Thursday, 18 December 2014

MMAREKANI AKAMATWA UGANDA KWA 'PESA BANDIA'



A pile of fake currency in Uganda

Mamlaka za Marekani zimemkamata Mmarekani nchini Uganda kwa madai ya kuendesha mtandao wa kimataifa wa biashara ya fedha bandia.

Ryan Gustafson, mwenye umri wa miaka 27, alifunguliwa mashtaka ya kufanya njama na biashara ya fedha bandia nje ya Marekani baada pesa hizo kutumika katika biashara mbalimbali Marekani.

Shirika la kijasusi la Marekani limefuatilia pesa hizo na kugundua ziko Kampala, ambapo wanasema wamekuta mtandao unaotengeneza pia euro, rupia za India, franca za Congo na fedha nyingine bandia za kiafrika.

Mshukiwa huyo anakabiliwa na miaka 25 jela.

A pair of fake hands found in Uganda
Mikono bandia, alokuwa akitumia mshukiwa kama glovu kuficha alama za vidole


"Tutawawajibisha wahalifu wa mitandao mpaka haki ipatikane hata waishi wapi," Mwanasheria Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ya Pennsylvania David Hickton aliandika kwenye taarifa yake.

Pesa bandia ziligundulika Pittsburgh, Pennsylvania, katika maduka ya rejareja na biashara nyingine.

Maafisa wa kijasusi waligundua fedha hizo zilikuwa zikitumwa kutoka Uganda.

Alama ya kidole kwenye moja ya mizigo ikawaongoza mpaka kwa Bw Gustafson, raia wa Marekani ambaye awali alikuwa akiishi Texas.


Mamlaka za Marekani zinakadiria mshukiwa huyo alisambaza takriban dola milioni 2 katika  soko la biashara ambazo zilikuwa bandia.




MCHELE MMOJA MAPISHI MENGI

   

Vimbwanga vya WhatsApp

BLOGGER WA KENYA MATATANI KWA 'KUMTUKANA' RAIS



Wednesday, 17 December 2014

SHERIA ZA WATOTO 'KUTOKA WATU WATATU'


Babies

Sheria ya kutengeneza watoto kutoka watu watatu – ambapo inasemwa wawili tu watakuwa wazazi halali- imetangazwa na serikali ya Uingereza.

Mbinu hiyo ya uzalishaji itatumia nasaba kutoka kwa mama, baba na mwanamke wa kujitolea ili kuzuia maradhi.

Wabunge hivi karibuni watapiga kura ili kuifanya Uingereza nchi ya kwanza duniani kuhalalisha utaratibu huo au la.

Wapinzani wanasema ni kinyume cha maadili kutengeneza watoto kutumia asidi nasaba, DNA kutoka watu watatu.

Wanasayansi wa Uingereza walioongoza utafiti huo wanatarajia kuanza kutumia utaratibu huo mwakani.

BLOGGER KENYA MATATANI KWA 'KUMTUKANA' RAIS


 Robert Alai

Blogger maarufu na mwenye utata wa Kenya amefunguliwa mashtaka ya kumdhalilisha rais , kufuatia ujumbe wa twitter aliyoweka mapema wiki hii.

Robert Alai, mkosoaji mkali wa serikali, alimwita Rais Uhuru Kenyatta "adolescent president".

Alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana kwa dola 2,000 na kuamriwa kutoweka ujumbe unaofanana na huo wakati uchunguzi ukiendelea.

Bw Alai ni miongoni mwa blogger maarufu na wenye ushawishi mkubwa Kenya.

Ana wafuasi 140,000 kwenye ukurasa wake wa twitter.

Siku hiyo aliyomwita rais jina hilo, pia akaweka namba za simu za rais na baadhi ya maafisa waandamizi.

Bw Alai tayari ana wengi wanaomwuunga mkono kwenye mtandao wa kijami wa Twitter kutoka kwa Wakenya wanaoona mashtaka hayo kama mbinu ya serikali ya kuzuia uhuru wa vyombo vya habari.

Alipotolewa tu kwa dhamana, aliandika kwenye twitter kuwa itakuwa ngumu kumnyamazisha.

Miaka miwili ilyopita, alikamatwa na kuhojiwa baada ya kudai kuwa msemaji wa serikali ya wakati huo alikuwa akipanga kumwuua.

BILL COSBY: MASHTAKA YA 1974 KUTOFUNGULIWA



Comedian Bill Cosby plays the vibraphone in Boston, Massachusetts (January 2006)

Mashtaka dhidi ya mchekeshaji Bill Cosby hayatofunguliwa juu ya madai kuwa alimdhalilisha kijinsia binti mdogo mwaka 1974, waendesha mashtaka wa Marekani alisema.

