Sunday, 4 January 2015
MSHTUKO: KIFO CHA MTOTO WA RAILA ODINGA
Fidel Odinga, mtoto mkubwa wa kiume wa kiongozi wa chama cha Cord cha Kenya, Raila Odinga, alikutwa siku ya Jumapili asubuhi nyumbani kwake Windy Ridge, Karen baada ya kurejea usiku alipotoka na rafiki zake.
Mwili wa mtoto huyo wa Raila ulikutwa kitandani. Polisi walisema mpaka sasa haijajulikana chanzo cha kifo chake.
Aliyezaliwa mwaka 1973, marehemu Fidel alimwoa mwanamke kutoa Eritrea, Getachew Bekele,ambaye amezaa naye mtoto mmoja.
Fidel alikuwa mtoto mkubwa katika familia ya watoto wanne Rosemary, Raila Junior na Winnie.
Taarifa ya kifo chake tu kilipojulikana, ujumbe wa kutoa pole ulimiminika kwenye mitandao ya kijamii.
Kurasa za Facebook zikafunguliwa na kusababisha wafuasi wengi kuzifuata saa chache baada ya kifo chake.
Chanzo: nation.co.ke
Imetafsiriwa na mwandishi wetu
SELENA GOMEZ AZUA KITAHANANI MSIKITINI
Selena Gomez alizua kizaazaa wiki hii baada ya kuonyesha kiwiko chake alipotembelea msikiti – hatahivyo ameitoa picha hiyo baada ya kujikuta akikosolewa na wengi.
Alipigwa picha hiyo alipozuru msikiti mkubwa wa Sheikh Zayed, na alijistiri mwili mzima kwa ajili ya ziara hiyo.
Lakini ilipokuja wakati wa kupiga picha, Selena aliachia kiwiko na sehemu ya mguu hadharani.
Sheria za msikiti huo ziko wazi kuwa sketi zote lazima zifunike mpaka kiwiko, na unakataza ‘tabia zozote za kukaribiana ‘.
Mtu mmoja aliandika: "Kama nia yao ilikuwa kujifunza Uislamu wasingesimama kama wamesimama nje ya bustani.
"Nampenda Selena Gomez lakini kufanya jambo kama hili kunanifanya nisiwe mshabiki wake tena."
Mwengine aliongeza: "Si chuki. Lakini angetakiwa kuwa makini zaidi kuhusu misikiti. Ile sehemu ni takatifu na eneo la kuswali. Si sehemu ya kustarehe na kuchukua picha.
Lakini wapo wengine waliomtetea nyota huyo, mmoja akiandika: "Sio kwamba wamewavunjia heshima. Maelfu ya watu hutembelea msikiti huo wa Sheikh Zayed huko Abu Dhabi.
"Ni sehemu ya ibada, ndio najua, lakini Mungu hajawahi kukataza watu wa dini nyingine kuingia msikitini. Kwahiyo tafadhali heshimu kuwa walitaka kujua zaidi kuhusu Uislamu na uzuri wa dini hiyo."
Selena Gomez na muigizaji na mwimbaji kutoka Marekani ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa muimbaji maarufu Justin Bieber.
Chanzo: www.mirror.co.uk
Imetafsiriwa na mwandishi wetu
KIFUNGO KWA KUMDHALILISHA RAIS KENYATTA
Okengo alikubali kosa la kumdhalilisha Rais Kenyatta |
Mwanafunzi wa mwaka wa nne Chuo Kikuu Kenya amehukumiwa mwaka mmoja jela kwa kumdhalilisha Rais Uhuru Kenyatta kwenye mtandao wa kijamii.
Alan Wadi Okengo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anajulikana pia kwa jina la lieutenant Wadi, lazima alipe faini ya $2,200, au atumikie kifungo cha mwaka mwengine wa pili.
Ametiwa hatiani pia kwa kauli za chuki, baada ya kusema watu kutoka kabila la Kikuyu ambalo ndilo alilotoka rais huyo watengwe katika baadhi ya sehemu nchini humo.
