Thursday 26 March 2015

MAREKANI YAONYA KUWEPO SHAMBULIO KAMPALA



A crowded street in Kampala. File photo
Marekani yaonya kuwepo shambulio Kampala

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeonya kuwa raia kutoka nchi za kimagharibi – wakiwemo Wamarekani – huenda wakawa wamelengwa kwa mashambulio ya ugaidi katika mji mkuu Kampala.

Ulisema “umepata taarifa za uwezekano wa kuwepo vitisho” kwenye maeneo ya mijini ambapo aghlabu raia wa kigeni hujikusanya.

Shambulio “huenda likatokea hivi karibuni” ilisema, huku ikisema mikutano mengine iliyokuwa imepangwa kufanyika katika hoteli za Kampala imeahirishwa.

Ubalozi huo haujatoa taarifa zaidi. Uganda imeshawahi kushambuliwa siku za nyuma na wapiganji wa Kisomali wa al-Shabab.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

Wednesday 25 March 2015

ALIYEKUWA RAIS WA LIBERIA KUFUNGWA UINGEREZA



 Charles Taylor in court (file photo)

Imetolewa amri kuwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles atatumikia kipindi chake chote cha gerezani Uingereza, baada ya kukataliwa kuhamishiwa Rwanda.

Alisema ananyimwa haki yake ya maisha na familia yake, kwasababu mke wake na watoto wake wamenyimwa viza ya Uingereza.

Majaji walikana kauli yake hiyo, wakisema hawakuomba viza hiyo inavyotakiwa.

Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilimtia hatiani juu ya uhalifu wa kivita kwa kuwaunga mkono waasi waliofanya ukatili Sierra Leone.


JEREMY CLARKSON ATOLEWA TOP GEAR YA BBC



Jeremy Clarkson

Mkataba wa Jeremy Clarkson hautoongezwa baada ya kufanya "shambulio lisilokuwa na uchochezi wowote” kwa msimamizi wa kipindi cha Top Gear, mkurugenzi mkuu wa BBC amethibitisha.

Tony Hall alisema “hakuchukua uamuzi huo kwa uwepesi” na alitambua “itagawanya maoni ya wengi”.

Hata hivyo, aliongeza “alivuka mpaka” na " hawezi kukubaliana na kilichofanyika katika tukio hilo".

Clarkson alisimamishwa kazi Machi 10, kwa kile kilichoitwa “ugomvi” na msimamizi wa Top Gear Oisin Tymon.

Ugomvi huo, uliotokea kwenye hoteli moja huko Yorkshire, inasemwa kuwa ilitokea kwasababu hapakuwepo na chakula cha moto baada ya kufanya kazi siku nzima.

TAKRIBAN WATOTO 500 HAWAJULIKANI WALIPO



Boko Haram leader Abubakar Shekau (12 May 2014)

Takriban watoto 500 wenye umri wa miaka 11 na chini ya hapo hawajulikani walipo katika mji mmoja Nigeria uliotekwa upya na wapiganaji, aliyekuwa mkazi wa Damasak aliiambia BBC.

Mfanyabiashara mmoja wa mji huo ulio kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa Boko Haram waliwachukua watoto hao walipokimbia.

Majeshi kutoka Niger na Chad waliuteka mji wa Damasak mapema mwezi Machi, na kuzima udhibiti wa mji huo kwa miezi kadhaa na wapiganaji hao.

Jesho la eneo hilo hivi karibuni limekuwa likiisaidia Nigeria kupambana na wapiganaji hao.

Maelfu wameuawa tangu mwaka 2009, wakati Boko Haram ilipoanza mapigano kwa nia ya kuunda taifa la Kiislamu.

Monday 23 March 2015

KENYA YAMWACHIA HURU BIBI WA MIAKA 100



Nairobi skyline

Bibi wa miaka 100 ameachiliwa huru kutoka gereza moja nchini Kenya baada ya kufanyika kampeni ya kitaifa ya kutaka aachiwe.

Margaret Ngima alifungwa katika gereza la Embu wiki iliyopita kwa kutoheshimu mahakama baada ya kushindwa kulipa faini ya dola elfu moja.

Bibi huyo wa mabibi alishutumiwa kwa kupuuza amri ya mahakama katika mgogoro wa ardhi na familia nyingine.

Kesi yake ilizusha hasira kali Kenya, na hatimaye faini yake kulipwa na seneta wa Nairobi  Mike Sonko.

Sunday 22 March 2015

DAWA YA MUONGO NI FUPI

     

Vimbwanga vya WhatsApp

WADANGANYIFU 300 WA MITIHANI WAKAMATWA INDIA



Indians climb the wall of a building to help students appearing in an examination in Hajipur, in the eastern Indian state of Bihar
Picha hizi zimewatia aibu mamlaka husika nchini India

Takriban watu 300 wamekamatwa katika jimbo la Bihar nchini India, mamlaka zilisema, baada ya ripoti kuibuka kuwa kulifanyika udanganyifu katika mitihani ya shule.

Wazazi na marafiki wa wanafunzi hao walipigwa picha wakipanda kuta za shule kuwapa majibu.

Wengi waliokamatwa walikuwa wazazi. Takriban wanafunzi 750 walifukuzwa.

Takriban wanafunzi milioni 1.4 wanafanya mitihani katika jimbo hilo la Bihar peke yake – mitihani inayoonekana muhimu kwa kuwapa nafasi ya kujiendeleza katika fani mbalimbali.

Mamlaka bila shaka wameadhirika sana na udanganyifu huo, mwandishi wa BBC alisema, huku tukio hilo likizusha kejeli kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wanafunzi walionekana wakinakili majibu kwenye vikaratasi vilivyopenyezwa, na polisi waliokuwa nje ya vituo vya mitihani walionekana wakipewa hongo wageuke wakijifanya hawaoni.