Walielezea kuwa kuna kikomo kinachozuia kuchukua hatua za kisheria baada ya muda fulani inapodaiwa kosa hilo kufanyika.

Judy Huth alidai kuwa Bw Cosby alimdhalilisha akiwa na umri wa miaka 15.

Ni miongoni mwa takriban wanawake 15 ambao mapema mwezi Novemba wamedai kuwa Bw Cosby aliwadhalilisha kijinsia.

Mawakili wa mchekeshaji huyo wamekana mengi ya madai hayo huku wengine wakiwapuuza wakisema aidha uongo au madai yamepitwa na wakati.

Wengi wa wanawake hao wanasema mchekeshaji huo aliwalewesha kabla ya kuwadhalilisha.

Bi Huth alidai alilazimishwa na Bw Cosby kumfanyia kitendo cha ngono huko Los Angeles.


Tuesday, 16 December 2014

HURU KUFUATIA KOSA LA KIFO CHA RAIA WA ANGOLA


Terence Hughes (L), Colin Kaler (2ndR) and Stuart Tribelnig (R) stand as a spokeswoman speaks to members of the media
Taarifa ikisomwa kwa niaba ya maafisa hao watatu

Walinzi watatu wa G4S, Uingereza wamekutwa hawana hatia kwa mashtaka ya kuua bila kukusudia wa mtu aliyefariki dunia wakati wa jaribio la kumfurumusha nchini katika uwanja wa ndege wa Heathrow.

Jimmy Mubenga, mwenye umri wa miaka 46, alipata ugonjwa wa moyo baada ya kushikiliwa kwenye ndege, Oktoba 2010.

Terence Hughes, 53, Colin Kaler, 52, na Stuart Tribelnig, 39, walikana kumshughulikia vibaya au kwa kumpuuza wakati wa tukio hilo, kwenye ndege ya Brirish Airways.

Walishutumiwa kwa kuzuia upumuaji wa Mubenga.

Jimmy Mubenga
Jimmy Mubenga alikuwa akirejeshwa Angola


Mahakama iliambiwa abiria walimsikia Bw Mubenga akilia "Siwezi kupumua" wakati alipobanwa kwenye kiti – huku tayari akiwa amefungwa pingu kwa nyuma na mkanda pia.

Lakini walinzi hao wamekana kumkandamiza kwenye kiti na kumweka kwenye mkao ulioathiri kupumua kwake.

Pia walisisitiza hawakumsikia akipiga kelele akisema hawezi kupumua

Bw Mubenga alifurumishwa nchini Uingereza kurejeshwa Angola baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kudhalilisha na kusababisha majeraha.

Kufuatia uamuzi huo, walinzi hao walisema walifurahishwa sana kufutiwa mashtaka hayo.

KENYA YAFUTA USAJILI WA NGOs ZAIDI YA 500


Passengers travelling to Nairobi wait to be searched for weapons in the town of Mandera at the Kenya-Somalia border, 8 December 2014
Kenya imeimarisha usalama kufuatia mashambulio na wanamgambo

Kenya imewafutia usajili mashirika yasiyo ya kiserikali 510 (NGOs), wakiwemo watuhumiwa watano wanaohusishwa na ugaidi, afisa mmoja alisema.

Serikali pia imepiga tanji akaunti zao za benki na kufuta vibali vya kazi vya wafanyakazi wa kigeni.

Hatua hiyo inafuatia mjadala mzito nchini Kenya juu ya mswada mpya tata wa usalama wenye lengo la kupambana na wapiganaji.

Kundi la al-Shabab linalohusishwa na al-Qaeda limezidi kufanya mashambulio Kenya.

Mashirika hayo yalifutiwa usajili wao kutokana na kushindwa kuwasilisha rekodi zao za fedha, alisema Henry Ochido, naibu mkuu wa bodi ya NGOs iliyoteuliwa na serikali, inayosimamia shughuli zao.

Bw Ochido aliiambia BBC, 15 wanatuhumiwa kwa magendo na kufadhili “ugaidi”.

Baadhi walihusishwa na mashambulio mawili ya mabomu ya mwaka 1998 ya balozi za Marekani nchini Kenya na nchi jirani ya Tanzania, alisema.

Bw Ochido alikataa kutaja majina ya mashirika hayo, akisema uchunguzi bado unaendelea.