Wednesday 25 March 2015
JEREMY CLARKSON ATOLEWA TOP GEAR YA BBC
Mkataba wa Jeremy Clarkson hautoongezwa baada ya kufanya "shambulio lisilokuwa na uchochezi wowote” kwa msimamizi wa kipindi cha Top Gear, mkurugenzi mkuu wa BBC amethibitisha.
Tony Hall alisema “hakuchukua uamuzi huo kwa uwepesi” na alitambua “itagawanya maoni ya wengi”.
Hata hivyo, aliongeza “alivuka mpaka” na " hawezi kukubaliana na kilichofanyika katika tukio hilo".
Clarkson alisimamishwa kazi Machi 10, kwa kile kilichoitwa “ugomvi” na msimamizi wa Top Gear Oisin Tymon.
Ugomvi huo, uliotokea kwenye hoteli moja huko Yorkshire, inasemwa kuwa ilitokea kwasababu hapakuwepo na chakula cha moto baada ya kufanya kazi siku nzima.
TAKRIBAN WATOTO 500 HAWAJULIKANI WALIPO
Takriban watoto 500 wenye umri wa miaka 11 na chini ya hapo hawajulikani walipo katika mji mmoja Nigeria uliotekwa upya na wapiganaji, aliyekuwa mkazi wa Damasak aliiambia BBC.
Mfanyabiashara mmoja wa mji huo ulio kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa Boko Haram waliwachukua watoto hao walipokimbia.
Majeshi kutoka Niger na Chad waliuteka mji wa Damasak mapema mwezi Machi, na kuzima udhibiti wa mji huo kwa miezi kadhaa na wapiganaji hao.
Jesho la eneo hilo hivi karibuni limekuwa likiisaidia Nigeria kupambana na wapiganaji hao.
Maelfu wameuawa tangu mwaka 2009, wakati Boko Haram ilipoanza mapigano kwa nia ya kuunda taifa la Kiislamu.
Monday 23 March 2015
KENYA YAMWACHIA HURU BIBI WA MIAKA 100
Bibi wa miaka 100 ameachiliwa huru kutoka gereza moja nchini Kenya baada ya kufanyika kampeni ya kitaifa ya kutaka aachiwe.
Margaret Ngima alifungwa katika gereza la Embu wiki iliyopita kwa kutoheshimu mahakama baada ya kushindwa kulipa faini ya dola elfu moja.
Bibi huyo wa mabibi alishutumiwa kwa kupuuza amri ya mahakama katika mgogoro wa ardhi na familia nyingine.
Kesi yake ilizusha hasira kali Kenya, na hatimaye faini yake kulipwa na seneta wa Nairobi Mike Sonko.
Sunday 22 March 2015
WADANGANYIFU 300 WA MITIHANI WAKAMATWA INDIA
Picha hizi zimewatia aibu mamlaka husika nchini India |
Takriban watu 300 wamekamatwa katika jimbo la Bihar nchini India, mamlaka zilisema, baada ya ripoti kuibuka kuwa kulifanyika udanganyifu katika mitihani ya shule.
Wazazi na marafiki wa wanafunzi hao walipigwa picha wakipanda kuta za shule kuwapa majibu.
Wengi waliokamatwa walikuwa wazazi. Takriban wanafunzi 750 walifukuzwa.
Takriban wanafunzi milioni 1.4 wanafanya mitihani katika jimbo hilo la Bihar peke yake – mitihani inayoonekana muhimu kwa kuwapa nafasi ya kujiendeleza katika fani mbalimbali.
Mamlaka bila shaka wameadhirika sana na udanganyifu huo, mwandishi wa BBC alisema, huku tukio hilo likizusha kejeli kubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Wanafunzi walionekana wakinakili majibu kwenye vikaratasi vilivyopenyezwa, na polisi waliokuwa nje ya vituo vya mitihani walionekana wakipewa hongo wageuke wakijifanya hawaoni.
Friday 20 March 2015
Thursday 19 March 2015
MAREKANI YAMWUUA KIONGOZI WA AL-SHABAB
Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kumwuua kiongozi wa al-Shabab, Adan Garar.
Pentagon ilisema mpiganaji huyo alipigwa na kombora kaskazini mwa Somalia siku ya Ijumaa.
Garar alikuwa mshukiwa wa shambulio la Westgate mwaka 2013 mjini Nairobi lililosababisha mauaji ya watu 67.
Marekani iliiamini Garar alikuwa akisimamia harakati “zilizowalenga Marekani na raia wengine wa kigeni”.
Alikuwa mwanachama wa usalama na ujasusi na pia “kiongozi aliyehusika na harakati zote za nje za al-Shabab”, kulingana na Pentagon.
Harakati hizo zilifanyika takriban kilomita 240, magharibi mwa Mogadishu karibu na mji wa Dinsoor.
RAIS WA TUNISIA AAHIDI KUPAMBANA NA UGAIDI
Majeshi ya usalama yalivamia makumbusho hayo kusaidia raia |
Rais wa Tunisia ameapa kupambana na ugaidi “bila huruma”, kufuatia shambulio la bunduki kwenye jumba la makumbusho la Bardo katika mji mkuu Tunis lililoua watu 19
Watalii 17 waliuawa katika shambulio hilo, wakiwemo kutoka Japan, Italia, Cololmbia, Australia, Ufaransa, Poland na Hispania, maafisa walisema.
Raia wawili wa Tunisia, mmoja akiwa polisi, nao pia waliuawa kwenye shambulio hilo la Jumatano.
Majeshi ya usalama yameua wapiganaji wawili lakini wanaendelea kuwasaka washirika wao.
Maafisa walisema zaidi ya watu 40, wakiwemo
watalii na raia wa Tunisia, wamejeruhiwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)