Tuesday, 4 November 2014

WANAWAKE 'RUKHSA' KUPAKA WAIGIZAJI VIPODOZI



A make-up studio in Delhi

Mahakama Kuu ya India imesema hatua ya kuzuia wanawake wenye fani ya kupaka watu vipodozi (make-up artist) kwa miaka 59 katika uwanda wa filamu wa nchi hiyo ni kinyume cha sheria na lazima iondolewe.

Majaji wawili wamesema ubaguzi wa kijinsia ni kukiuka sheria za katiba.

Chama kimoja cha wafanyakazi chenye ushawishi mkubwa nchini humo miaka mingi kimekuwa kikisema wanaume wanahitaji ajira.

Wanawake wanaruhusiwa kufanya kazi kama wanamitindo wa nywele katika utengenezaji wa filamu lakini yeyote atakayejaribu kumpaka muigzaji kipodozi hutishiwa au hata kudhalilishwa.

"Ubaguzi huu utaendelea vipi? Hatuwezi kukubali. Haiwezi kuruhusiwa chini ya katiba yetu. Kwanini mwanamme tu aruhusiwe kupaka watu vipodozi? Alinukuliwa akisema jaji Dipak Misra na UU Lalit katika gazeti la India Express.

“Hatuoni sababu kwanini mwanamke azuiwe kutia watu vipodozi ilimradi ana sifa zinazostahili."


KASHFA YA FEDHA MALAWI, SITHOLE AFUNGWA



US dollars (file photo)

Mahakama ya Malawi imemhukumu aliyekuwa mfanyakazi wa serikali, miaka tisa gerezani na kazi ngumu kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya rushwa maarufu kama “cashgate” nchini humo.

Mhasibu msaidizi Victor Sithole ni afisa wa pili kukutwa na hatia kutokana na suala hilo.

Alikutwa na hatia kwa wizi wa zaidi ya $66,000 (£41,000).

Takriban watu 70 wamekamatwa baada ya uchunguzi wa fedha uliofanyika mwaka jana kudhihirisha kuwa takriban dola milioni 60 zilichomolewa kwenye mfuko wa serikali.

Wafanyabiashara na wanasiasa wanadaiwa kushirikiana na wafanyakazi wa serikali kulipia bidhaa na huduma ambazo hazijawahi kuonekana.

Mwandishi wa BBC alisema kukamatwa kwa Sithole Agosti mwaka jana kulianzisha kwa kile kilichokuja kuitwa “cashgate” – kashfa ya fedha mbaya kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Ilikuja kudhihirika mwezi mmoja baada ya mkurugenzi wa bajeti wa wizara ya fedha kwa wakati huo Paul Mphwiyo kupigwa risasi.

SERIKALI YAKATA RUFAA KESI YA PISTORIUS



Oscar Pistorius pictured on 17 October 2014

Waendesha mashtaka wa serikali nchini Afrika Kusini wamekata rufaa dhidi ya mashtaka na hukumu aliopewa mwanariadha Oscar Pistorius.

Katika nyaraka za rufaa hiyo, waendesha mashtaka wamesema hukumu hiyo inawashangaza kutokana na kuwa nyepesi, isiyofaa na isingeweza kutolewa na mahakama yoyote makini.

Mwezi uliopita, Pistorius alianza kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa mauaji ya kukusudia au kutokukusudia (culpable homicide) ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp.

Alifutiwa mashtaka ya mauaji ya mpenzi wake huyo.

Pistorius anaruhusiwa kuomba kutumikia kifungo cha nyumbani kwa muda utakaobaki baada ya kukaa gerezani kwa miezi kumi.

Chanzo: AP, AFP


MGONGANO WA KISIASA ZAMBIA



Egar Lungu
Edgar Lungu ni kiungo muhimu kwenye chama cha Patriotic Front

Waziri wa ulinzi wa Zambia ambaye ana ndoto za kuwania urais, Edgar Lungu amerejeshwa kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu wa chama tawala, baada ya kufukuzwa siku ya Jumatatu na rais wa mpito Guy Scott.

