Monday, 24 November 2014

MTOTO AUAWA NA POLISI AKIWA NA BUNDUKI BANDIA



 Tamir Rice
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 amepigwa risasi na polisi wa mji wa Cleveland nchini Marekani na kufariki dunia, baada ya kubeba kwa kile kilichokuja kujulikana ni bunduki bandia.

Polisi wamesema afisa mmoja alimfyatulia risasi mara mbili mtoto huyo baada ya kushindwa kutii amri ya kunyanyua mikono.

Kuna mtu alimripoti mtoto huyo kwa polisi kuwa alikuwa akitisha watu na bunduki hiyo lakini hakujua kama ni ya kweli au la.

Afisa mmoja alikuwa ndio kwanza yuko kwenye mwaka wake wa kwanza katika kazi hiyo ya jeshi la polisi, mwengine tayari alikuwa na uzoefu wa miaka 10.

Daktari wa kaunti ya Cuyahoga aliyemfanyia uchunguzi amemtambua mtoto huyo kuwa  Tamir Rice.

Mtoto huyo alipigwa risasi siku ya Jumamosi mchana na kufariki dunia hospitalini asubuhi ya Jumapili.

BALAA: 'VIBOMU' KWENYE MITIHANI


 


 Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

KENYA YAUA 'WAPIGANAJI 100 WA ALSHABAB'



RAIS OBAMA: HILLARY ATAKUWA RAIS MZURI



Hillary for 2016 merchandise

Hillary Clinton atakuwa "rais mzuri" iwapo ataamua kugombea Urais wa Marekani mwaka 2016, Rais Barack Obama alisema.

Aliiambia ABC News kuwa Bi Clinton "asingekuwa anakubaliana na mie kwa kila kitu", ambaponi ishara ya kuwavutia wapiga kura baada ya kukaa madarakani kwa miaka minane.

Bi Clinton, mwenye umri wa miaka 67, alishindwa katika uteuzi wa kugombea urais kupitia chama cha Democrat ambapo Bw Obama ndio aliibuka kidedea.

Anatarajiwa kutangaza iwapo atagombea tena mapema mwaka 2015

Sunday, 23 November 2014

GORDON BROWN 'KUACHIA NGAZI KAMA MBUNGE'



 Former Prime Minister Gordon Brown speaks at a campaign event in favour of the union in Clydebank, Scotland, September 16
Aliyekuwa waziri mkuu Gordon Brown anatarajiwa kuachia ngazi kama mbunge katika uchaguzi mkuu ujao, ripoti zinasema.

Mbunge huyo wa Kirkcaldy na Cowdenbeath atatangaza uamuzi wake huo “katika siku chache zijazo”, mshirika mmoja aliliambia gazeti la Sunday Mirror la Uingereza.

Hakuna uthibitisho wowote rasmi lakini viongozi waandamizi wa chama cha Labour wameiambia BBC wanatarajia ang’atuke.

Bw Brown mwenye umri wa miaka 63, ambaye alikuwa mstari wa mbele hivi karibuni katika kampeni dhidi ya uhuru wa Uskochi, amekitumikia chama hicho takriban miaka 32.

Alikuwa waziri mkuu tangu mwaka 2007 hadi 2010, chama cha Labour kiliposhindwa, tena katika matokeo mabaya kuwahi kutokea tangu mwaka 1983.

Kufuatia kushindwa huko, amekuwa haonekani sana bungeni tangu wakati huo.

KENYA YAUA 'WAPIGANAJI 100 WA ALSHABAB'



A Kenyan soldier patrols the scene of an attack on a bus, some 30km from Mandera town, in northern Kenya - 22 November 2014

Jeshi la Kenya limeua zaidi ya wapiganaji 100 wa al-Shabab waliohusishwa na shambulio baya sana kwenye basi, naibu rais wa Kenya alisema.

William Ruto alisema majeshi yamefanya misako miwili nchini Somalia, kuharibu vifaa na kambi ambapo shambulio hilo la basi lilipopangwa.

Katika shambulio la Jumamosi, wapiganaji waliwachomoa abiria wasio waislamu kutoka kwenye basi kaskazini mwa Kenya, na kuua 28.

Al-Shabab limefanya mfululizo wa mashambulio nchini Kenya tangu mwaka 2011, mwaka ambao Kenya ilipeleka majeshi Somalia kusaidia kupambana na wapiganaji.

Chanzo: BBC                            
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

'BOKO HARAM' WAUA WAUZA SAMAKI 48



 Aftermath of a Boko Haram attack in Kano state, 15 November 2014

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram imeripotiwa kuwa wameua watu 48 katika shambulio dhidi ya wauzaji samaki karibu na mpaka wa Chad.

Kundi la wauzaji hao walisema baadhi walikatwa shingo wakati wengine walifungwa kwa kamba na kuzamishwa katika ziwa Chad.

Shambulio hilo lilifanyika siku ya Alhamis, lakini taarifa hizo zimechelewa kujulikana kwasababu Boko Haram wameharibu mitambo ya simu za mkononi eneo hilo.

Ni shambulio la pili kubwa kufanywa na Boko Haram katika siku mbili.

Katika shambulio la Alhamis, wafanyabiashara hao walikuwa wakielekea Chad kununua samaki ndipo wanamgambo hao waliweka kizuizi karibu na kijiji cha Doron Baga, takriban kilomita 180 kaskazini mwa Maiduguri katika jimbo la Borno.

Abubakar Gamandi, mkuu wa umoja wa wauza samaki, alisema wanamgambo hao hawakutumia bunduki zozote.

“Washambuliaji hao waliwaua wauzaji hao kimya kimya bila kutumia bunduki kuzuia kuonekana na majeshi,” aliliambia shirika la habari la AFP.

KIINGEREZA KAZIIIIIIIIII

  

Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

KIFO CHA MTOTO KILICHOZUA HASIRA, UGANDA

RAIS WA INDONESIA ASAFIRI DARAJA LA 'ECONOMY'

UCHAGUZI WA KWANZA TUNISIA BAADA YA MAGEUZI



Activists in Monastir, Tunisia. Photo: 2 November 2014

Raia wa Tunisia wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu “vuguvugu la mageuzi ya nchi za Kiarabu” kutokea mwaka 2011 na kuchochea mageuzi hadi nchi nyingine eneo hilo.

Zaidi ya watu 25 wanagombea kinyang’anyiro hicho, lakini aliye madarakani kwa sasa  Moncef Marzouki na Beji Caid Essebsi wanaonekana kukubalika zaidi.

Uchaguzi huo ni sehemu ya mpito wa kisiasa baada ya kupinduliwa kwa Zine al-Abidine Ben Ali.

Uchaguzi wa wabunge ulifanyika mwezi Oktoba.

Tunisia – nchi inayoonekana kiini cha mageuzi katika nchi za Kiarabu – pia inachukuliwa kuwa nchi iliyofanikiwa zaidi baada ya mageuzi hayo, na yenye ghasia kidogo kulingana na nchi nyingine.