Blogger maarufu alifunguliwa mashtaka hivi karibuni baada ya kumwita Bw Kenyatta "adolescent president".
Kenya ina wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii na mwandishi wa BBC nchini humo alisema kesi hiyo imezua mjadala mzito wa kipi kinaruhusiwa kwenye mitandao hiyo.
Mwandishi huyo alisema watu wengi wanahisi Okenga alivuka mipaka, kwa kuwa kauli zake zilikuwa na chuki binafsi na hazikutakiwa kuchapishwa.
Okenga alikiri makosa yote mawili, kauli za chuki na kumdhalilisha mkuu wa nchi.
Gazeti la Daily Nation kupitia mtandao wao limeripoti kuwa alikamatwa akiwa anajaribu kukimbia nchini humo.
UKIPUNGUA, 'MINYAMA UZEMBE' HUENDA WAPI?
Kuwa na mwili wenye unene wa kupindukia ni tofauti na kuwa na
uzito mkubwa kuliko kawaida ingawa watu wengi huchanganya mambo haya
mawili na kufikiri kuwa ni jambo moja.
Unene wa kupindukia unatokana na kuwa na mafuta mengi mwilini ambayo yanasababisha mtu kuwa na nyama nyingi ambazo wengine huziita “minyama uzembe” na kitambi.
Lakini uzito mkubwa wa mwili unaweza kutokea pale mtu anapokuwa na misuli mikubwa, mifupa mikubwa, maji mengi mwilini pamoja na mafuta. Baadhi ya magonjwa na matumizi ya dawa pia yanaweza kuchagia mtu kuwa na uzito mkubwa.
Watu wenye tatizo la tezi shingo linalofanya kazi zake chini ya kiwango wanaweza kukabiliwa na tatizo hili. Matumizi ya dawa kama vile baadhi ya vidonge vya uzazi wa mpango na dawa za magonjwa ya akili, pia yanaweza kusababisha tatizo la mwili kuwa na uzito mkubwa.
Wanasayansi wa afya wamekuwa wakieleza kuwa kuna uhusiano mkubwa na wa karibu sana kati ya unene wa kupindukia na magonjwa ya moyo, kiharusi, kupanda kwa shinikizo la damu, saratani za aina mbalimbali, kisukari, kukoroma wakati wa usingizi, maumivu ya mgongo na uvimbe wa maungio yaani baridi yabisi.

Kutokana na kupendelea
kuwa na umbo la kuvutia na sababu za kiafya, watu wengi hulazimika
kupunguza unene na uzito wa miili yao.
Lakini maswali ya msingi ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu kupungua kwa unene wa mwili ni pamoja na njia ipi iliyo bora ya kupunguza uzito au unene?
Lakini maswali ya msingi ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu kupungua kwa unene wa mwili ni pamoja na njia ipi iliyo bora ya kupunguza uzito au unene?
INDIA KUCHUNGUZA UTUMIAJI WA CHOO
Serikali
ya India imetangaza kuwepo na mpango wa kitaifa wa kuangalia iwapo watu
wanatumia vyoo.
Ni
sehemu ya mpango wa taifa kufanya nchi hiyo iwe safi, uliozinduliwa na waziri
mkuu mpya, Narendra Modi, miezi mitatu iliyopita.
Wakaguzi
wa usafi watafanya uchunguzi nyumba hadi nyumba wa namna watu wanavyotumia
vyoo, na wakihifadhi matokeo kwenye simu za mkononi na vifaa vengine vya
kiteknolojia.
Taarifa
ya serikali ilisema hatua hiyo inaadhimisha utafiti wa awali ambao ulisimamia ujenzi
wa vyoo.
Serikali
hiyo ilisema imejenga vyoo nusu milioni tangu mwezi Oktoba.
Hatahivyo,
Umoja wa Mataifa unaamini takriban nusu ya watu nchini India hawako radhi
kutumia vyoo vya ndani, matokeo yake ni kuibuka kwa maradhi tele yanayohusu
uchafu na vifo vya mapema.
Chanzo:
Reuters na AFP
Subscribe to:
Posts (Atom)