Thursday, 11 September 2014

BILL GATES ATOA FEDHA KUPAMBANA NA EBOLA



 Liberian health care workers on an Ebola burial team collect the body of an Ebola victim at a motor vehicle garage in Paynesville on the outskirts of Monrovia, Liberia (9 September 2014)
Fedha zaidi zimetangazwa kusaidia dharura iliyopo kusaidia katika kupambana na mlipuko wa Ebola, Afrika magharibi.

Wakfu wa Bill Gates inatoa dola za kimarekani milioni 50 kusaidia jitihada za kupambana na kirusi hatari kwenye nchi zilizoathirika.

Msaada huu unatolewa kuongezea fedha nyingine zilizotangazwa na serikali za Uingereza na Marekani, pamoja na Umoja wa Ulaya.

Lakini baadhi ya mashirika ya kutoa misaada ilisema kinachohitajika zaidi na haraka barani Afrika ni wataalam wa kuweza kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo.

Wakfu wa Gates – ulioundwa na muasisi wa Microsoft Bill Gates na mkewe Melinda imesema itatoa haraka iwezekanavyo “fedha zinazohitajika” kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yanayohusika na mpambano dhidi ya Ebola, ili kununua vifaa vinavyotakiwa.

Na imesema itafanya kazi bega kwa bega na washirika wengine kuharakisha utengenezaji wa dawa na chanjo dhidi ya virusi hivyo, ambavyo vimesababisha takriban vifo vya watu 2,300.

MTANZANIA ACHAGULIWA MAKAMU RAIS WA BET NETWORK




BET Networks, shina la Viacom Inc. (NASDAQ: VIA, VIAB), imetangaza kumwajiri Kay Madati kuwa Makamu wa Rais na Afisa Mkuu wa Digitali.

Madati, raia wa Tanzania aliyeishi Afrika, Uingereza na Marekani, ataiongoza timu nzima ya BET katika nyanya zote za kidigitali, mchakato wa masuala ya simu na mitandao ya kijamii na pia kusimamia shughuli zote za ubunifu, teknolojia na maendeleo katika mfumo mzima wa BET hasa unaohusika na masuala ya kidigitali.

Kabla ya kuteuliwa huko BET, hivi karibuni Madati alikuwa Mkuu wa Burudani na Habari Facebook Inc.

Yeye na timu yake walisaidia kuifanya Facebook Inc. kuwa mshirika mkuu upande wa kidigitali na kwenye mitandao ya kijamii kwa kushirikiana na studio za filamu, mifumo ya televisheni na makampuni ya burudani.

Kabla ya kujiunga na kampuni hiyo mwaka 2011, Madati alikuwa Makamu Rais wa kutathmini tabia za watazamaji/wasikilizaji kwa kupata habari CNN Worldwide na pia aliwahi kufanya kazi upande wa masoko Octagon Worldwide na BMW ya Amerika Kaskazini.




Chanzo: www.forbes.com

Wednesday, 10 September 2014

WATANZANIA 2 NA WANYARWANDA 2 WAFUNGWA AFRIKA KUSINI


Gen Faustin Kayumba Nyamwasa in court in Kagiso near Krugersdorp on 28 August 2014
Jenerali Nyamwasa ameilaumu serikali ya Rwanda kuhusika na ufyatuliaji risasi

 Mahakama ya Afrika kusini imewahukumu watu wanne kufungwa miaka nane jela kwa kosa la jaribio la kumwuua aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa.

Alipigwa risasi tumboni mjini Johannesburg Juni 2010, siku chache baada ya kukimbia Rwanda baada ya mfarakano na Rais Paul Kagame.

Hakimu mkazi alisema “watuhumiwa wakuu” hawajakamatwa.

Mashambulio kadhaa dhidi ya waombaji hifadhi wa Rwanda nchini Afrika kusini yamesababaisha mvutano wa kidiplomasia baina ya Pretoria na Kigali.

Serikali ya Rwanda imekana kabisa kuhusika na mauaji ya wapinzani wake Afrika Kusini.

'Bado wana woga '

Upande wa mwendesha mashtaka ulitaka wapewe kifungo cha miaka 15 kwa Wanyarwanda wawili, Amani Uriwane na Sady Abdou, na Watanzania wawili Hassan Mohammedi Nduli na Hemedi Dendengo Sefu,waliotiwa hatiani kwa jaribio la mauaji.

Kuwapa kifungo cha miaka minane kila mmoja, Hakimu Stanley Mkhari alisema kuwa watu hao walikuwa kizuizini tangu tukio hilo la ufyatuaji risasi kutokea.

"Nyie si watuhumiwa wakuu katika suala hili. Kwa maoni yangu mlitakiwa kuwa mbele yangu na wote waliowezesha pesa kupatikana na waliowafadhili kufanya uhalifu huo," amenukuliwa akisema.

Wanaume wengine wawili waliachiwa huru kwa kuhusishwa na kosa hilo mwezi uliopita.

