Tuesday, 13 January 2015

TOVUTI MPYA YAUNDWA KUFICHUA SIRI ZA AFRIKA



 Young Ivorian learn how to use a computer on 22 April 2004 in Abidjan

Tovuti  inayofichua mambo yaliyojificha uliolilenga hasa bara la Afrika umeanzishwa, ukikusudia kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa barani humo.

Imeahidi kuficha utambulisho kwa yeyote atakayetaka kutoa taarifa za siri kwa magazeti huru.

Tovuti hiyo - inayoitwa afriLeaks - imesema inataka kuwaunganisha wafichuaji maovu na kundi la waandishi wa habari wanaofichua  na kuandika habari za uchunguzi, na pia kutoa mafunzo maalum kwa waandishi hao.

Makundi ya vyombo vya habari Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Botswana tayari washajiunga na mtandao huo.  

Afrika limekua kwa kasi kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni lakini idara nyingi zinabaki kuwa dhaifu, na rushwa inakisiwa kuigharimu bara hilo mabilioni ya dola kila mwaka.

Afrileaks, iliyoundwa kutokana na vyombo vya habari 19 na makundi ya kutetea haki za binadamu, imedhamiria “kueleza ukweli “.

Miongoni mwa 19 mengi ni magazeti likiwemo la Afrika kusini Mail & Guardian, Daily Nation la Kenya na  Premium Times la Nigeria.

Nia hasa ni kuwafichua wanasiasa na wafanyabiashara barani humo wanaotumia vibaya madaraka yao.

Chanzo: theguardian.com

'MAAMUZI' YA GRACE MUGABE YAZUIWA MAHAKAMANI



A Zimbabwean villager weeps in front of burning and demolished makeshift shelters at Manzou Farm in Mazowe - 8 January 2015

Mahakama kuu ya Zimbabwe imesimamisha hatua ya kuondoshwa kwa zaidi ya familia 200 kwenye shamba lililopo kaskazini mwa nchi hiyo hadi kutakapokua na nyumba mbadala kwa ajili yao.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamemshutumu mke wa rais wa nchi hiyo, Grace Mugabe, kutaka kubadilisha shamba hilo kuwa hifadhi ya wanyama.

Afisa mmoja amekana kuwa Bi Mugabe ana uhusiano wowote na eneo hilo.

Hata hivyo familia hizo zinasisitiza waliambiwa na polisi waondoke ili kumpisha Rais Robert Mugabe na mke wake.

WAFANYAKAZI WA TAZARA WAGOMA, TANZANIA



A woman walks next to train tracks in Zambia on 12 November 2014

Huduma za reli baina ya Tanzania na Zambia zimesita kutokana na mgomo wa zaidi ya wafanyakazi 1,500 kutoka Tanzania.

Afisa mmoja wa umoja wa wafanyakazi alisema wafanyakazi hao hawajalipwa kwa miezi mitano na serikali ya Tanzania kutokana na mgogoro wa fedha katika mamlaka hizo za reli.

Serikali bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na tukio hilo.

China imefadhili ujenzi wa reli hiyo, ambayo ina kilomita 1,860 (1,155 maili ), katika miaka ya 70 kwa nia ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

Iliwapa serikali ya nchi hizo mbili mkopo usio na riba wa dola za kimarekani milioni 500 kila mmoja, kwa ajili ya mradi huo.

Hatahivyo, Mamlaka za Reli ya Tanzania- Zambia, iliyoundwa na serikali hizo mbili, inaendesha shughuli zake kwa hasara, alisema mwandishi wa BBC aliyopo mjini Dar es Salaam.

Mamlaka hiyo inamsaka mwekezaji kwa udi na uvumba kuinusuru, kwani serikali za Tanzania na Zambia zinasita kuendelea kuifadhili reli hiyo, aliongeza.

Watu wa vijijini aghlabu hutumia huduma hizo za reli. Na pia hutumiwa kusafirisha mizigo, hasa shaba na mbao, kutoka Zambia kuelekea Tanzania, alisema mwandishi huyo.

Afisa wa Jumuiya ya Wafanyakazi wa Reli Tanzania Erastus Kihwele ameiambia BBC Focus on Africa kuwa serikali hizo mbili zingetafuta “fedha za dharura” kulipa wafanyakazi.

Alisema wengi wao hawana pesa za kulipa kodi  za nyumba au ada za shule kwa ajili ya watoto wao kwasababu hawajalipwa mshahara kwa miezi mitano.

Mgomo huo unatarajiwa kudumu kwa wiki moja, lakini unaweza kuendelea zaidi kama matakwa yao hayakutekelezwa, Bw Kihwele aliongeza.

