Wednesday, 3 September 2014

MOTO WAKATIZA BIG BROTHER AFRIKA



Big Brother winner Cherise Makubale
Cherise Makubale wa Zambia alikuwa mshindi wa kwanza wa Big Brother Africa 



Uzinduzi wa mfululizo wa Big Brother Afrika umecheleweshwa kutokana na moto mkubwa uliotokea katika studio zao maalum mjini Johannesburg.

Kipindi hichi, kilichotarajiwa kuanza Jumapili, kimesimamishwa huku watayarishaji wanajaribu kutafuta nyumba mbadala “haraka iwezekanavyo”

Hakuna aliyejeruhiwa kwenye moto huo na sababu haitojulikana mpaka uchunguzi utakapofanyika.

Washindani kutoka nchi 14 walitarajiwa kushiriki kwenye kipindi hicho ikiwa ni cha tisa.

Kilitarajiwa kuwepo kwa siku 91 kabla ya kupata mshindi wa kumrithi yule wa mwaka jana Dilish Matthews kutoka Namibia.

Mshindi wa mwaka huu anatarajiwa kushinda dola za kimarekani 300,000, sawa na kiwango kilichotolewa mwaka 2013.

Watengenezaji wa kipindi hicho Endemol South Africa na M-Net wamesema jitihada za kutafuta jengo jengine ili kurekodi kipindi hicho itakuwa ngumu katika kipindi kifupi kutokana na “ubora wa miundo mbinu” ambayo haitopatikana haraka.

Kila jitihada itafanyika kutafuta suluhu haraka iwezekanavyo ili kipindi hicho kinachotazamwa na idadi kubwa ya watu Afrika kiendelee,” waliongeza.

Channel 24 imesema tayari matayarisho yalipatwa na mtikisiko baada ya washindani kutoka Ghana walipokabiliwa na matatizo ya kupata viza na badala yake kuchukuliwa Waghana ambao tayari ni wakazi wa Afrika Kusini.

Washiriki wa Rwanda- kwa mara ya kwanza- na Sierra Leone nao pia ilibidi wafutwe.
Kipindi hicho kipya kilitarajiwa kuonyeshwa kote barani Afrika kupitia satelaiti.

Big Brother imekuwa maarufu sana tangu ilipoanza mwaka 2003, na imepata washindi kutoka Tanzania, Angola, Nigeria, Namibia, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Mshindi wa kwanza, Cherise Makubale, alitokea Zambia.

Mwaka 2010, kipindi hicho kilirindima kwenye vichwa mbalimbali vya habari duniani baada ya mmoja wa washiriki wa kiume  alipotolewa kwenye jumba hilo la Big Brother kwa kumpiga ngumi mshiriki wa kike.

Awali watengenezaji wa kipindi hicho nchini Afrika Kusini walimruhusu Hannington Kuteesa kubaki kwenye kipindi hicho, jambo liliosababaisha malalamiko mazito.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na mwandishi wetu
 

UNAPOBAMBWA NA MWANAO

Vimbwanga vya WhatsApp

Tuesday, 2 September 2014

IS YATUHUMIWA KWA MAUAJI YA KIMBARI




 A member of the Iraqi Shiite militia, Kataib Hezbollah (Hezbollah Brigades), aims his rifle during fighting against Islamic State (IS) fighters, in Amerli town (1 September 2014)


Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema lina ushahidi mpya kuwa wapiganaji wa Islamic State wamefanya mauaji ya kimbari kaskazini mwa Iraq.

Shirika hilo limesema kundi hilo la IS limegeuza eneo hilo kuwa “uwanja wa ukatili wa kumwaga damu”.

Awali Umoja wa Mataifa ulitangaza kutuma wataalamu Iraq kuchunguza “vitendo vinavyokiuka haki za binadamu kwa kiwango kisichofikirika”.

IS na waasi washirika wa Ki-Sunni wameteka maeneo makubwa ya Iraq na Syria.

Maelfu ya watu wameuawa, wengi wao wakiwa raia, na zaidi ya milioni wamelazimika kukimbia makazi yao katika miezi ya hivi karibuni.

Amnesty imesema imekusanya ushahidi kuwa kumekuwa na mauaji ya watu wengi yaliyofanyika kaskazini mwa mji wa Sinjar mwezi Agosti. Matukio mawili ya kutisha yalifanyika baada ya wapiganaji wa IS walipovamia vijiji na kuua mamia ya watu Agosti 3 na 15.

“Makundi ya wanaume na vijana wa kiume wakiwemo watoto wa chini ya miaka 12 kutoka vijiji vyote viwili walitekwa na wapiganaji wa IS, wakachukuliwa na kufyatuliwa risasi,” shirika hilo lenye makao makuu Uingereza limesema.

