Tuesday, 2 September 2014

KENYA KUPAMBANA NA "WAFANYAKAZI HEWA"




Kenya's President Uhuru Kenyatta addresses the nation at Nyayo national stadium in Nairobi, 1 June 2014
RaisUhuru  Kenyatta alikuwa wa kwanza kujisajili kama mfanyakazi wa serikali


Kenya imeanza kuwasajili wafanyakazi wote wa serikali kwa njia ya elektroniki (biometrically) katika jaribio la kuondosha “wafanyakazi hewa”

Wafanyakazi watakaoshindwa kujisajili katika kipindi cha wiki mbili zijazo hawatoendelea kulipwa, taarifa ya serikali imesema.

Serikali ina shuku kuwa maelfu ya watu wanaendelea kupokea mishahara baada ya kuacha kazi serikalini.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa wa kwanza kujisajili- ameahidi kupambana na rushwa.

‘Kupoteza muda’          

“Ni kwa faida yenu kujisajili la sivyo utaonekana kama mfanyakazi hewa” aliwaambia wafanyakazi katika pwani ya Mombasa.

Mapema mwaka huu mkaguzi wa mahesabu aligundua takriban dola milioni moja kwa mwezi hupotea kwa “wafanyakazi hewa”.

Wafanyakazi wote wa serikali wanatakiwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo kufika kwenye vituo vya utambulisho kuhakikisha taarifa zao zinachukuliwa kwenye mchakato huo wa kujisajili, taarifa ya serikali inasema.

Taarifa hiyo imesema, yeyote atakayeshindwa kufika kituoni hapo bila sababu yoyote ya msingi atatolewa kwenye mchakato wa malipo ya mshahara.

Katika kituo kimoja Nairobi, mwandishi wa BBC Paul Nabiswa amesema maafisa walikuwa wakichukua utambulisho kama vile alama za vidole na kutaka ushahidi wa viwango vyao vya elimu kabla ya kuwapa kitambulisho kuwa taarifa zao zimechukuliwa.

Anasema kumekuwa na hisia tofauti

“Huku ni kupoteza muda” Mfanyakazi wa manisapaa ya Nairobi Henry Okello alisema.

"Watu hawatofanya kazi, watakaa kwenye foleni mpaka dakika ya mwisho- kwanini wasije kutuhesabu maofisni?” alihoji.

No comments:

Post a Comment