Jenerali Nyamwasa alisema alikuwa amefurahi baada ya kutolewa uamuzi wa hukumu hiyo, lakini bado ana wasiwasi na usalama wa Wanyarwanda waishio uhamishoni, shirika la habari la Reuters limesema.

 

FAIDA YA MAN UNITED 'KUTETEREKA'


Aliyekuwa meneja wa Man United, David Moyes


Manchester United imetangaza kuporomoka kwa faida ya kila mwaka wa fedha katika mwaka ambao David Moyes alikuwa meneja. 

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema kipato halisi kimeporomoka kwa asilimia 84 na kufikia takriban dola milioni 45. 

Klabu hiyo imesema inatarajia mapato yake ya mwaka 2015 kushuka kutokana na klabu hiyo kushindwa kufuzu kucheza Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 1994-95. 

Klabu hiyo imesema Moyes na wasaidizi wake walilipwa zaidi ya dola milioni 8 kama fidia kufuatia kufukuzwa kazi mwezi Aprili, chini ya mwaka mmoja tangu apewe kazi hiyo.

Chanzo: FB - Salim Kikeke

ATI MTU 'MWEUSI' ANAKULA TOFAUTI NA 'MWEUPE'




Vimbwanga vya WhatsApp

URAIA PACHA BADO NGOMA NZITO



URAIA pacha kwa Watanzania walioko nje ya nchi jana uliendelea kutawala katika mijadala kwenye Bunge la Katiba huku wengi waliochangia wakikubaliana wasio na uraia Katiba iruhusu wapewe chini ya utaratibu wa uraia wa pacha.

Wachangiaji wengi walisema hakuna sababu ya kuwanyima uraia hao kwa kisingizio kuwa sio wazalendo.

Selemani Ali alisema Watanzania walioenda nje ya nchi kusaka maisha umefika wakati warejeshewe uraia wao kwani watapata fursa pia ya kufaidika na matunda ya nchi yao.

Lakini Luis Majaliwa alisema Watanzania hao hawana hadhi ya kupewa uraia kwa sababu si wazalendo kwani walikimbia nchi kwa kuona maisha ni magumu na kuwaacha wenzao wanahangaika kuikwamua nchi kwenye maendeleo.

Alisema, “iweje leo hii walioacha jahazi linazama waona mambo yanaenda vizuri waruhusiwe kuja kupewa tena uraia.”

RAIS KIKWETE HATAONGEZA MUDA BUNGE LA KATIBA

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania, John Cheyo akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, alipokuwa akitoa tamko kuhusu mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kutaka Bunge Maalumu lifikie ukomo Oktoba 4, mwaka huu yamezua sintofahamu mjini hapa huku uamuzi huo ukionekana kuwachanganya viongozi wa Bunge hilo.

Kutwa nzima ya jana, viongozi wa Bunge Maalumu walishinda kwenye vikao vya mashauriano huku wabunge wa CCM wakitarajiwa kukutana jana usiku kwenye makao makuu ya chama hicho kupewa taarifa rasmi za uamuzi huo.

Katika makubaliano baina ya TCD na Rais Kikwete, imeamuliwa kuwa uamuzi wa Rais kupitia Tangazo la Serikali (GN) 254 la kuongeza siku 60 hadi Oktoba 4 uheshimiwe na baada ya tarehe hiyo Bunge liahirishwe.

Uamuzi huo ni kinyume cha azimio la Bunge Maalumu la Agosti 5, 2014 ambalo lilirekebisha Kanuni ya 14 (4) na kuifuta Jumamosi katika siku zilizotajwa kuwa za kazi, pia sikukuu na siku za Jumapili.

Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alikaririwa akiwaambia wajumbe wa Bunge hilo kwamba Rais alikuwa ameridhia kwamba siku 60 alizotoa hazingejumuisha Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi, Tanzania

MIFUPA YA DINOSARIA YAPATIKANA TANZANIA

Aina mpya ya Dinosaria (Dinosaurs)  imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania.

Mabaki hayo ya Dinosaria yaliyopewa jina la – ‘Rukwatitan Bisepultus’ – yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

baadhi ya mifupa ya  mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa
Baadhi ya mifupa ya mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa
Baadhi ya mifupa ya mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa

Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka  milioni 100 iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili.

Mnyama huyo ni aina ya Titanosaurus ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi.

Gorscak etal_Fig 3_Silhouette

Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chokaa iliumbika) takriban miaka milioni 140 iliyopita.

Eneo la bonde yalikopatikana mabaki ya mnyama huyo mkubwa. Picha kwa hisani ya Patrick O’Connor wa Ohio University

Tanzania ina historia ya kuwa na wanyama hao wakubwa.Mwaka 1906 wanasayansi kutoka Ujerumani waligundua mabaki ya dinosaria kule Tendaguru, Lindi, wakayafukua na kuyapeleka Ujerumani ambako yamehifadhiwa tangu wakati huo.

Je, mifupa hiyo iliyogundulika Rukwa itabaki Tanzania iwe kivutio cha utalii na utafiti au itatoka nje ya nchi?

Chanzo: taarifa.co.tz