Tuesday, 24 February 2015
INDONESIA: HUKUMU YA KIFO KWA 'WAGENI'
Rais wa Indonesia Joko Widodo alisema mataifa ya kigeni yasiingilie haki ya nchi yake kutumia hukumu ya kifo.
Anapata shinikizo kutoka viongozi wa Australia, Brazil na France, ambao raia wake ni miongoni mwa watu 11 wanaokabililiwa na hukumu ya kifo kwa makosa ya kufanya biashara ya dawa za kulevya.
Bw Widodo alisema kuwa hukumu hiyo kwa kufyatuliwa risasi itatekelezwa.
Awali, mahakama ya Jakarta ilitupilia mbali rufaa ya raia wawili wa Australia waliyoombewa na rais wao ya kupunguziwa hukumu.
Indonesia ni moja ya nchi yenye adhabu kali mno duniani dhidi ya biashara ya dawa za kulevya.
Ilifufua hukumu ya kifo mwaka 2013 baada ya kusimamishwa kwa miaka minne na kiongozi mpya Bw Widodo anachukua hatua kali zaidi kuhusu suala hilo.
Mwezi Januari, wauzaji sita wa dawa za kulevya – watano wakiwa raia wa kigeni – waliuawa.
Duru ya pili ya kutekelezwa hukumu hiyo inayohusu watu 11 inatarajiwa kufanyika katika siku za hivi karibuni.
Monday, 23 February 2015
KESI YA BI GBAGBO WA IVORY COAST YAANZA
Aliyekuwa mke wa rais wa Ivory Coast, Simone Gbagbo, amekana kuwa na kosa lolote katika madai ya kuhusika kwenye ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Bi Gbagbo alikuwa akitoa ushahidi kwa mara ya kwanza katika kesi yake huko Abidjan.
Mume wake, ambaye alikuwa rais Laurent Gbagbo, anasubiri kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Alikataa kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi wa rais, yaliyochochea ghasia kwa miezi kadhaa yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.
Pia alisistiza mume wake alikuwa mshindi halali wa uchaguzi badala ya mpinzani wake, Alassane Ouattara, aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi huo.
Polisi walipata kazi ya kuwatenganisha wafuasi na wapinzani wa Gbagbo baada ya mfarakano ulipoibuka nje ya mahakama.
Sunday, 22 February 2015
MBUNGE CANADA ALAUMU KUBANWA NA 'CHUPI'
Mbunge wa Canada alitoa kisingizio cha ajabu kuwahi kutolewa kwa kuondoka bungeni haraka – nguo ya ndani kumbana.
Ilivyoonekana nguo za ndani zilizombana zilimpa ugumu kukaa wakati walipokuwa wakipiga kura, mbunge wa upinzani Pat Martin alimwambia Spika aliyekuwa kamahanika.
Hatahivyo, aliwahi kurudi kupiga kura yake.
Bw Martin alizua vifijo na vicheko bungeni humo baada ya kuelezea sababu za kutoka kwa muda.
"Walikuwa wakiuza chupi za kiume kwa nusu bei na mie nikanunua kadhaa ambazo bila shaka zimekuwa ndogo kwangu. Napata ugumu kukaa kwa hakika.”
Spika wa bunge hilo alisema awali alimwamuru Bw Martin kukaa chini alipotaka kuondoka.
"Sikuelewa ufafanuzi wake wakati huo na sidhani kama naielewa sasa”, alisema.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Friday, 20 February 2015
KIMA ATARAJIWA KUACHIWA URITHI WOTE
Wanandoa wa India waliotengwa baada ya familia zao kutoridhishwa na ndoa yao wameamua kuacha mali zao zote kwa kima wao.
Brajesh Srivastava na mkewe Shabista waliiambia idhaa ya Hindi ya BBC kuwa walikuwa "wapweke kwa miaka mingi" kabla ya kumnunua kima huyo aitwaye Chunmun, mwaka 2005 kwa rupia 500 yaani dola 8.
Wanandoa hao, ambao hawana watoto, wanasema wamemlea kama mtoto wao.
Bw Srivastava ni Hindu na mkewe Mwislamu, na ndoa za imani tofauti bado zina utata katika baadhi ya maeneo India.
Bi Srivastava alisema familia zao zote mbili ziliwatenga baada ya ndoa yao na walikuwa wapweke mpaka walipomnunua Chunmun.
"Wakati huo alikuwa mtoto, alikuwa chini ya umri wa mwezi mmoja, na mama yake alikufa kutokana na umeme," alisema.
Humnywisha Chunmun maziwa, matunda na chakula chochote anachopika. Chumba chake kina feni ambacho hutumika wakati wa joto na ‘heater’ wakati wa baridi.
Wednesday, 18 February 2015
BI HARUSI AOLEWA NA MGENI MWALIKWA KWA HASIRA
Bi harusi
mmoja wa India ameolewa na mmoja wa waalikwa katika harusi yake baada ya bwana
harusi mtarajiwa kupatwa na kifafa na kuzimia.
Ripoti
zilisema bwana harusi huyo mtarajiwa, Jugal Kishore, alikuwa na kifafa na
hakumwambia mtarajiwa wake, Indira na familia ya binti huyo.
Wakati Bw Kishore alipopelekwa hospitali, bi harusi huyo mwenye hasira aliamua kutafuta mume mbadala.
Alimwomba mmoja wa upande wa familia ya shemeji yake, aliyekuwa mwalikwa, kumwoa badala ya mtarajiwa wake. Jambo alilokubali.
Tukio hilo lilitokea mjini Rampur katika jimbo lililo kaskazini mwa India Uttar Pradesh.
Kulingana na gazeti la The Time la India, Bw Kishore, mwenye umri wa miaka 25, alianguka chini mbele ya wageni waalikwa alipotaka tu kumkamata mkono bi harusi wake Indira.
Aliporejea hospitalini, Bw Kishore alimwomba Indira abadili mawazo, akimwambia atabezwa na marafiki na ndugu zake akirudi bila mke, lakini bi harusi huyo alikataa.
Afisa polisi Ram Khiladi aliiambia BBC kuwa awali Bw Kishore na familia yake walikasirishwa na kupeleka malalamiko polisi.
"Lakini kwa kuwa bi harusi huyo kashaolewa, utafanya nini? Familia hizo zimeshatafuta suluhu na wamefuta malalamiko," aliongeza.
Tuesday, 17 February 2015
MTOTO ALBINO AKUTWA KAKATWA MIGUU TANZANIA
Mtoto mdogo albino ambaye hakujulikana alipo tangu siku ya Jumapili amepatikana kaskazini mwa Tanzania, huku miguu yake yote miwili ikiwa imekatwa.
Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na kifo chake.
Awali kulikuwa na hofu kuwa huenda ameuliwa na waganga wa kienyeji wanaopiga ramli.
Polisi walisema Yohana Bahati mwenye umri wa mwaka mmoja alichukuliwa na watu waliovamia nyumba ya mama yake, na kumpiga na panga.
Viungo vya albino, husakwa na waganga wa kienyeji wanaopiga ramli nchini Tanzania.
Nchi hiyo ilipiga marufuku waganga wa kienyeji kuendeleza shughuli zao mwezi Desemba katika jaribio la kuzuia mashambulio na utekajinyara.
Baba wa mtoto huyo, aliyekuwa karibu wakati wa shambulio hilo, anahojiwa, mkuu wa polisi wa kanda hiyo Joseph Konyo aliliambia shirika la habari la AFP.
Subscribe to:
Posts (Atom)