Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

Saturday 7 February 2015

ALI KIBA AZUNGUMZIA BIFU LAKE NA DIAMOND



Hatimaye staa wa Bongofleva Ali Kiba amekiri kuwa yuko katika bifu na mwanamuziki mwenzie Diamond Platnumz kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Kauli hiyo ya Ali Kiba inapingana na ile ya hivi karibuni iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati za bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisisitiza kuwa wanamuziki hao hawana tofauti zozote na kwamba ni watu tu ndio wanakuza suala hilo.

Hata hivyo, juzi Ali Kiba aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli kuna ugomvi baina yao, huku akisisitiza kwamba tofauti yao ilianza mwaka 2012. Wakati Ali Kiba akifunguka kuhusu bifu hilo hali imekuwa tofauti kwa Diamond ambapo amekaririwa mara kadhaa kuwa hana tofauti yeyote na mwanamuzi huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na kuunganisha Kundi la Kigoma All Stars. Akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali katika mahojiano maalumu, mwanamuziki huyo pia alielezea mambo mengi kuhusu muziki wake na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;

Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?

Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga muda mrefu …Labda watu wahisi kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo wake (alisema bila kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta katika wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.

Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo ule, ila ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri tufanye wimbo mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady Jay Dee.

Swali: Umeshawahi kuwa karibu na Diamond?

Friday 6 February 2015

FAMILIA 'YAMUAGA' BOBBI KRISTINA BROWN



Bobbi Kristina Brown's Family Gathering at Hospital
Si  taarifa amabzo familia ya Bobbi Kristina Brown ingependa kusikia.  
 
Jumatano, siku nne baada ya binti huyo mwenye umri wa miaka 21 kukutwa hana fahamu nyumbani kwake, daktari ameiambia familia yake kuwa hakuna kinachoweza kufanyika .

 "Kila mmoja anakuja hospitali  kusema kwaheri ," alisema mmoja wa wanafamilia.  

Taarifa hizo zilimshtua hasa baba yake, Bobby Brown. "Bobby amekuwa akilia mfululizo tangu jana" kilisema chanzo hicho. "Tunaomboleza."

Mwanafamilia mwengine wa pili alikwenda hospitali usiku kuaga – na kukiri kuwa taarifa hizo za kushtua ni  ngumu sana kuamini.

"Ukimwona, utasema labda kalala tu ," kimesema chanzo hicho.

Chanzo kimoja chenye ukaribu sana na familia hiyo kimesema wamekuwa wakifanya swala karibu na kitanda chake tangu mwanzoni mwa juma  na licha ya taarifa hizo za kushtusha, “bado wana matumaini”.

Chanzo: www.people.com         
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu        

Tuesday 3 February 2015

BOBBI KRISTINA BROWN 'HALI MAHUTUTI'



Whitney Houston (left) and daughter Bobbi Kristina Brown. Photo: 2011
Whitney Houston pamoja na Kristina Brown mwaka 2011

Bobbi Kristina Brown, binti wa mwimbaji marehemu Whitney Houston, "yuko katika hali mbaya” baada ya kukutwa hana fahamu, familia yake imesema.

Bi Brown, mwenye umri wa miaka 21, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumamosi baada ya kukutwa katika hali hiyo ya kupoteza fahamu bafuni nyumbani kwake mjini Atlanta.

Mama yake, aliyekuwa aking’ara duniani kote, alikutwa amefariki dunia Februari 2012, akiwa na umri wa miaka 48, bafuni katika hoteli Los Angeles.

Hospitali haijsema lolote kuhusu hali yake ila familia yake imesema wapo naye.

Taarifa iliyotolewa, na familia ya Bi Brown: "Bobbi Kristina anapambana na amezungukwa na familia yake."

"Tunawaomba mheshimu ombi letu la kutuachia faragha wakati huu mgumu."

Siku ya Jumatatu, polisi walisema waliitwa nyumbani kwake Atlanta siku ya Jumamosi kwa minajil ya mtu “kuzama”.

Afisa mmoja wa polisi aliiambia redio moja kuwa hawakukuta dawa zozote za kulevya nyumbani kwake.

Baba yake Bobbi Kristina ni msanii maarufu wa miondoko ya hip-hop Bobby Brown.

Friday 9 January 2015

MTOTO WA JACKIE CHAN AFUNGWA JELA





Jaycee Chan, mtoto wa kiume wa muigizaji nyota Jackie Chan, amefungwa jela miezi sita kwa kosa linalohusiana na dawa za kulevya.

Chan, mwenye umri wa miaka 32, alikiri kosa kwenye mahakama ya wilaya ya Dongcheng, Beijing kwa “kuhifadhi watu wengine kutumia dawa za kulevya.”

Polisi walivamia nyumbani kwake mwezi Agosti na kukuta zaidi ya gramu 100 za marijuana.

Alikabiliwa na kifungo cha miaka mitatu.

Kukamatwa kwake kulifanyika wakati wa msako mkali wa dawa za kulevya China ambapo watu maarufu kadhaa walijikuta wakikamatwa.

Juni 2014, Rais Xi Jinping walimwamuru polisi kutumia hatua kali kuzuia matumizi ya dawa za kulevya.

Kukiri kwa mtoto wa mmoja wa waigizaji maarufu China kunatoa ujumbe muhimu kutoka serikali ya China: hakuna mwenye kinga ya kukamatwa inapokuja suala la dawa za kulevya.