Naibu Kamishna wa haki za binadamu Flavia Pansieri ameonya IS (mwanzo ikijulikana kama ISIS) ilikuwa ikiwalenga Wakristo, Wayazidi, Wa-Shabak, Wa-Sabea na jumuiya za Kishia “kupitia mauaji ya kikatili kupita kiasi”.

Chanzo: BBC

NDEGE YA KENYA YAANGUKA TANZANIA


Masalia ya ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited iliyoanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti 

Ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited imeanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwateketeza watu watatu waliokuwamo ndani.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa katika harakati za kuitafuta.

Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia.

Meneja wa Udhibiti wa JKIA, Clever Davor aliliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada ya uwanja huo ikiwa imeruka angani urefu wa futi 14,000.

Awali, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KCAA) ilitoa taarifa juu ya kuchelewa kwa ndege hiyo iliyokuwa ikitarajiwa kutua katika uwanja wa JKIA saa 2 usiku.

Jana asubuhi, Kamanda wa Viwanja vya Ndege wa Kenya (KAPU), Joseph Ole Tito alithibitisha kupotea kwa ndege hiyo kabla ya kuonekana baadaye katika Hifadhi ya Serengeti.

Polisi wa Kenya hawakueleza ndege hiyo ya mizigo aina ya Fokker F-27-500 ilikuja nchini kwa shughuli gani.

Ndege zote zinazotoka Kenya kwenda nchi za jirani, huanzia safari zake katika viwanja vya JKIA, Wilson au Wajir ili kuwa na usimamizi wa karibu.

Chanzo: Mwananchi, Tanzania

KENYA KUPAMBANA NA "WAFANYAKAZI HEWA"




Kenya's President Uhuru Kenyatta addresses the nation at Nyayo national stadium in Nairobi, 1 June 2014
RaisUhuru  Kenyatta alikuwa wa kwanza kujisajili kama mfanyakazi wa serikali


Kenya imeanza kuwasajili wafanyakazi wote wa serikali kwa njia ya elektroniki (biometrically) katika jaribio la kuondosha “wafanyakazi hewa”

Wafanyakazi watakaoshindwa kujisajili katika kipindi cha wiki mbili zijazo hawatoendelea kulipwa, taarifa ya serikali imesema.

Serikali ina shuku kuwa maelfu ya watu wanaendelea kupokea mishahara baada ya kuacha kazi serikalini.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa wa kwanza kujisajili- ameahidi kupambana na rushwa.

‘Kupoteza muda’          

“Ni kwa faida yenu kujisajili la sivyo utaonekana kama mfanyakazi hewa” aliwaambia wafanyakazi katika pwani ya Mombasa.

Mapema mwaka huu mkaguzi wa mahesabu aligundua takriban dola milioni moja kwa mwezi hupotea kwa “wafanyakazi hewa”.

Wafanyakazi wote wa serikali wanatakiwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo kufika kwenye vituo vya utambulisho kuhakikisha taarifa zao zinachukuliwa kwenye mchakato huo wa kujisajili, taarifa ya serikali inasema.

Taarifa hiyo imesema, yeyote atakayeshindwa kufika kituoni hapo bila sababu yoyote ya msingi atatolewa kwenye mchakato wa malipo ya mshahara.

Katika kituo kimoja Nairobi, mwandishi wa BBC Paul Nabiswa amesema maafisa walikuwa wakichukua utambulisho kama vile alama za vidole na kutaka ushahidi wa viwango vyao vya elimu kabla ya kuwapa kitambulisho kuwa taarifa zao zimechukuliwa.

Anasema kumekuwa na hisia tofauti

“Huku ni kupoteza muda” Mfanyakazi wa manisapaa ya Nairobi Henry Okello alisema.

"Watu hawatofanya kazi, watakaa kwenye foleni mpaka dakika ya mwisho- kwanini wasije kutuhesabu maofisni?” alihoji.

Monday, 1 September 2014

URUSI YAISIHI UKRAINE: MAZUNGUMZO YA AMANI



Pro-Russian rebel in Donetsk region (31 August 2014)
Waasi wanaounga mkono Urusi wamekuwa wakidhibiti maeneoe mengi Ukraine siku za karibuni
Hatua ya “kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo” Ukraine lazima ipewe kipaumbele katika mazungumzo muhimu yanayofanyika Jumatatu, waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema.

Majeshi ya Ukraine “lazima yaondoke maeneo wanaoweza kuwadhuru raia” amesema Sergei Lavrov.

Maafisa wa Ukraine na Urusi wanatarajia kufanya mazungumzo na waasi na waangalizi wa kimataifa kwenye mji mkuu wa Belarus, Minsk.

