Kikombe cha kahawa asubuhi ni kinywaji ambacho wengi wetu huanza nacho.
Kama unahisi bila hiyo huwezi kuanza siku yako vizuri, basi ujue si peke yako.
Miongoni mwa wanataaluma 10,000 walioshiriki kwenye utafiti ulioafanywa na Pressat,
asilimia 85 walisema wanakunywa takriban vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.
Na takriban asilimia 70 walikiri kuwa ufanyaji wao wa kazi utaathirika bila
kupata kikombe cha kahawa.
Inaonekana kunywa kahawa ni jambo la lazima kazini kwa wataalamu wengi.
Wanaokunywa zaidi, hadi vikombe vinne kwa siku, ni wenye kazi zenye mikiki
zaidi ‘stress’: waandishi wa habari ndio wanaokunywa kahawa, wakifuatiwa na maafisa
polisi na walimu.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha South Carolina kimegundua
kuwa
mtu asizidishe milligram 200 za caffeine kwa
siku, ambazo ni sawa na vikombe vinne vya kahawa.
Kunywa kahawa kwa wingi ili tu kuweza kupambana na tafrani na uchovu wa kazi
unaweza kusababisha hatari kwa afya yako, kuanzia kupooza na wasiwasi, na hadi
kupata matatizo ya moyo, japo utafiti huo umeonyesha asilimia 62 ya wafanyakazi
hawakujua athari za kiafya zinazowakabili.
Kwa wastani utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanakunywa kahawa zaidi
kuliko wanawake lakini zaidi kidogo kwa asilimia 5.
Zifuatazo ni taaluma kumi zinazokunywa sana kahawa, kulingana na utafiti:
- Waandishi
wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari
- Maafisa
wa polisi
- Walimu
- Mafundi
bomba
- Wauguzi
na wafanyakazi wa afya
- Wakurugenzi
wa kampuni
- Wauzaji
bidhaa kwa njia ya simu
- Watoa
huduma za IT
- Wafanyakazi
wa maduka ya rejareja
- Madereva
Chanzo: pressat.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu