Friday, 24 October 2014

WA KWANZA KUPATA EBOLA MALI AFARIKI DUNIA



A woman's temperature is checked at the Guinea-Mali border, 2 October 2014
Watu kutoka Guinea wanapimwa joto la mwili kabla ya kuingia Mali

Maafisa wa afya wanahofia watu wengi walimgusa muathirika wa kwanza wa Ebola kutoka Mali – mtoto wa miaka miwili.

Hivi karibuni aliwasili Guinea, miongoni mwa nchi zilioathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa huo, na amefariki dunia.

Mtoto huyo alionyesha dalili, zikiwemo kutoka damu puani, wakati akisafiri kwenye basi la umma na kupita miji mbalimbali, lilisema shirika la Afya Duniani (WHO).
 
Watu 43, wakiwemo wafanyakazi wa afya10, ambao walimgusa kwa namna moja au nyingine wametambuliwa na kutengwa.

Mama wa mtoto huyo alifariki dunia nchini Guinea wiki chache zilizopita ambapo ndugu zake wakamchukua mtoto na kwenda naye Mali.

Zaidi ya watu 4,800 wamefariki dunia kutokana na Ebola – hasa Liberia, Guinea na Sierra Leone – tangu mwezi Machi.

RAIS KIKWETE: KAZI YA URAIS SI MASKHARA



Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya urais ni ngumu na anatamani amalize kipindi chake ili awe mtu huru kufanya mambo yake, ikiwamo kilimo, huku akiamini atapatikana Rais bora kuiongoza vizuri zaidi Tanzania kuliko yeye.

Rais Kikwete alisema hayo Beijing alipokuwa akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha mataifa yao nchini China.

Kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Nyumba ya Wageni wa Serikali ya China ya Diaoyutai, Rais Kikwete katika shughuli yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku sita kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais Xi Jinping.

“Ni kweli naona kama muda hauendi kwa kasi ya kutosha ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu, nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha,” alisema Rais Kikwete kwenye mkutano huo baada ya naibu balozi wa Nigeria, Sola Onadipe kuelezea kushangazwa na kauli yake ya kutamani muda wake wa uongozi ufike ili apumzike.

“Kwanza utaratibu huu wa miaka mitano au miaka 10 ni wa kikatiba, ni jambo lililoko katika Katiba yetu na hatuna kishawishi cha kulibadilisha.

“Pili, kazi hii ya urais ni ngumu sana. Kwa hakika nawaonea gere sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi,” alisema Rais Kikwete.

“Lakini pia kuna uzuri katika mfumo huu wa kwetu kwa sababu kila baada ya miaka mitano na hata kama ni baada ya kila miaka 10, anaingia mtu mwingine madarakani akiwa na fikra mpya na mawazo mapya.”
 
Rais Kikwete alisema mfumo huo unamridhisha na hakuna kinachomshawishi abakie madarakani zaidi ya muda wa kikatiba.

DK SALIM A SALIM NA BALOZI MBITA WATUZWA

Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim akipokea Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika kwa Mwaka 2014 kutoka kwa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Smail Chergui.

Tuzo hiyo ilitolewa mjini Arusha pembezoni mwa Warsha ya Tano ya Ngazi ya Juu kuhusu Amani na Usalama Bararani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika inayoendelea mjini humo. Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Balozi Mstaafu na Mpigania Uhuru Mahiri Barani Afrika, Balozi Hashim Mbita.
Balozi Chergui akimkabidhi Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika ya Mwaka 2014, Binti wa Balozi Hashim Mbita, Sheila Hashima Mbita ambaye aliipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Baba yake ambaye hakuweza kufika kutokana na matatizo ya kiafya.
Tuzo hizo zimetolewa kwao kutokana na mchango mkubwa walioutoa Barani Afrika na kwa Umoja wa Afrika ambapo Dkt. Salim alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa OAU kuanzia mwaka 1989 hadi 2001. Kwa upande wake Balozi Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukombozi Barani Afrika chini ya OAU kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 ilipomaliza kazi yake baada ya Uhuru wa Afrika Kusini.

Chanzo: wavuti.com

MGONJWA WA KWANZA WA EBOLA APATIKANA MALI



 Health worker in Mali. Photo: 9 October 2014

Serikali ya Mali imethibitisha kuwepo mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini humo. 

Inasemwa kuwa mtoto wa kike wa miaka miwili amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huo. Hivi karibuni alirejea kutoka Guinea.

