Saturday, 15 November 2014

PADRI WA UGANDA AKUTWA KABURINI MEXICO



Mass grave in Pueblo Viejo, Mexico, 6 Oct 14

Wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi nchini Mexico wamegundua mwili wa mchungaji wa Kikatoliki kutoka Uganda, ikiwa ni  miongoni mwa mabaki ya miili iliyopatikana kwenye kaburi lenye watu wengi mwezi uliopita.

Mchungaji John Ssenyondo alikuwa hajulikani alipo tangu alipotekwa katika jimbo la Guerrero lililopo kusini-magharibi, miezi sita iliyopita.

Kaburi hilo liligunduliwa na polisi waliokuwa wakiwatafuta wanafunzi 43 ambao walitoweka eneo hilo tarehe 26 Septemba.

Tukio la kupotea au kutojulikana walipo wanafunzi hao wa ualimu lilisababisha hasira kali Mexico na kusababisha msako wa kitaifa.

Vipimo vya asidi nasaba (DNA) vilivyofanywa mapema mwezi huu vimeonyesha miili kwenye kaburi hilo lililojificha karibu na mji wa Ocotitlan – ambapo mabaki ya Mchungaji Ssenyondo yalipatikana – si ya wanafunzi hao.

Mchungaji Ssenyondo alitekwa Aprili 30 na watu wasiojulikana wenye silaha, ambao waliweka vizuizi barabarani na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao.

Alikuwa nchini humo kwa miaka mitano. Vipimo vyake vya meno ndivyo vimesaidia kumtambua.

"Hatujui lengo lao,'' alisema Victor Aguilar, mwakilishi wa dayosisi ya Chilpancingo-Chilapa. "Unajua ukatili umeenea sana katika jimbo hili."

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

RAIS BOUTEFLIKA 'ALAZWA UFARANSA'



 Abdelaziz Bouteflika
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amelazwa katika hospitali moja nchini Ufaransa, kulingana na maafisa wa Ufaransa.

Kiongozi huyo, aliyepooza mwaka jana, kwa sasa anatibiwa Grenoble, vyanzo vya polisi na serikali vimesema.

Maafisa hao hawakutoa maelezo zaidi kuhusu afya ya Bw Bouteflika.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 77 ameiongoza Algeria tangu mwaka 1999, na amekuwa akionekana hadharani kwa nadra sana tangu kuchaguliwa kwake tena kwa mara ya nne mwezi Aprili.

Bw Bouteflika alilazwa hospitalini siku ya Alhamis, kulingana na maafisa wa Ufaransa waliotaka majina yao yahifadhiwe.

'Si kweli'

Gazeti la Ufaransa la Le Dauphine Libere limesema Bw Bouteflika alilazwa kwenye wodi ya masuala ya moyo katika hospitali binafsi kwenye mji ulio kusini-mashariki mwa Ufaransa.

Gazeti hilo liliripoti kuwa ghorofa nzima aliopo yeye lililipiwa ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.

Serikali ya Algeria haijasema lolote kuhusiana na taarifa hizo za kulazwa kwa rais.

Hatahivyo, mkuu wa chama tawala FLN alisema taarifa hizo “si za kweli”, shirika la habari la Reuters lilisema.

Friday, 14 November 2014

WABUNGE NA POLISI WAPURUKUSHANA BUNGENI


 Police officers closing parliament's doors in Cape Town, South Africa in August 2014

Polisi wa kuzuia ghasia Afrika kusini wamepambana na wabunge wa upinzani saa chache baada ya bunge kumfutia rais Jacob Zuma tuhuma za matumizi ya dola milioni 23 za fedha za taifa kukarabati nyumba yake binafsi huko Nkandla.
Waliingilia kati baada ya mbunge wa upinzani Ngwanamakwetle Mashabela kurudia mara kwa mara kumwita Bw Zuma mwizi.
Wabunge wanne walijeruhiwa katika tafrani hiyo iliyotokea katika kikao cha usiku.
Mwezi Machi, mchunguzi wa ufisadi nchini humo alisema Bw Zuma ‘alifaidika kupita kiasi’ kutokana na ukarabati huo.
Mwendesha mashtaka Thuli Madonsela pia alimshutumu kwa kukiuka maadili na kupendekeza alipe fedha zilizotumika kukarabati vitu visivyohusiana na masuala ya usalama huko Nkandla, kwenye jimbo la KwaZulu Natal, lililo na bwawa la kuogelea na mabanda ya mifugo.


Jacob Zuma's Nkandla residence
Nyumba yake binafsi ina bwawa la kuogelea na mabanda kadhaa ya mifugo
Lakini ripoti ya kamati ya bunge – iliyopitishwa na wabunge walio wengi kutoka chama cha African National Congress (ANC) siku ya alhamis- imemsafisha Bw Zuma kuwa na kosa lolote.
Serikali nayo pia ilisema ilibidi fedha hizo kutumika kwa minajil ya usalama.
 

NANI ASEMA UZEE KIKWAZO

  

Vimbwanga vya WhatsApp

Habari nyingine:

MWANAMKE 'AFUFUKA' BAADA YA KUTANGAZWA KUFA http://bit.ly/1BmEsml

BURKINA FASO WAKUBALIANA SERIKALI YA MPITO http://bit.ly/1wwULFd

BURKINA FASO WAKUBALIANA SERIKALI YA MPITO



Talks on the transition in Ouagadougou. 13 Nov 2014

Utaratibu wa serikali ya mpito nchini Burkina Faso umekubalika baada ya kuwepo mazungumzo baina ya viongozi wa kisiasa, kijeshi na kiraia.

