Monday, 1 September 2014

BI MUGABE AJIKITA KWENYE SIASA ZIMBABWE


Grace Mugabe, 49, ana watoto watatu na Rais Mugabe
Grace Mugabe, 49, ana watoto watatu na Rais Mugabe
Mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amejiunga na siasa baada ya kupitishwa kuwa kiongozi wa jumuiya ya wanawake wa chama tawala cha Zanu-PF.

Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 49, ataanza kushikilia wadhifa huo mwezi Desemba katika mkutano mkuu wa mwaka.

Mwandishi wa BBC Brian Hungwe wa Zimbabwe anasema nafasi hiyo itampa fursa Bi Mugabe kushiriki kwenye kamati muhimu za kutunga sera za chama cha Zanu-PF.

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya Zanu-PF wa nani atamrithi Bwana Mugabe, ambaye alichaguliwa tena kuwa Rais mwaka jana.
Robert Mugabe, 90, ameongoza tangu Zimbawe ilipopata uhuru mwaka 1980
Robert Mugabe, 90, ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980
Bi Mugabe alipendekezwa rasmi kuwa katibu mkuu wa jumuiya ya wanawake ya Zanu-PF katika uchaguzi uliofanyika mji mkuu Harare.
Uchaguzi huo ulihutubiwa na mumewe mwenye umri wa miaka 90, ambaye ameiongoza Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1980.

Ni mke wake wa pili na alikuwa katibu muhtasi wake. Walioana mwaka 1996 na wana watoto watatu.

Mwandishi wa BBC anasema kuingia kwake kwenye siasa bila shaka kutachochea wasiwasi zaidi juu ya mrithi wa Bwana Mugabe.

No comments:

Post a Comment