Tuesday, 9 December 2014

VIFO KUTOKANA NA MALARIA VYAPUNGUA KWA NUSU



Mosquito

Jitihada za dunia zimepunguza nusu ya watu wanaokufa na malaria – ambapo ni mafanikio makubwa, kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO.

Linasema kati ya mwaka 2001 na 2003, vifo milioni 4.3 vimezuiwa, ambapo milioni 3.9 miongoni mwao ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano eneo la kusini mwa jangwa la Sahara.

Kila mwaka, watu wengi zaidi wanapata dawa za kuwakinga na malaria, WHO limesema.

Mwaka 2004, 3% walio hatarini kupata ugonjwa huo walikuwa na uwezekano wa kupata chandarua, lakini sasa ni 50%.

Kushinda mapambano

Idadi ya watu wanaopima imeongezeka, na watu wengi zaidi wana uwezo wa kupata dawa kutibu vijidudu vya malaria, inayosambazwa na kung’atwa na mbu mwenye vidudu hivyo.

Nchi nyingi sasa zinaelekea kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.


child sleeping under a bed net

Mwaka 2013, nchi mbili - Azerbaijan na Sri Lanka – waliripoti kutokuwepo na mgonjwa hata mmoja wa maradhi hayo kwa mara ya kwanza, na nyingine 11 (Argentina, Armenia, Misri, Georgia, Iraq, Kyrgyzstan, Morocco, Oman, Paraguay, Turkmenistan na Uzbekistan) nao wamefanikiwa kutokuwa na kesi mpya.  

Barani Afrika, ambapo 90% ya vifo vyote vya malaria hutokea hapo, imepungua kwa kiwango kikubwa.

Idadi ya watu waliopata maradhi hayo barani humo imepungua kwa robo – kutoka watu milioni 173 mwaka 2000 hadi milioni 128 mwaka 2013.

Hii ni licha ya ongezeko la 43% ya idadi ya watu barani Afrika wanaoishi maeneo yaliyo rahisi kupata maradhi hayo.

Monday, 8 December 2014

RAIS KABILA AUNDA SERIKALI YA UMOJA, DRC


Joseph Kabila at the UN

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, ametangaza kuwa na serikali mpya itakayojumuisha wanachama kadhaa wa upinzani.

Mwanachama mwandamizi wa chama cha upinzani cha Movement for the Liberation of Congo ametajwa kuwa makamu wa waziri mkuu.

Wengine wengi waliokuwa wapinzani nao pia wamepewa nafasi mbalimbali.

Serikali hiyo ya umoja inaundwa huku kukiwa na hisia kuwa Bw Kabila, ambaye yupo madarakani tangu mwaka 2001, anaweza kujaribu kubadili katiba ili agombee kwa muhula wa tatu.

Wachambuzi wamesema kuwaingiza wanachama kutoka upinzani na waliokuwa wapinzani katika uongozi wake wa sasa huenda ikawa jaribio la kuimarisha ufuasi wake na kugawanya tayari upinzani ulio dhaifu.

Wanasema huenda ikawa ni kujiandaa kwa kubadili katiba au kucheleweshwa kwa uchaguzi mwaka 2016.

Evariste Boshab, kiongozi wa chama tawala cha People's Party for Reconstruction and Democracy na wakili anayezungumza kwa ushupavu kuhusu mabadiliko ya kikatiba, ametajwa naye pia kuwa makamu waziri mkuu.
 

MFANYAKAZI WA NDANI AKIRI KUMBAMIZA MTOTO, UGANDA



Woman feeds baby

Mfanyakazi wa ndani nchini Uganda ambaye video yake ilipatikana kwa siri akimbamiza na kumpiga mateke mtoto mdogo amekubali kosa la kumdhalilisha mtoto.

Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, alishtakiwa mahakamani kwa kumtesa mtoto wa kike wa miezi 18.

Video ikionyesha utesaji wa mtoto huo ulizua tafrani kubwa iliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Baba yake mtoto huyo, Eric Kamanzi, aliweka kamera baada ya kugundua mtoto wake akiwa na majeraha na anaburuza mguu.

Mwendesha mashtaka wa serikali Joyce Tushabe aliiambia mahakama kuwa mfanyakazi huyo “anajutia” na kuomba msamaha.

Video hiyo iliyochukuliwa na kamera iliyokuwa imefichwa pembezoni mwa ukumbi, inamwonyesha Tumuhirwe akimpiga mtoto huyo alipokataa kula kisha akamtupa chini kwenye sakafu, huku akimpiga na tochi kabla ya kumkanyaga na kumpiga mateke.

Baada ya kunasa ukatili huyo, baba wa mtoto huyo aliripoti tukio hilo kwa polisi Novemba 13.

Tumuhirwe, ambaye hakuwa na wakili mahakamani, sasa anakabiliwa na miaka 15 jela kwa uhalifu huo.

Wakili wa serikali ameomba kesi hiyo iahirishwe siku ya Jumatatu ili aweze kukusanya ushahidi zaidi.

Hukumu ya Tumuhirwe itatolewa Desemba 10.      

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na mwandishi wetu               

Sunday, 7 December 2014

IDRIS ASHINDA BIG BROTHER AFRIKA 2014



 

Idris Sultan mwenyeji wa Arusha, Tanzania mwenye umri wa miaka 21 anajieleza kama hodari, mcheshi, mchangamfu na mbunifu  ameibuka kidedea katika shindano la Big Brother Afrika 2014.

Anapenda miondoko mbalimbali ya muziki, na wasanii wanaomvutia zaidi ni Chris Brown, Michael Jackson, Usher, Ed Sheeran, Sam Smith, Lana Del Ray na Nina Simone.

Idris anasema hana mtu mmoja tu anayemvutia ‘role model’  badala yake huvutiwa na mtu mmoja mmoja kwa kila jambo, huku akiongeza kuwa mama yake amechangia pakubwa katika maisha yake.

Idris anaondoka na kitita cha dola za Kimarekani elfu 300.

Mwaka 2001 Mtanzania mwengine Richard Dyle Bezuidenhout alishinda shindano hilo, hivyo kumfanya Idris kuwa Mtanzania wa pili kunyakua taji hilo tangu mashindano hayo kuanza.

MARAIS MATAJIRI WA BARA LA AFRIKA 2014

   

Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani. Pia ni bara la pili lenye watu wengi sana na linachukuliwa kuwa bara maskini mno.

Kuna mataifa 47 ya Afrika yanayoongozwa na viongozi walioongoza kwa zaidi ya muongo mmoja.

Baadhi ya viongozi hawa na familia zao ni matajiri sana na mali zao zinaonekana kupatikana isivyo halali. Wanapata mali zao kutoka maliasili za mataifa hayo.

Marais na Wafalme 8 matajiri wa Afrika wa mwaka 2014. Bonyeza hapa: http://bit.ly/1BqRbn9


RAIS MUGABE NA MKEWE WOTE WATAMBA, ZIMBABWE



 

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama hicho, wakati mke wake Grace amepewa nafasi ya juu katika chama hicho.

Kupandishwa cheo kwa Grace Mugabe kuongoza jumuiya ya wanawake wa chama cha Zanu-PF inamweka katika nafasi nzuri ya kumrithi mumewe siku za usoni, wachambuzi wanasema.

Mke huyo wa Mugabe amewakosoa wapinzani wa kisiasa, akiwemo makamu wa Rais Joyce Mujuru, katika miezi ya hivi karibuni.

Bw Mugabe, mwenye umri wa miaka 90, anatarajiwa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi tena mwaka 2018.

Akizungumza katika mkutano wa Zanu-PF, Bw Mugabe aliwashukuru maelfu ya wafuasi wake kwa kumchagua kuwa kiongozi wa chama hicho.

"Najua nilipotoka... mimi sipo juu ya watu walionizaa,” Bw Mugabe aliyeiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980, alisema.

ZARI 'THE BOSS LADY' ANAVYOWIKA TANZANIA

 
Wengi tunamfahamu kama Zari The bossy lady lakini jina lake halisi ni Zarinah Hassan mwanamuziki wa Uganda ambaye ameweka makazi yake nchini Afrika Kusini.

Licha ya kuwa kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu, lakini umaarufu wake umeongezeka maradufu tangu alipoanza kuwa karibu na mwanamuziki Diamond Platinumz.

Ukaribu baina ya nyota hao umezua maswali mengi hasa baada ya kuzagaa kwa picha zao zinazowaonyesha wakiwa kwenye mapozi yenye utata.

Pamoja na kuwa wenyewe wamekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kudai kuwa kuna kazi ya sanaa wanaifanya pamoja lakini vyombo vya habari vimekuwa vikiwamulika.

Kana kwamba hiyo haitoshi, siku za hivi karibuni mrembo huyu wa Uganda ameonyesha kuzidi kuwa karibu na Diamond katika shughuli mbalimbali ikiwemo kwenye hafla ya utoaji tuzo za muziki za Channel O zilizofanyika nchini Afika Kusini.

Saturday, 6 December 2014

TOTO TUNDU - KANSIIME

    
Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

RAIS WA KENYATTA AFUTIWA MASHTAKA NA ICC