Takriban watu 2,600 wamekufa mashariki mwa Ukraine tangu mapigano kuanza mwezi Aprili.

Mapigano hayo yaliibuka baada ya upande wa kusini wa Ukraine, Crimea kujitenga mwezi Machi.

Mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja yaliyofanyika wiki iliyopita baina ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenziwe wa Ukraine Petro Poroshenko hayakuzaa matunda yoyote.

Waasi wamezidi kutanda kwenye ardhi ya Ukraine katika siku za hivi karibuni, katika miji yote miwili ya Luhansk na Donetsk, na upande wa kusini zaidi maeneo ya bandari ya Mariupol.

Msemaji wa jeshi la Ukraine Leonid Matyukhin amesema majeshi yalikuwa yakipambana na vifaru vya Urusi katika mji wa Luhansk.

Ripoti zilizotolewa usiku zinasema waasi wamedhibiti uwanja wa ndege.

Chanzo: BBC             
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

KATIBA BADO KIZAAZAA, TANZANIA



Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana waligoma mbele ya Rais Jakaya Kikwete kuruhusu wajumbe wao kurejea katika Bunge Maalumu la Katiba, walipokutana katika kikao cha kusaka suluhu ya mkwamo wa mchakato wa Katiba.

Mkutano wa jana ulikuwa na sehemu mbili kuu, wa kwanza ulifanyika katika Ikulu ya Kilimani, Dodoma ambako viongozi hao walikutana na Rais Kikwete na mwingine katika Hoteli ya St. Gasper ambao uliwashirikisha viongozi na maofisa wa vyama vilivyoshiriki bila Rais Kikwete.

Mkutano huo ni matunda ya jitihada zinazofanywa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambacho kiliratibu mazungumzo hayo yaliyochukua zaidi ya saa mbili na nusu, katika Ikulu ya Kilimani, wakati yale ya St. Gaspar yalichukua takriban saa moja na nusu.

Viongozi walioshiriki kikao hicho cha Ikulu ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara), Magdalena Sakaya.

Wengine ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Katibu Mkuu wake, Mosena Nyambabe, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa UDP ambaye pia ndiye mwenye zamu ya uenyekiti wa TCD, John Cheyo na Mwenyekiti wa UPDP pamoja na mwakilishi wa vyama visivyokuwa na wabunge ndani ya TCD, Fahmi Dovutwa.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Rais Kikwete baada ya kuanza kwa kikao hicho alitoa fursa kwa kila aliyekuwapo kuzungumza na hapo zilijitokeza hoja mbalimbali, nyingi mwelekeo wake ukiwa ni kutaka kusitishwa kwa Bunge Maalumu ili kutoa fursa kwa nchi kuendelea na masuala mengine makubwa.

Chanzo chetu kilisema: “Rais amekuwa msikivu kweli, amewasikiliza wote lakini ugumu ulianza kuonekana pale ilipotolewa kauli ya kuwauliza wale watu wa Ukawa kama wanaonaje wakirejea halafu hoja zao zikazungumzwa ndani ya Bunge Maalumu, yaani hawataki kabisa kusikia hilo.”

Kuhusu hoja ya kusitishwa kwa Bunge, habari zinasema ilijadiliwa kwa kirefu na wataalamu wa sheria wakijaribu kutoa uzoefu wao, lakini kikwazo kilichoonekana ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo haimpi Rais mamlaka ya kusitisha Bunge.

“Rais alisema hoja zao ni nzuri na zina mashiko, lakini suala kubwa likawa ni kwamba tunafikaje huko wanakopendekeza? Maana sheria iko kimya kuhusu mamlaka ya Rais kusitisha Bunge Maalumu, ndiyo maana sasa tulitoka Ikulu tukaenda St. Gaspar ili kujadili, ngoja tusubiri hiyo tarehe 8 maana siyo mbali,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

Kwa taarifa zaidi, bonyeza hapa http://bit.ly/1vCIxPA

Chanzo: Mwananchi, Tanzania

GHADHABU DHIDI YA DIAMOND, UJERUMANI



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu8s4lWHtsuZm__YwPa-unU0UZnTZuTAFuPBKmeBNsTnSVTxCTAtVVtNY-aNr3gHFzZ0pEO2FIol85de1k4ta66-x1jVqTEFe9xH2bAc6Iykbr-85qgIojHp_8Ma0nfDTi0X4TQpAf9iye/s1600/huu+ndio+ukumbi+uliharibiwa+na+washabiki+mjini+stuttgart,ujerumani.jpg

  • Kashindwa kuwika Stuttgart, kisa na mkasa?
  • Kafika ukumbini saa 10 alfajiri, washabiki wanasubiri show tangu saa 4 usiku
  • Promoja Mjaijeria aingia mitini.
  • Dj apata kisago, eti vyombo vibovu. Aibu!
Stuttgart, Ujerumani - Usiku wa Jumamosi ya tarehe 30 Agosti 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor,  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.

Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki.

Ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa. Mmoja wa Djs hao alipoteza laptop yake, mwanadada Dj Flor alipatwa shock (mstuko wa moyo) na kukimbizwa hosptali.
Washabiki hao walimpa kipigo Dj Drazee ambaye naye yupo hoi hospitalini. 
Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu alijawahi kutokea. Kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND" link:

http://www.stuttgarter-nachrichten.de/inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-fe25d10b6ed9.html


Chanzo: wavuti.com

DIRISHA LA USAJILI 2014/2015

Unaweza kusikia kuhama kwa mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez kwenda Real Madrid.
Javier Hernandez anaweza kutimkia Real Madrid.
Javier Hernandez anaweza kutimkia Real Madrid
Queens Park Rangers wanahusishwa na kuhama kwa mshambuliaji wa zamani wa Spurs Jermain Defoe. Klabu ya Toronto FC ya Canada imeeleza kuwa itakuwa na furaha zaidi kurejea kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza.
West Ham United nao wamegeuza kibao kwa mlinzi wa Manchester City Micah Richards.

Richards, 26, anajiandaa kujiunga Fiorentina kwa mkopo. Mshahara wake utakuwa pauni 75,000 kwa wiki, Micah ameonekana kuwa tatizo kwa Hammers.

Baada ya West Ham kugoma kumnyakuwa Fiorentina wameonyesha nia na Micah Richards.
Baada ya West Ham kugoma kumnyakua Fiorentina wameonyesha nia na Micah Richards
Baada ya West Ham kugoma kumnyakua Fiorentina wameonyesha nia na Micah Richards.

Lakini sasa tunasikia kwamba mchezaji Nick Powell wa Man U anatarajiwa kuhamia Leicester kwa mkopo.

Baada ya tetesi kwamba mshambuliaji Radamel Falcao atajiunga na Real Madrid kugonga mwamba, inaonekana kwamba Manchester City ndio wako mbioni kumnyakua.

Real Madrid. Hapana. Radamel Falcao anaweza kuondoka Monaco na kwenda Etihad.
 Radamel Falcao anaweza kuondoka Monaco na kwenda Etihad
Real Madrid. Hapana. Radamel Falcao anaweza kuondoka Monaco na kwenda Etihad.

Hata hivyo Alvaro Negredo amefunguliwa mlango na kwenda Valencia, na kutoa nafasi City kwa ajili ya kumleta mshambuliaji wa kati.

Arturo Vidal na Danny Welbeck nao pia wanaweza kuondoka kwenye vilabu vyao.

Kiungo wa Juventus Arturo Vidal anauzwa kwa ada ya pauni milioni 30.
Kiungo wa Juventus Arturo Vidal anauzwa kwa ada ya pauni milioni 30
Dirisha la usajili kufungwa saa 5 usiku leo Jumatatu.

Taarifa za usajili zitaendelea kukujia.

Chanzo: taarifa.co.tz

BI MUGABE AJIKITA KWENYE SIASA ZIMBABWE


Grace Mugabe, 49, ana watoto watatu na Rais Mugabe
Grace Mugabe, 49, ana watoto watatu na Rais Mugabe
Mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amejiunga na siasa baada ya kupitishwa kuwa kiongozi wa jumuiya ya wanawake wa chama tawala cha Zanu-PF.

Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 49, ataanza kushikilia wadhifa huo mwezi Desemba katika mkutano mkuu wa mwaka.

Mwandishi wa BBC Brian Hungwe wa Zimbabwe anasema nafasi hiyo itampa fursa Bi Mugabe kushiriki kwenye kamati muhimu za kutunga sera za chama cha Zanu-PF.

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya Zanu-PF wa nani atamrithi Bwana Mugabe, ambaye alichaguliwa tena kuwa Rais mwaka jana.
Robert Mugabe, 90, ameongoza tangu Zimbawe ilipopata uhuru mwaka 1980
Robert Mugabe, 90, ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980
Bi Mugabe alipendekezwa rasmi kuwa katibu mkuu wa jumuiya ya wanawake ya Zanu-PF katika uchaguzi uliofanyika mji mkuu Harare.
Uchaguzi huo ulihutubiwa na mumewe mwenye umri wa miaka 90, ambaye ameiongoza Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1980.

Ni mke wake wa pili na alikuwa katibu muhtasi wake. Walioana mwaka 1996 na wana watoto watatu.

Mwandishi wa BBC anasema kuingia kwake kwenye siasa bila shaka kutachochea wasiwasi zaidi juu ya mrithi wa Bwana Mugabe.