, halafu kuelekea eneo ambalo ombaomba wengine wengi hukusanyika na kuanza kuwagawia chakula hicho.

'Sikutarajia kurekodi kitu kama hichi... kusema ukweli, nilidhani ingekuwa mwanzo wa kufichua tabia za ombaomba,’ Paler Lin aliandika kwenye ukurasa wake wa YouTube.

'Nina furaha sana nimeweza kushuhudia na kurekodi tukio la kipekee.

'Sijamsaidia tu ombaomba, lakini nimeweza kukutana na binadamu wa aina yake na rafiki.

'Tulikuwa tukimfuatilia kwa takriban saa moja nzima.'

Thomas alimwambia Paler Lin aliacha kazi yake ili kuwatunza wazee wake, lakini baada ya wote wawili kufariki, hakuwa na uwezo wa kulipia nyumba na kujikuta yupo mtaani.

Paler Lin pia ameanzisha ukurasa maalum wa kukusanya fedha kwenye  Indiegogo kwa ajili ya Thomas, kwa matumaini ya kupata $10,000 kwa ajili yake.

Ukurasa huo tayari umeshachangisha zaidi ya dola 35,000.

Kutazama video hiyo bonyeza hapa http://dailym.ai/1rk67Qr

Chanzo: dailymail.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu







Wednesday, 24 December 2014

GEORGE HW BUSH APELEKWA HOSPITALI



 File photo of George H W Bush, July 2013
Aliyekuwa rais wa Marekani George Bush Senior amepelekwa hospitali baada ya kukosa pumzi, msemaji wake alisema.

Bw Bush, mwenye umri wa miaka 90, alipelekwa hospitali ya Houston Methodist kama kuangaliwa na “atafanyiwa uchunguzi”, pia tena uangalizi tu, alisema Jim McGrath.

Miaka miwili iliyopita, Bw Bush alitibiwa kwenye hospitali hiyohiyo kwa zaidi ya miezi miwili kwa maradhi yanayohusiana na mapafu na kifua na mengineyo.

Alikuwa rais kutoka mwaka 1989 hadi 1993.

Ni rais mzee kuwa hai Marekani na mkongwe miongoni mwa wapiganaji wa Vita Kuu vya Kwanza Vya Dunia.

Kwa sasa hawezi tena kutumia miguu yake. Mtoto wake wa kiume George W Bush alikuwa rais kuanzia mwaka 2001 hadi 2009.

Tuesday, 23 December 2014

MUUZAJI 'KINARA' WA PEMBE ZA NDOVU AKAMATWA TZ



African elephant

Mfanyabiashara wa Kenya anayeshukiwa kuhusika na ujangili wa kimataifa wa pembe za ndovu amekamatwa nchini Tanzania.

Polisi walisema Feisal Mohamed Ali alihusishwa na mauzo ya tani tatu za meno ya tembo mjini Mombasa nchini Kenya.

Bw Ali alijificha kwa miezi kadhaa na alikuwa katika orodha ya Shirika la Polisi la Kimataifa, Interpol la wanaosakwa kwa uuzaji haramu wa pembe za ndovu.

Uwindaji haramu wa tembo umeongezeka barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni, sababu moja ikiwa imechochewa na China kutaka bidhaa hiyo.

Mwezi Juni, polisi wa Kenya walifanya uvamizi na kugundua pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya tembo 100 waliouawa.

Tangu wakati huo Ali amekuwa mbioni, kulingana na shirika la habari la AFP, na kuorodheshwa kama “mhalifu wa kimazingira” na Interpol kabla ya kukamatwa.

Shirika la Wanyamapori Kenya limesema wawindaji haramu wameua tembo 142 nchini humo kwa mwaka huu pekee.

Msemaji mmoja alisema idadi hiyo imepungua kutoka 302 mwaka jana, sababu moja ikiwa ni  kutokana na sheria za kupinga uwindaji haramu.

Lakini nchini Tanzania, Bw Ali alipokamatwa, takriban tembo 10,000 waliuawa mwaka jana.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


Monday, 22 December 2014

ESCROW YAMTOA PROF TIBAIJUKA, MUHONGO KIPORO



Rais wa Jamhuri wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kutengua uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kijiridhisha kuwa amekiuka maadili ya utumishi wa Umma kwa kuingiziwa fedha kiasi cha Sh1.65bilioni kwenye akaunti yake binafsi.

Rais Kikwete ametangaza kufukuzwa kazi kwa waziri huyo leo alipokuwa anazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa, na baada ya kutangaza kufukuzwa kwake maelfu ya wazee waliohudhuria kwenye mkutano huo walipiga kelele za kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake.

Rais kikwete amesema miongoni mwa mapendekezo ya Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Escrow Tegeta yaliyofikishwa kwenye Serikali ni pamoja na kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Rais Kikwete amesema baada ya uchunguzi wa vyombo husika viliweza kubaini kuwa kiasi cha Sh1.65bilioni kiliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Profesa Tibaijuka, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa Umma.

“Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba atupishe ili tuweze kuteua waziri mwingine kwani viashiri vyote vinaonyesha kuwa alikiuka kanuni na sheria ya maadili ya Umma,” anasema Rais Kikwete.

Aidha Rais Kikwete amesema katika suala la Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo analiweka kiporo maana bado hajapata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha, hivyo pindi atakapopata ufafanuzi na kujiridhisha ataujulisha umma .

Amesema kuhusu suala la bodi ya Tanesco hana shida nalo kwa sababu tayari bodi hiyo imeshamaliza muda wake hivyo ni kama imekwishajifuta yenyewe, na kuongeza kuwa tayari Ikulu imeshapewa taarifa za kumtaka achague bodi nyingine, hivyo ndani ya siku chache bodi mpya ya Tanesco itatangazwa.

Amesema suala la Katibu Mkuu wa Nishati na Madini na viongozi wengine wa utumishi wa Umma ambao wametajwa katika sakata hilo tume ya maadili, Taasisi ya Kuzuia na Kupapambana Rushwa (Takukuru) pamoja na jeshi la polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wao, na ikithibitika kuwa walikiuka maadili yao ya kazi sheria stahiki zitachukuliwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz

MIRABA MINNE NDANI YA KISANDUKU

    

Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

UCHUMI WA ZIMBABWE WAZIDI KUSUASUA