Zaidi ya watu 4,800 wamefariki dunia kutokana na Ebola – hasa Liberia, Guinea na Sierra Leone – tangu mwezi Machi.

Wakati huo huo, timu ya wanasayansi imeundwa kutathmini uwezo wa kutumia damu ya wagonjwa waliopona baada ya kuugua Ebola na itumike kama tiba.

Matumaini ni kuwa kinga za asili za mwili ‘antibodies’ zinazotumiwa na mfumo wa kinga mwilini kupambana na Ebola zinaweza kuhamishwa kutoka aliyepona hadi kwa mgonjwa.Utafiti huo utaanzia Guinea.

Vile vile, daktari mmoja kutoka New York aliyerejea hivi karibuni kutoka nchini Guinea ambapo wengi wameathirika na ugonjwa huo amekutwa ana virusi vya Ebola.

Dr Craig Spencer, aliyewatibu wagonjwa waliokuwa na Ebola wakati akifanya kazi na shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF), kuanza kupata homa siku ya Alhamis, siku chache aliporejea.

Ni wa kwanza kugunduliwa na Ebola mjini New York, na mgonjwa wa nne Marekani kukutwa na virusi hivyo.

Thursday, 23 October 2014

TUZO KWA SIMBA WA SERENGETI, TANZANIA



Lions in the Serengeti

Taswira murua ya simba wakiwa wamepumzika kwenye majabali  huko Serengeti imeshinda  tuzo ya picha Bora ya Mwaka ya Wanyamapori  2014 (WPY).

Michael "Nick" Nichols alikuwa akiwafuatailia kwa miezi sita kabla ya kupiga picha hii ya kipekee.


WPY ina miaka 50 sasa, na ni miongoni mwa mashindano makubwa ya picha duniani.

Kupata habari zaidi, bonyeza link ifuatayo, http://www.bbc.co.uk/news/science-environment-29701853

                                                               


HALAHALA! NA CHAGUO LA MKE

   

Vimbwanga vya WhatsApp

WAKASIRISHWA KUZUIWA KUBUSU, ZIMBABWE



The University of Zimbabwe circular
Orodha ya vitu 11 vya utovu wa nidhamu
Kukatazwa kubusiana kwa wanafunzi iliyotolewa na chuo kikuu cha Zimbabwe ‘haina maana’, mwakilishi wa wanafunzi aliiambia BBC.

Vipeperushi kutoka mamlaka za chuo zimesema wale “watakaokutwa kwenye hali zenye utata” kwenye chuo hicho kilichopo mjini Harare watachukuliwa hatua.

“Kwa umri huu kuambiwa huruhusiwi kubusu au kumkumbatia mtu...si sawa. Tsitsi Mazikana alisema.

Chuo hicho hakijasema chochote hadi sasa kuhusu uamuzi huo wa wanafunzi kupinga suala hilo.

Mwanzo wa mwaka wa masomo kulitolewa kama sehemu ya orodha ya “ utovu wa nidhamu unaosababisha mtu kufukuzwa kwenye makazi ya chuo”.

Miongoni mwa masharti 11 pia inakatazwa kula vyumbani.

Wednesday, 22 October 2014

'APIGWA MAWE HADI KUFA' NA AL-SHABAB



Hundreds of newly trained al-Shabab fighters perform military exercises in the Lafofe area 18km south of Mogadishu, Somalia, taken on 17 February 2011

Mahakama ya kiislamu imempiga mawe hadi kufa kijana mmoja, kusini mwa Somalia baada ya kumkuta na hatia ya kubaka mwanamke mmoja, mtandao mmoja umeripoti.

Jaji aliamuru Hassan Ahmad Ali, mwenye umri wa miaka 18, kumlipa fidia ya ng’ombe mwanamke huyo  kabla ya kuuawa, kulingana na ripoti moja ya redio iliyotolewa ya kuhusu hiyo.  

Ali alikana kumbaka mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28, Fadumo Hasan Mohmoud.

Kundi la wapiganaji la al-Shabab linatekeleza sheria kali za kiislamu katika maeneo wanayoyadhibiti.

Mwezi uliopita, mwanamke mmoja alipigwa mawe hadi kufa katika mji wa bandari wa Barawe baada ya mahakama ya kiislamu kumkuta na hatia ya kuwa na waume wanne kwa mpigo.

Ali alikutwa na hatia ya kumbaka Bi Mohmoud huku akiwa kamshikilia bunduki katika kijiji cha Dharuro kwenye eneo la Shabelle, imeripoti kituo cha redio cha al-Furqan kinachoungwa mkono na al-Shabab.