Waandishi wanasema kumekuwa na mvutano wa madaraka unaochipuka wa nani atakayemrithi aliyekuwa rais Michael Sata, aliyeaga dunia wiki iliyopita.

Katika taarifa, iliyotiwa saini na wote wawili Bw Scott na Bw Lungu, chama tawala, the Patriotic Front, kilisistiza umuhimu wa umoja huku Zambia ikiomboleza kifo cha kiongozi huyo.

Usiku wa Jumatatu, polisi walirusha mabomu ya machozi kusambaza wafuasi wa Bw Lungu waliokasirishwa na kufurumushwa kwake.

Monday, 3 November 2014

UWANJA WA NDEGE WA DAR 'WASHIKA MKIA'

 

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki amesema uwanja wake umechakaa kiasi cha kukosa sifa za kuwa uwanja wa kisasa barani Afrika na dunia.

Kauli ya Malaki imekuja baada ya ripoti ya matokeo ya utafiti wa mtandao wa Sleeping in Airport uliyofanywa 2014 kuonyesha kuwa JNIA inashika nafasi ya nne kwa viwanja duni Afrika.

“Huo ni ukweli usiopingika kwa sababu uwanja ulijengwa zamani na miundombinu yake haikidhi mahitaji ya sasa…. hali ni mbaya,” alisema Malaki.

“Kiwanja kinakabiliwa na tatizo la miundombinu chakavu, vyoo visivyotosheleza na wakati huohuo kuzidiwa na wingi wa abiria, jambo linalosababisha huduma zake kuwa chini ya kiwango.

“Hatuwezi kuwa bora kwa uwanja huu… hebu fikiria uwanja uliojengwa kuhudumia watu milioni 1.2 kwa mwaka, sasa unahudumia watu 2.5 milioni, hapa lazima huduma zitakuwa chini ya kiwango na msongamo utakuwa mkubwa.”

Alisema katika kukabiliana na changamoto ya msongamano, ofisi yake iko katika hatua za kuongeza vizimba vya kugongea hati za kusafiria kutoka saba vya sasa na kuwa 21.

Alisema tayari wameshazungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kuongeza wafanyakazi, pia kuunganisha na kuwa sehemu moja kwa mlango wa abiria wanaowasili na wa ndani, kazi itakayokamilika wiki mbili zijazo.

MJUMBE WA MALAWI 'AMPUUZA' BW MUGABE



Thoko Banda
Thoko Banda amesema hatopuuza wajibu wake wa kutetea haki za bindamu kwasababu ya kazi

Mwanadiplomasia wa Malawi amekataa kazi ya kuwa balozi nchini Zimbabwe kwasababu anapinga udikteta, ameiambia BBC.

"Watu wenye hisia wanatakiwa kuwaunga mkono watu wa Zimbabwe, hasa wale wanaoishi katika hali ya umaskini," alisema Thoko Banda.

Mwaka 2006, iliripotiwa kuwa alimwita Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe "mjinga".

Bw Banda aliiambia BBC hatotumia maneno hayo tena.

Bw Mugabe amekuwa madarakani Zimbabwe tangu mwaka 1980 lakini amekana kukikuka haki za binadamu.

Serikali zote mbili hazijasema lolote kuhusu kauli hiyo ya Bw Banda.

Bw Mugabe anabaki kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika na anaungwa mkono na viongozi wengi wa bara hilo, licha ya kukosolewa sana na nchi za kimagharibi.


UNAPOJIFUNGIA NJE UKIWA 'UTUPU'

 

Vimbwanga vya WhatsApp

Habari nyingine:

Polisi wa Kenya 'wauawa Turkana' http://bit.ly/1o8IKHZ

Ukibakia shule wazawadiwa ng'ombe http://bit.ly/1wr71uy

Mauaji ya kutisha DRC http://bit.ly/1zrplWM

Shairi: Huna mvuto http://bit.ly/1DPWQQA