Sunday 4 January 2015

SELENA GOMEZ AZUA KITAHANANI MSIKITINI




Selena Gomez visits Abu Dhabi's Sheikh Zayed Grand Mosque

Selena Gomez alizua kizaazaa wiki hii baada ya kuonyesha kiwiko chake alipotembelea msikiti – hatahivyo ameitoa picha hiyo baada ya kujikuta akikosolewa na wengi.

Alipigwa picha hiyo alipozuru msikiti mkubwa wa Sheikh Zayed, na alijistiri mwili mzima kwa ajili ya ziara hiyo.

Lakini ilipokuja wakati wa kupiga picha, Selena aliachia kiwiko na sehemu ya mguu hadharani.

Sheria za msikiti huo ziko wazi kuwa sketi zote lazima zifunike mpaka kiwiko, na unakataza ‘tabia zozote za kukaribiana ‘.

Mtu mmoja aliandika: "Kama nia yao ilikuwa kujifunza Uislamu wasingesimama kama wamesimama nje ya bustani.

Selena Gomez

"Nampenda Selena Gomez lakini kufanya jambo kama hili kunanifanya nisiwe mshabiki wake tena."

Mwengine aliongeza: "Si chuki. Lakini angetakiwa kuwa makini zaidi kuhusu misikiti. Ile sehemu ni takatifu na eneo la kuswali. Si sehemu ya kustarehe na kuchukua picha.

Lakini wapo wengine waliomtetea nyota huyo, mmoja akiandika: "Sio kwamba wamewavunjia heshima. Maelfu ya watu hutembelea msikiti huo wa Sheikh Zayed huko Abu Dhabi.

"Ni sehemu ya ibada, ndio najua, lakini Mungu hajawahi kukataza watu wa dini nyingine kuingia msikitini. Kwahiyo tafadhali heshimu kuwa walitaka kujua zaidi kuhusu Uislamu na uzuri wa dini hiyo."

Selena Gomez na muigizaji na mwimbaji kutoka Marekani ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa muimbaji maarufu Justin Bieber.


Chanzo: www.mirror.co.uk                               
Imetafsiriwa na mwandishi wetu

Saturday 3 January 2015

WASANII WA HIP-HOP WANAOLIPWA ZAIDI 'CASH KINGS'

Dr. Dre
Dr Dre

Msemo "count up the cash" mwanzo wa wimbo wa Dr Dre wa Get Your Money Right bila shaka yana ukweli mtupu. 

Hatua yake ya kuiuzia kampuni ya Apple viskilizio vya masikioni (headphones) Beats, mapato yake ya dola milioni 620 katika kipindi cha miaka 12 iliyopita ni makubwa kuwahi kutokea kwa msanii yoyote aliyewahi kufanyiwa tathmini na Forbes.

Jumla ya kipato chake ni zaidi ya pesa kiduchu cha $60 milioni anachopata Jay Z, ambaye aliimba pamoja naye kwenye wimbo wa Get Your Money Right, na Diddy aliyeshika nafasi ya pili.

Kanye West
Kanye West hakufanikiwa kuwa tano bora


Taarifa zilizojiri, kipato cha Dr Dre ni zaidi ya kipato cha wote 24 walioorodheshwa.

Drake amechukua nafasi ya nne akiwa na dola milioni 33 jambo litakalomfurahisha sana, aliwahi kuiambia Forbes "Kama sipo kwenye orodha yenu, ntasikitika sana" mwaka 2013.

Macklemore & Ryan Lewis wa Seattle wenye kuwa na kipato cha dola milioni 32 wamechukua nafasi ya tano, akifuatiwa na Kanye West aliyezalisha dola milioni 30.

Pharrell Williams'
Pharell Williams, aliyetamba sana na kibao cha Happy ameshika nafasi ya tisa


Utajiri wa Birdman $24m, Lil Wayne $23m na $22m za Pharrell Williams unawaweka nafasi ya juu zaidi ya Eminem anaokadiriwa kuwa na utajiri wa takriban $18m na kukamilisha orodha ya 10 bora kwenye miondoko hiyo ya Hip-Hop.

Nicki Minaj ni mwanamke pekee kwenye orodha hiyo akiwa na kipato cha takriban dola milioni 14 licha ya kuondoka American Idol na kutofanya ziara za muziki. 

Ili kuwepo kwenye orodha hiyo, Forbes huangalia kipato kinachotokana kwenye ziara/shoo, mauzo ya rekodi zao, uchapishaji, mauzo ya vifaa mbalimbali nakadhalika.


Friday 12 December 2014

PHARRELL WILLIAMS AZOA TUZO ZA MUZIKI ZA BBC





Pharrell Williams amekuwa king’ara katika tuzo za kwanza za kipekee za muziki za BBC.

Mtayarishaji na mwandishi wa muziki huyo kutoka Marekani alitajwa kuwa msanii bora wa kimataifa na kushinda nyimbo bora ya mwaka kwa kibao chake cha Happy.

Ed Sheeran alitajwa kuwa msanii bora wa mwaka wa Uingereza, na pia aliimba wimbo wake bomba kabisa uliotengenezwa na Pharerell, uitwao Sing, akitumia tu gitaa lake.

Shughuli hiyo pia ilishuhudia wasanii One Direction, Take That na Coldplay wakiimba jukwaani.

Pharrell alishindwa kuhudhuria tuzo hizo, kwani alikuwa akirekodi onyesho la vipaji la Marekani liitwalo The Voice.

Aliunganishwa na sherehe hizo kwa njia ya satelaiti, na kuelezea mafanikio ya kibao hicho cha Happy kuwa ni cha “ajabu” na “si jambo analoweza kuelezea yeye mwenyewe”.