Monday, 12 January 2015

MARUFUKU KUTENGENEZA 'SNOWMEN' SAUDI ARABIA


 

Huku sehemu chache za Saudi Arabia zikipata  theluji kwa nadra, fatwa iliyotolewa ya kupiga marufuku kutengeneza sanamu ya mtu kwa theluji ‘snowmen’ uliotolewa na kiongozi wa Kiislamu umekuwa ukisambaa kwa kasi.

Uamuzi huo uliotolewa na Sheikh Mohammed Saleh al-Munajjid ambaye ni maarufu sana unaonekana ulitolewa muda mrefu tu.

Sheikh huyo ametangaza kuwa kutengeneza sanamu huyo ni sawa na kutengeneza taswira ya binadamu, jambo ambalo linapigwa marufuku na dini ya Kiislamu.

Uamuzi wake huo umekosolewa na wengi kwenye mtandao wa kijami wa Twitter, huku raia kadhaa wa Saudia wameweka picha si tu za ‘snowmen’ lakini pia ngamia kwa kutumia theluji na ma biharusi kwa theluji.

Chanzo: Mtandao wa Sheikh

JK: ELIMU BURE MWAKANI TANZANIA



Rais Jakaya Kikwete ametangaza habari njema kwa Watanzania kwamba kuanzia mwaka kesho, elimu ya msingi na sekondari itatolewa bure.

Alitangaza azma hiyo ya serikali juzi, wakati akizungumza katika karamu aliyowaandalia mabalozi ya  kuukaribisha  mwaka  2015 iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alisema hatua hiyo inakuja baada ya serikali kukamilisha  sera mpya ya elimu na ufundi ili kuboresha sekta hiyo ambayo imepitishwa na  Baraza la Mawaziri.

Hatua hiyo inachukuliwa katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata kiwango hicho cha elimu kwa gharama inayobebwa na serikali.

“Kwenye sera mpya, imeainisha jinsi ya utoaji wa elimu bora na viwango vinavyokubalika katika ufundi, hii itawezesha  elimu hizi mbili kukidhi matakwa katika soko la ajira pamoja na kujiajiri,” alisema.

“Wazo hili la kufanya elimu hii kuwafikia kila mmoja sasa ndilo jukumu lililo mbele yetu tukianza na maandalizi ya kuhakikisha tunalitimiza lengo hili kuu kwa ufanisi mkubwa,”alisema.

Sunday, 11 January 2015

52 WAFARIKI DUNIA KWA KUNYWA BIA YENYE SUMU



 Craft beer

Bia ya kienyeji iliyo na sumu imeua watu 52 Msumbiji, mamlaka za afya katika nchi hiyo iliyo kusini mwa Afrika zimesema siku ya Jumapili.

Watu wengine 51 walilazwa katika hospitali za wilaya ya Chitima na Songo kwenye jimbo la Tete kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, na 146 wamefika hospitalini kuchunguzwa iwapo wameathirika na sumu hiyo, afisa wa afya wa wilaya Alex Albertini ameiambia Redio Mozambique.

Wale waliokunywa bia hiyo walikuwa wakihudhuria msiba eneo hilo siku ya Jumamosi, alisema Albertini.

Pombe,jina la bia ya kienyeji ya Msumbiji, hutengenezwa kwa mtama au unga wa ngano.

Mamlaka husika zinaamini kinywaji hicho kilipata sumu kwa kutiliwa nyongo ya mamba wakati wa msiba huo.

Damu na bia za kienyeji zimepelekwa mji mkuu Maputo kufanyiwa uchunguzi, alisema mkurugenzi wa afya wa jimbo Carle Mosse.

Hakuna hata mmoja wa waombolezaji waliokunywa bia hiyo asubuhi waliolalamika kuumwa, lakini wale waliokunywa mchana, waliumwa, mamlaka zilisema.

Wanaamini bia hiyo lazima ilitiwa sumu wakati waombolezaji walipokuwa makaburini kuzika.

Mwanamke aliyetengeneza bia hiyo ni miongoni mwa waliokufa.

Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Mamlaka za afya zimeanza kuchangia kwa kupeleka vyakula na vifaa vengine kwa familia zilizoathirika.

Chanzo: AP                                                              

Saturday, 10 January 2015

MUUGUZI AUA WAGONJWA 30 KISA 'KUBOREKA'



 


Mahakama ya Ujerumani imeambiwa aliyekuwa muuguzi wa kiume amekiri kuua zaidi ya wagongwa 30 kwenye hospitali alipokuwa akifanyia kazi, kwa madai kuwa ‘kaboreka tu’.

Mtaalamu wa magonjwa ya akili alisema wakati wa kesi hiyo kuwa muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 38 alikiri kufanya mauaji hayo katika uchunguzi aliofanyiwa hivi karibuni, msemaji wa mahakama alisema.

Kesi ya aliyekuwa muuguzi huyo ilianza Oldenburg,  kaskazini mwa Ujerumani mwezi Septemba, akituhumiwa kwa mauaji ya wagonjwa watatu na jaribio la mauaji ya wengine wawili.

Mtaalamu huyo alisema alikiri mashtaka hayo, na pia akasema alizidisha kipimo cha dawa kwa wagonjwa wengine 90, ambapo 30 walifariki dunia, msemaji huyo alisema.


Wachunguzi wanahisi nia yake ilikuwa kuibua dharura za kitabibu ili apate nafasi ya kuonyesha ujuzi wake wa kumwibua mgonjwa aliyezimia, lakini pia alikuwa ‘ameboreka tu’.

Inaaminiwa alikuwa akiwachoma wagonjwa na sindano yenye dawa ya kutibu moyo iliyovuruga mapigo ya moyo na kushusha kiwango cha damu.

Chanzo: AP






Friday, 9 January 2015

SHAHIDI WA ICC KENYA 'AHUSISHWA NA UFISADI'



Meschak Yebei with his son in Kenya

Mtu mmoja aliyekutwa amekufa Kenya aliyehusishwa na kesi ya Naibu Rais William Ruto alikutwa katika majaribio ya kuwahonga mashahidi, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC ilisema.

Waendesha mashtaka walisema hawakupanga kumwita, Meshack Yebei, kama shahidi kwasababu hiyo.

Mwili wa Bw Yebei ulikutwa magharibi mwa Kenya mapema mwezi huu.

Wakili wake alisema angetakiwa kuwa shahidi wa Bw Ruto, anayekana mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Bw Ruto alishtakiwa kwa ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa serikali kushtakiwa na mahakama iliyopo The Hague tangu ianzishwe zaidi ya muongo mmoja uliopita.

ICC ilifuta mashtaka kama hayo dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita, akidai mashahidi wa upande wa mashtaka wamekuwa wakitishwa na kubadilisha ushahidi wao.

Bw Kenyatta alisema hakuwa na hatia na pia upande wa mashtaka hawakuwa na kesi dhidi yake.


Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


KIONGOZI WA DINI ABU HAMZA AFUNGWA MAISHA



 A courtroom sketch shows Abu Hamza, 56, with his defence lawyer Sam Schmidt 9 January 2015

Kiongozi wa kiislamu mwenye msimamo mkali Abu Hamza al-Masri amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama mjini New York kwa kuunga mkono ugaidi.

Alitiwa hatiani mwezi Mei kwa makosa mengi, ikiwemo utekajinyara na jaribio la kuunda kambi ya mafunzo ya kigaidi Marekani.

Kesi yake ilihusisha mchakato mrefu wa kuhamishwa kutoka Uingereza.

Wakati wa kutolewa hukumu, mawakili walimwomba jaji azingatie kuwa amepoteza mikono yake na jicho lake.

Pia walisema mpango wa kumfunga  Abu Hamza katika gereza kubwa la huko Colorado utakiuka ahadi Marekani iliwapa majaji wa London kumhamisha mwaka 2012.

Waendesha mashtaka siku ya Ijumaa walisema serikali ya Marekani haikuwahi kuweka ahadi kama hiyo kwa Uingereza na kifungo cha maisha ndio njia pekee.