Waasi wanaounga mkono Urusi wamekuwa wakidhibiti maeneoe mengi Ukraine siku za karibuni |
Majeshi ya Ukraine “lazima yaondoke maeneo wanaoweza kuwadhuru raia” amesema Sergei Lavrov.
Maafisa wa Ukraine na Urusi wanatarajia kufanya mazungumzo na waasi na waangalizi wa kimataifa kwenye mji mkuu wa Belarus, Minsk.
Takriban watu 2,600 wamekufa mashariki mwa Ukraine tangu mapigano kuanza mwezi Aprili.
Mapigano hayo yaliibuka baada ya upande wa kusini wa Ukraine, Crimea kujitenga mwezi Machi.
Mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja yaliyofanyika wiki iliyopita baina ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenziwe wa Ukraine Petro Poroshenko hayakuzaa matunda yoyote.
Waasi wamezidi kutanda kwenye ardhi ya Ukraine katika siku za hivi karibuni, katika miji yote miwili ya Luhansk na Donetsk, na upande wa kusini zaidi maeneo ya bandari ya Mariupol.
Msemaji wa jeshi la Ukraine Leonid Matyukhin amesema majeshi yalikuwa yakipambana na vifaru vya Urusi katika mji wa Luhansk.
Ripoti zilizotolewa usiku zinasema waasi wamedhibiti uwanja wa ndege.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment