Thursday, 15 January 2015

CHARLIE HEBDO: MAGAZETI YA AFRIKA YAOMBA RADHI


Apology published by Kenya's The Star on 15 January 2015
Gazeti la The Star lina ushawishi Kenya

Magazeti mawili ya Afrika yameomba radhi kwa kuchapisha ukurasa wa juu wa jarida la  Charlie Hebdo likiwa na kibonzo cha Mtume Muhammad, baada ya wasomaji wa Kiislamu kulalamika.

Gazeti la Kenya The Star na The Citizen la Afrika kusini yamesema yanajuta kwa kuwakosea Waislamu.  

Chombo cha kudhibiti vyombo vya habari Kenya kimemwita shaurini mmiliki wa gazeti la Star baada ya kulishutumu kukiuka sheria ya kuheshimiana.

Nchini Senegal, serikali imepiga marufuku usambazaji wa jarida hilo la Charlie Hebdo.

Gazeti la pili la Kenya, Business Daily, nalo limechapisha ukurasa huo wa mbele wa jarida hilo la Ufaransa.

Katika toleo lake la Alhamis asubuhi, The Star lilisema wasomaji wengi wa Kiislamu wamelalamika juu ya “uzalishaji mdogo” wa ukurasa wa mbele wa Charlie Hebdo siku ya Jumatano.  

Wakiomba radhi, gazeti hilo, la tatu kwa ukubwa Kenya, limesema “linajuta sana kwa kosa na uchungu uliosababishwa na picha hiyo”.

HUDUMA YA AFYA ANGANI YAZINDULIWA KENYA



President Kenyatta at the launch of an air ambulance service in Nairobi on 14 January 2015

Kenya imezindua huduma yao ya kwanza ya gari la wagonjwa la angani itakayosaidia kuwahamisha majeshi ya usalama waliojeruhiwa kwenye mapambano.

Rais Uhuru Kenyatta alisema huduma hiyo ni muhimu kuhakikisha wanapata tiba haraka.

Huduma hiyo inatarajiwa kuwapa matumaini zaidi wafanyakazi wa masuala ya usalama wanaokabiliwa na vitisho vya mara kwa mara, mwandishi wa BBC alisema.

Baadhi ya wanajeshi na polisi wametoka damu mpaka kufa au kufa kutokana na ukosefu wa maji maeneo ya vijijini nchini Kenya kwasababu ya muda mrefu unaotumika kuwafikisha hospitalini.

Serikali ya nchi hiyo sasa imefanya makubaliano na Shirika la Msalaba Mwekundu, Red Cross na kampuni binafsi ya madaktari wasio na mipaka ya AMREF kutoa huduma za helikopta na magari wanapopata tu simu za kuhitaji huduma hiyo haraka.

 Huduma hiyo pia itatolewa kwa wafanyakazi wa serikali, hasa wale wanaofanya kazi kwenye nyanja ya usalama vijijini na walio na vifaa vichache vya kutolea matibabu.

Kundi la Kisomali la al-Shabab limeongeza mashambulio nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni.


Wednesday, 14 January 2015

ZAIDI YA MIILI 100 KUPATIKANA MTO GANGES, INDIA


 

Serikali nchini India inachunguza kupatikana kwa zaidi ya miili mia moja, iliyokutwa katika mto Ganges kaskazini mwa nchi hiyo.

Hakuna tuhuma za uhalifu zinazofikiriwa, lakini badala yake inaonekana miili hiyo, ambayo sasa imeharibika sana, iliachwa ielee katika mto huo, baada ya familia zao kushindwa kuwachoma moto kama taratibu za Wahindu zinavyotaka.

Waandishi wa eneo hilo walisema licha ya maiti kuonekana kwenye mto huo mara kwa marasi kawaida kuona miili ya watu wengi sehemu moja.

Kuna wasiwasi kuwa inasababisha matatizo makubwa kiafya na kuna taarifa kuwa hata wafanyakazi wa kufanya usafi waliokuwa wakitoa miili sasa wamekataa kuendelea.

Inasemwa kuwa idadi kubwa ya maiti zilizokuwa zikielea ni za watoto.

Chanzo: cbsnews.com

TOTO TUNDU - MKUKI KWA NGURUWE .....

    

Vimbwanga vya WhatsApp

WAPEWA CHAKULA BURE KWA KUWA NA 'SURA NZURI'



The judging panel
Majaji wakiamua nani ana sura nzuri zaidi wa kupewa chakula cha bure


Wateja katika mkahawa mmoja unaofanya mapishi ya Korea, Zhengzhou, katika jimbo la Henan, wanapewa chakula cha bure iwapo atapigiwa kura kuwa miongoni mwa wenye sura nzuri.

Gazeti la mtandaoni la China Daily lilisema kundi la watu likifika kula hupigwa picha wanapowasili.

Hata hivyo, si wafanyakazi wa mkahawa huo uliopo China wanaoamua nani ana sura au mtindo mzuri wa nywele.

Kazi hiyo hufanywa na wafanyakazi kutoka kliniki moja ya upasuaji ya kubadilisha maumbile, ambao hutazama picha hizo na kuchagua tano bora.

Baadhi ya watu nchini humo wamefurahishwa na kupewa chakula bure lakini wengine walisema ni kuwavunjia watu heshima.

Tuesday, 13 January 2015

TOVUTI MPYA YAUNDWA KUFICHUA SIRI ZA AFRIKA



 Young Ivorian learn how to use a computer on 22 April 2004 in Abidjan

Tovuti  inayofichua mambo yaliyojificha uliolilenga hasa bara la Afrika umeanzishwa, ukikusudia kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa barani humo.

Imeahidi kuficha utambulisho kwa yeyote atakayetaka kutoa taarifa za siri kwa magazeti huru.

Tovuti hiyo - inayoitwa afriLeaks - imesema inataka kuwaunganisha wafichuaji maovu na kundi la waandishi wa habari wanaofichua  na kuandika habari za uchunguzi, na pia kutoa mafunzo maalum kwa waandishi hao.

Makundi ya vyombo vya habari Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Botswana tayari washajiunga na mtandao huo.  

Afrika limekua kwa kasi kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni lakini idara nyingi zinabaki kuwa dhaifu, na rushwa inakisiwa kuigharimu bara hilo mabilioni ya dola kila mwaka.

Afrileaks, iliyoundwa kutokana na vyombo vya habari 19 na makundi ya kutetea haki za binadamu, imedhamiria “kueleza ukweli “.

Miongoni mwa 19 mengi ni magazeti likiwemo la Afrika kusini Mail & Guardian, Daily Nation la Kenya na  Premium Times la Nigeria.

Nia hasa ni kuwafichua wanasiasa na wafanyabiashara barani humo wanaotumia vibaya madaraka yao.

Chanzo: theguardian.com