Thursday, 27 November 2014

GHANA YAKUMBWA NA KASHFA YA 'DAWA ZA KULEVYA'


map





Upande wa upinzani nchini Ghana umetoa wito wa kuwepo  uchunguzi wa bunge katika madai kuwa muuzaji mmoja wa dawa za kulevya aina ya cocaine alikuwa na uwezo wa kuingia katika sehemu maalum ya mapumziko ya rais kwenye uwanja mkuu wa ndege nchini humo.

Anayedaiwa kuwa muuzaji alikamatwa nchini Uingereza, huku maafisa watatu wamefunguliwa mashtaka Ghana.

Tukio hilo limekuwa gumzo miongoni mwa raia wa Ghana, wakati upinzani na chama tawala wakishutumiana kuhusu biashara ya dawa za kulevya.

Afrika magharibi ni njia kuu ya mpito ya kupitisha dawa hizo kimagendo barani Ulaya.

Serikali imekana kuhusika kwa namna yoyote na tukio hilo kwa kile redio za nchi hiyo zilivyoiita “kashfa ya cocaine”.

Rais John Mahama pia amekana vikali taarifa kuwa Bi Nayele Ametefe aliyekamatwa uwanja wa ndege wa Heathrow Novemba 9, ana uhusiano na familia yake.




Wednesday, 26 November 2014

RIPOTI YA TEGETA ESCROW ILIYOSOMWA BUNGENI, TZ

Yasemekana hawakulala Wabunge hawa, walikesha hivi wakiilinda ripoti
                                            


 Ripoti hii ya kusikiliza kwa bahati mbaya imeanzia katikati japo ni dakika chache tu za mwanzo


Chanzo: wavuti.com

ZITTO AHOJIWA NA BBC KUHUSU KASHFA YA ESCROW


 
Kashfa ya TegetaEscrow inazidi kufukuta nchini Tanzania. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo aliwasilisha ripoti ya uchunguzi katika bunge la nchi hiyo. Katika matangazo ya Dira ya Dunia TV, Zuhura Yunus alimhoji mbunge huyo kujua zaidi.

Tuesday, 25 November 2014

MAHAKAMANI KWA KUMFANYA BINTI KUWA 'MWEUPE'





 






















Halle Berry amempeleka aliyekuwa mpenzi wake Gabriel Aubry mahakamani kwa madai ya kutaka kubadilisha muonekano wa binti yao ili awe mweupe.

Anadai Aubry amezinyoosha nywele za Nahla zilizojinyonganyonga na kuzipaka rangi kwa nia ya kumfanya asionekane Mmarekani mweusi.

Nyaraka za mahakamani zinamshutumu Aubry kwa kumsababishia “uharibifu wa kisaikolojia na wa mwili” kwa binti yao mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia aanze kuwaza “kwanini muonekano wake wa asili hautoshi ”.

 “Nataka mimi na Gabriel tuchukue uamuzi pamoja juu ya binti yetu, ukuaji wake, maendeleo yake na maisha yake kwa ujumla,” alisema Berry kwenye nyaraka hizo.

Wakili wa Berry, Steve Kolodny, ndie aliyekuwepo mahakamani siku ya Jumatatu pamoja na Aubry.
Jaji alitoa uamuzi kuwa hakuna mzazi hata mmoja anayeweza kubadili muonekano wa Nahla kutoka asili yake.

Wapenzi hao waliachana mwaka 2010 baada ya kuwa pamoja kwa miaka minne.


Chanzo: www.independent.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
 

WAKENYA WAKIMBIA BAADA YA SHAMBULIO


Protesters in Nairobi (25 November 2014)

Mamia ya watu wamekimbilia uwanja mdogo wa jeshi katika mji wa Mandera nchini Kenya kukiwa na hofu ya wapiganaji kuanzisha mashambulio upya.

Wengi waliokimbia nia wafanyakazi wa serikali wasio Waislamu wanaotaka serikali iwaondoshe eneo hilo, mwandishi wa habari wa BBC alisema.

Kundi la al-Shabab linalohusishwa na Al-Qaeda liliua watu 28 kwenye shambulio la basi siku ya Jumamosi.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anapata shinikizo kubwa kusimamisha mashambulio hayo.

Makao makuu ya Al-Shabab yako nchi jirani ya Somalia, lakini limeanzisha mashambulio Kenya tangu mwaka 2011, baada ya Kenya kupeleka majeshi mpakani kusaidia kupambana na wapiganaji.

Mwandishi wa BBC aliyopo kwenye mji mkuu, Nairobi, alisema upinzani na baadhi ya wabunge wa chama tawala wametoa wito wa idara ya usalama kubadilishwa kabisa, ikiwemo kufukuzwa kwa waziri wa mambo ya ndani Joseph Ole Lenku na mkuu wa polisi David Kimaiyo.
 

'MILIPUKO MIWILI' MJINI MAIDUGURI, NIGERIA


 Boko Haram leader Abubakar Shekau with fighters. 31 Oct 2014


Wanawake wawili wa kujitoa mhanga wamejilipua kwa mabomu katika soko lenye mkusanyiko wa watu wengi katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo vingi, walioshuhudia walisema.

Takriban watu 30 waliuawa baada ya  vijana hao wawili walipojilipua, walioshuhudia waliwaambia shirika la habari la AP.

Mmoja aliyeshuhudia Sani Adamau aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mlipuko wa pili ulitokea watu walipokuwa  wanajaribu kuwasaidia wale waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa kwanza.

Kundi la wapiganaji la Boko Haram limeshafanya mashambulio mengi Nigeria.

Kundi hilo lilianzia Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, baada ya kuundwa mwaka 2002, lakini tangu wakati huo limefurumushwa mjini humo na jeshi pamoja na makundi ya sungusungu.

Sasahivi linadhibiti maeneo makubwa ya miji na vijiji huko Borno, huku kukiwa na hofu ya kuiteka Maiduguri.

Boko Haram halijasema lolote kuhusu shambulio hili.



UPIGAJI PICHA YA HARUSI KAMA NI HIVI, BASI KIBOKO

  


Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

WAKILI MAARUFU ASIMULIA MKASA WAKE WA 'SUMU'

KAMPUNI YA UBELGIJI YA GFI YASHUTUMIWA DRC

WAKILI MAARUFU ASIMULIA MKASA WAKE WA 'SUMU'

Mbunge wa Musoma Vijijini na pia wakili maarufu Tanzania, Nimrod Mkono

Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ambaye hivi karibuni alinusurika kifo akidaiwa kulishwa sumu akiwa London, Uingereza amesimulia jinsi tukio hilo lilivyomkuta.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkono alisema endapo uchunguzi wa suala hilo utakamilika na kuthibitisha kwamba alilishwa sumu, atapambana na wahusika kwa kuwa wamehatarisha maisha yake.

Mkono ambaye pia ni wakili maarufu nchini, alitoa kauli hizo jijini hapa jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mwenendo wa afya yake.

Alidai kwamba, lengo la kumlisha sumu ni kuharibu figo zake ndani ya saa 72 wakati alipokuwa katika ziara ya nchini humo.

“Niko vizuri na afya njema… kama kuna mtu anawinda jimbo langu mwambieni ameshindwa na wananchi wangu nawaeleza kuwa niko salama wasiwe na hofu. Ninataka kujua nani kanilisha sumu na kwa nini?” alisema Mkono.

Akisimulia tukio hilo alisema, Novemba 11 akiwa miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, walisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Uingereza akiwa salama salimini.

Monday, 24 November 2014

KAMPUNI YA UBELGIJI YA GFI YASHUTUMIWA DRC

A demolished medical centre in Democratic Republic of Congo (2009)

Kampuni ya uchimbaji madini ya Ubelgiji imekuwa “ikidanganya mfululizo” kuhusu kutumia tingatinga kuvunja mamia ya nyumba huko Jamhuri ya Kidemkrosai ya Congo, shirika la kutetea hakia za binadamu la Amnesty.

Ushahidi mpya ulionyesha shirika la Groupe Forrest International (GFI) lilisambaza tingatinga kubomoa nyumba karibu na mgodi wa shaba na kobalti, ripoti hiyo ilisema.

GFI, iliyokataa kuhusika na kubomoa nyumba hizo kinyume na sheria mwaka 2009, lazima walipe fidia, shirika la Amnesty limesema.

DRC ina utajiri wa raslimali, lakini raia wao wengi wanaishi kwenye umaskini.  

Inakadiriwa kuwa ina 34% ya akiba ya madini ya kobalti na 10% ya akiba ya shaba.

Mwendesha mashtaka wa serikali alifanya uchunguzi wa ubomoaji huo na kujaribu kuwashtaki waliohusika, lakini kuzuiwa na maafisa wa serikali kufanya hivyo, kulingana na ripoti ya Amnesty.

Kampuni hiyo ya madini ilijitoa huko DRC mwaka 2012 na sasa mgodi huo unamilikiwa na serikali.