Monday, 12 January 2015

ANGA NAYO KUTUMIKA KAMA SULUHU YA FOLENI DAR?

     
Foleni ya magari katika miji mingi barani Afrika ni jambo la kawaida, na linalolalamikiwa kila mara. Kumekuwa na jitihada mbalimbali kujaribu kukabiliana na hali hiyo. Abiria pia wanatafuta njia zao kujaribu kuepuka foleni. Salim Kikeke ametembelea Dar es Salaam, na kushuhudia tatizo hilo, na suluhu inayotafutwa

MARUFUKU KUTENGENEZA 'SNOWMEN' SAUDI ARABIA


 

Huku sehemu chache za Saudi Arabia zikipata  theluji kwa nadra, fatwa iliyotolewa ya kupiga marufuku kutengeneza sanamu ya mtu kwa theluji ‘snowmen’ uliotolewa na kiongozi wa Kiislamu umekuwa ukisambaa kwa kasi.

Uamuzi huo uliotolewa na Sheikh Mohammed Saleh al-Munajjid ambaye ni maarufu sana unaonekana ulitolewa muda mrefu tu.

Sheikh huyo ametangaza kuwa kutengeneza sanamu huyo ni sawa na kutengeneza taswira ya binadamu, jambo ambalo linapigwa marufuku na dini ya Kiislamu.

Uamuzi wake huo umekosolewa na wengi kwenye mtandao wa kijami wa Twitter, huku raia kadhaa wa Saudia wameweka picha si tu za ‘snowmen’ lakini pia ngamia kwa kutumia theluji na ma biharusi kwa theluji.

Chanzo: Mtandao wa Sheikh

JK: ELIMU BURE MWAKANI TANZANIA



Rais Jakaya Kikwete ametangaza habari njema kwa Watanzania kwamba kuanzia mwaka kesho, elimu ya msingi na sekondari itatolewa bure.

Alitangaza azma hiyo ya serikali juzi, wakati akizungumza katika karamu aliyowaandalia mabalozi ya  kuukaribisha  mwaka  2015 iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alisema hatua hiyo inakuja baada ya serikali kukamilisha  sera mpya ya elimu na ufundi ili kuboresha sekta hiyo ambayo imepitishwa na  Baraza la Mawaziri.

Hatua hiyo inachukuliwa katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata kiwango hicho cha elimu kwa gharama inayobebwa na serikali.

“Kwenye sera mpya, imeainisha jinsi ya utoaji wa elimu bora na viwango vinavyokubalika katika ufundi, hii itawezesha  elimu hizi mbili kukidhi matakwa katika soko la ajira pamoja na kujiajiri,” alisema.

“Wazo hili la kufanya elimu hii kuwafikia kila mmoja sasa ndilo jukumu lililo mbele yetu tukianza na maandalizi ya kuhakikisha tunalitimiza lengo hili kuu kwa ufanisi mkubwa,”alisema.

Sunday, 11 January 2015

52 WAFARIKI DUNIA KWA KUNYWA BIA YENYE SUMU



 Craft beer

Bia ya kienyeji iliyo na sumu imeua watu 52 Msumbiji, mamlaka za afya katika nchi hiyo iliyo kusini mwa Afrika zimesema siku ya Jumapili.

Watu wengine 51 walilazwa katika hospitali za wilaya ya Chitima na Songo kwenye jimbo la Tete kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, na 146 wamefika hospitalini kuchunguzwa iwapo wameathirika na sumu hiyo, afisa wa afya wa wilaya Alex Albertini ameiambia Redio Mozambique.

Wale waliokunywa bia hiyo walikuwa wakihudhuria msiba eneo hilo siku ya Jumamosi, alisema Albertini.

Pombe,jina la bia ya kienyeji ya Msumbiji, hutengenezwa kwa mtama au unga wa ngano.

Mamlaka husika zinaamini kinywaji hicho kilipata sumu kwa kutiliwa nyongo ya mamba wakati wa msiba huo.

Damu na bia za kienyeji zimepelekwa mji mkuu Maputo kufanyiwa uchunguzi, alisema mkurugenzi wa afya wa jimbo Carle Mosse.

Hakuna hata mmoja wa waombolezaji waliokunywa bia hiyo asubuhi waliolalamika kuumwa, lakini wale waliokunywa mchana, waliumwa, mamlaka zilisema.

Wanaamini bia hiyo lazima ilitiwa sumu wakati waombolezaji walipokuwa makaburini kuzika.

Mwanamke aliyetengeneza bia hiyo ni miongoni mwa waliokufa.

Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Mamlaka za afya zimeanza kuchangia kwa kupeleka vyakula na vifaa vengine kwa familia zilizoathirika.

Chanzo: AP