Sunday, 30 November 2014

MAVAZI YA MABINTI WA OBAMA YALETA KIZAAZAA



 US President Barack Obama smiles at his daughters Sasha and Malia after he pardoned a turkey during a ceremony at the White House on 26 November 2014 in Washington



Mabinti wa Rais Barack Obama Sasha na Malia wameelezewa na afisa mmoja wa chama cha Republican kukosa heshima na hadhi kutokana na mavazi yao siku ya sherehe za Thanksgiving.

Elizabeth Lauten, mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge wa Republican Stephen Fincher, aliandika kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kauli yake hiyo ilikoselewa na wengi na hatimaye kufutwa.

Bi Lauten ameomba radhi kwa “maneno yake yaliokera.”

Aliwashambulia mabinti hao kutokana na mavazi waliovaa katika shughuli ya kila mwaka iliyofanyika Ikulu ya White House.

Malia, mwenye umri wa miaka 16, na Sasha, 13, walisimama karibu na baba yao siku ya shughuli hiyo.

Bi Lauten alisema mabinti hao wangejitahidi "kuonyesha hadhi kidogo".

"Vaa kama unastahili heshima, sio kama uko baa," aliongeza.

Kauli zake hizo zilisababisha hamaki kwenye mitandao ya kijamii, huku kukiwa na madai kuwa alikuwa “akiwadhalilisha” mabinti hao vijana.

Chanzo: washingtontimes.com

AJERUHIWA KWA CHOO CHA KUIBUKA ARDHINI



A scooter lies in pieces after a public toilet suddenly emerged from the ground

Mtu mmoja katika mji wa Amsterdam amejeruhiwa baada ya choo cha umma kinachomazishwa ardhini kuibuka ghafla  bila kutarajia.

Mtu huyo alijeruhiwa na mfano wa motokari iliyoruka angani kwa inayoitwa choo cha Urilift kilichoibuka ghafla.

Kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini kwa majeraha madogo.

Vyoo hivyo vimezagaa maeneo mengi katikati ya Amsterdam, na huibuka kutoka ardhini usiku kuzuia watu kukojoa mitaani.

Walioshuhudia waliripoti kusikia mlio mkubwa sana wakati wa ajali hiyo.

Mtu mmoja aliweka picha baada ya tukio hilo katika mtandao wa kijamii wa twitter na kuandika : “Nimepita pembezoni mwa mlipuko kama dakika mbili zilizopita. Nahisi nina bahati.”

Haiko wazi nini kilisababisha tukio hilo.

Matokeo ya uchunguzi huo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa juma.


Vyoo vya Urilift hupatikana Amsterdam na katika nchi mbalimbali barani Ulaya.


Chanzo: Independent.co.uk

Saturday, 29 November 2014

MICHEPUKO HII ITAADHIRI WENGI



 Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

MALAWI NA TANZANIA BADO ZAZOZANIA ZIWA NYASA



IDADI YA UTUMWA UINGEREZA 'KUBWA MNO'



Woman victim (posed by model)

Inawezekana kuwepo waathirika wa utumwa kati ya 10,000 hadi 13,000 Uingereza, idadi kubwa kuliko takwimu za awali, wizara ya mambo ya ndani imependekeza.

Waathirika wa utumwa wa kisasa ni pamoja na wanawake wanaolazimishwa kuingia kwenye biasahara ya uchangudoa, wafanyakazi wa ndani “wanaofungiwa”, na wanaofanya kazi mashambani, viwandani na kwenye boti za uvuvi.

Takwimu za mwaka 2013 ni mara ya kwanza kwa serikali hiyo kutoa idadi rasmi ya ukubwa wa tatizo hilo.

Wizara ya mambo ya ndani imeanzisha mkakati wa kupambana na utumwa huo.

Imesema waathirika hao inahusisha watu kutoka zaidi ya nchi 100 – na zaidi kutoka Albania, Nigeria, Vietnam na Romania – pamoja na watoto na watu wazima waliozaliwa Uingereza.

Mwaka jana Kituo cha Takwimu za Shirika la Uhalifu wa Taifa wa Kuuza Binadamu kilisema waathirika wa utumwa nchini Uingereza ilikuwa 2,744.

Tathhmini hiyo ilitolewa kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo polisi, idara ya uhamiaji, na mashirika ya kutoa misaada.

MALAWI NA TANZANIA BADO ZAZOZANIA ZIWA NYASA



Kile kilichoonekana kuanza kama mzaha kati ya Tanzania na Malawi kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa, sasa kimeanza kuchukua sura mpya kwa kila nchi kuendelea kutekeleza kitu inachokiamini kuwa ni sahihi.

Baada ya kutokea vuta nikuvute kati ya nchi hizo mbili zilizokuwa marafiki wa miaka mingi, marais wastaafu kutoka Msumbiji, Joaquim Chissano, Festus Mogae wa Bostwana na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini walipewa jukumu la kutafuta maridhiano.

Hivi karibuni marais hao walikutana na Rais Peter Mutharika kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo, lakini kwa bahati mbaya walichodhani kuwa ni jambo dogo, kiligeuka kuwa ‘mfupa mgumu’ baada ya rais huyo kusema Tanzania haimiliki hata inchi moja ya Ziwa Nyasa.

Kama hiyo haitoshi, Mutharika anasema kuwa msimamo wake hauwezi kubadilika kwa kuwa mipaka ya nchi hizo mbili iliwekwa na wakoloni na kuipa uhalali Malawi umiliki wa ziwa hilo.

Wakati hayo yakiendelea huko Malawi, hapa nchini Serikali inaendelea na mipango ya kuboresha miundombinu ndani ya ziwa hilo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa meli yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200.

MUBARAK WA MISRI AFUTIWA MASHTAKA YA MAUAJI



 Hosni Mubarak in court in Cairo, 29 November

Mahakama mjini Cairo imemfutia mashtaka aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak kwa jaribio la kupanga kuwaua waandamanaji wakati wa ghasia za kumpindua mwaka 2011.

Mahakama uliibuka kwa shangwe baada ya jaji kuhitimisha kesi ya Mubarak kwa kufuta mashtaka yaliyohusishwa na mauaji ya mamia ya watu.

Pia alifutiwa mashtaka ya ufisadi iliyohusisha mauzo ya gesi Israel.

Mubarak, mwenye umri wa miaka 86, anatumikia kifungo kingine cha miaka mitatu kwa ubadhirifu wa mali ya umma.

Friday, 28 November 2014

MALEMA ASIMAMISHWA BUNGENI, AFRIKA KUSINI


 Julius Malema speaks as he launches his Economic Freedom Fighters party in Johannesburg, South Africa on 11 July 2013

Mkuu wa chama cha upinzani cha Afrika kusini Julius Malema na wabunge wake 11 wamesimamishwa katika bunge bila malipo baada ya kumdhalilisha rais wa nchi hiyo.

Wakati Rais Jacob Zuma alipolihutubia bunge mwezi Agosti, wanachama wa Economic Freedom Fighters (EFF) walipiga kelele wakisema "lipa pesa zetu".

Walikuwa wakimaanisha matumizi ya dola milioni 23 ya pesa za serikali kukarabati nyumba yake binafsi huko Nkandla.

Mapema mwezi huu, bunge lilimfutia makosa.

Chama hicho cha EFF kilisema kitapambana mahakamani kusimamishwa huko, ambapo ni kati ya siku 14 hadi 30.