Msemaji wa mazungumzo hayo mjini Ouagadougou alisema makubaliano hayo yamekubalika bila kupingwa.

Serikali hiyo ya mpito inatarajia kurejesha nchi katika uongozi wa kiraia na kuandaa uchaguzi mwakani.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Rais Blaise Comapore alipolazimishwa kujiuzulu tarehe 31 Oktoba kufuatia maandamano mazito.

Lt Kanali Isaac Zida alijitangaza kuwa mkuu wa taifa hilo la Afrika magharibi tarehe 1 Novemba kufuatia Rais Compaore kukimbilia nchi jirani ya Ivory Coast baada ya kukaa madarakani kwa miaka 27.

Kulingana na azimio walilokubaliana siku ya Alhamis, rais wa mpito atachaguliwa na kundi maalum litakalohusisha viongozi wa kidini, kijeshi, kisiasa na kitamaduni.

Baada ya hapo rais atamtaja waziri mkuu atatakayeteua  wanachama 25 wa serikali.

Azimio hilo pia limetoa wito wa kuwepo wanachama 90 wa baraza la kitaifa la mpito kuhudumu kama bunge.

Lt Kanali Zida, aliyeahidi kukabidhi madaraka kwa raia, anatarajiwa kutii azimio hilo kwa siku chache zijazo, maafisa walisema.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

MWANAMKE 'AFUFUKA' BAADA YA KUTANGAZWA KUFA



Body in morgue (stock image)
Bi Janina aliwekwa chumba cha kuhifadhia maiti kabla ya wakati wake

Mwanamke mmoja raia wa Poland mwenye umri wa miaka 91 aliyekaa chumba cha kuhifadhia maiti kwa saa 11 baada ya kutangazwa kufariki dunia amerejea kwenye familia yake, akilalamika kusikia baridi.

Maafisa walisema Janina Kolkiewicz alitangazwa kufa baada ya dakatari wa familia kumfanyia vipimo.

Hata hivyo, wafanyakazi wa chumba hicho cha kuhifadhia maiti walishtuka kuona mfuko maalum alimohifadhiwa ukitikisika. Polisi wameanza uchunguzi.

Aliporejea nyumbani, Bi Kolkiewicz alipata joto kwa kunywa bakuli la supu na mikate ya maji miwili.  

Familia yake na daktari walisema wameshtushwa na jambo hilo.

Mtoto wa kike wa ndugu wa bibi huyo, katika mji wa Ostrow Lubelski, mashariki mwa Poland alimwita daktari huyo baada ya kurudi nyumbani asubuhi moja na kumkuta shangazi yake hapumui na mapigo ya moyo yamesimama.

Baada ya kumpima bibi huyo, daktari alimwambia ameshafariki dunia na kumwandikia cheti cha kifo.

Mwili ukapelekewa chumba cha kuhifadhia maiti na maandalizi ya mazishi yalikuwa yafanyike baada ya siku mbili.

Cheti hicho sasa kimetangazwa kuwa batili, gazeti la Dziennik Wschodni limeandika.

Bi  Kolkiewicz hana habari ni kwa kiasi gani alikaribia kuzikwa hai, kwani binti yake alisema ana ugonjwa wa kusahau.




Thursday, 13 November 2014

MGAMBO USO MDUCHUUU

 

Vimbwanga vya WhatsApp


Habari nyingine:

RAIA WENGI BADO KUAMUA NANI AWE RAIS TANZANIA http://bit.ly/1v5JOj2

DEWJI ATAJWA BILIONEA NAMBA MOJA TZ http://bit.ly/1EEJ2KX

DEWJI ATAJWA BILIONEA NAMBA MOJA TANZANIA


Ni mfanyabiashara kijana aliyekamata nafasi ya 24 katika orodha ya matajiri 55 wa Afrika.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (39), ametajwa kuwa ndiyo bilionea namba moja nchini kwa sasa, akifuatiwa na Rostam Aziz (49).

Kwa mujibu wa ripoti ya Jarida la Ventures Afrika lililotolewa jana, wafanyabiashara hao ndiyo Watanzania pekee waliongia kwenye orodha ya mabilionea 55 barani Afrika.

Dewji, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mjini kwa tiketi ya CCM, ni mfanyabishara kijana aliyekamata nafasi ya 24 katika orodha hiyo akiwa na utajiri wa Dola 2 bilioni Marekani (Sh3 trilioni).

Nafasi hiyo inamfanya kijana huyo kutambulika kama tajiri namba moja nchini kwa sasa na siyo tena Rostam.

Katika orodha hiyo Dewji amemwacha Rostam kwa nafasi 16. Rostam anashika nafasi ya 40 akiwa na utajiri wa Dola 1.2 bilioni za Marekani.

Mwaka jana, Rostam alitajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania. Hiyo ilikuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la Marekani la Forbes. Rostam alikamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.6 trilioni).

Katika orodha hiyo, yumo pia Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma kuwa mmoja wa mabilionea wa Tanzania na Afrika.