Monday, 19 January 2015

'WATOTO' WARUSHIWA MABOMU YA MACHOZI KENYA



Pupils protesting at Lang'ata school

Polisi wa Kenya wamerusha mabomu ya machozi kwa wanafunzi katika shule moja kubwa mjini Nairobi waliokuwa wakiandamana kupinga kuuzwa uwanja wao wa kuchezea kwa mwekezaji.

Wanafunzi hao walirejea kwenye shule yao ya Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili za mgomo wa walimu na kukuta eneo hilo la kuchezea likiwa limewekwa vizuizi.

Shule hiyo ina takriban watoto 1,000 kati ya umri wa miaka mitatu na 14 na kuendeshwa na baraza la mji wa Nairobi.

Watoto chungu nzima waliumizwa katika sekeseke hilo na polisi waliokuwa wakitawanya maandamano hayo na hivyo kupelekwa hospitali.

Baadhi waliwakabili polisi hao wa kuzuia vurugu, wakiwapungia fimbo.

Afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa alipopigwa na jiwe lililorushwa na mmoja wa waandamanaji.

BAKHSHISHI ATAKAYETOA TAARIFA YA ALBINO ALIYETOWEKA



A policeman holds up a picture of missing albino girl Pendo Emmanuelle Nundi

Polisi wa Tanzania wamesema watatoa tuzo kwa yeyote atakayetoa taarifa utakaoweza kusaidia mtoto wa kike albino ambaye hajulikani alipo anayehofiwa kutekwa kwa minajil ya  kupata viungo vyake vya mwili.

Pendo Emmanuelle Nundi, mwenye umri wa miaka 4, alitekwa mwezi uliopita. Baba wa binti huyo ni miongoni mwa watu 15 waliokamatwa kutokana na kutekwa huko.

Viungo vya mwili wa albino, husakwa na waganga wa kienyeji.

Tanzania imewapiga marufuku waganga wa kienyeji wanaopiga ramli katika jitihada za kuzuia mashambulio dhidi ya albino.

Polisi wameahidi kutoa shilingi milioni tatu za Kitanzania sawa na $1,700 kujaribu kumtafuta binti huyo ambaye hajulikani alipo “mfu au hai”.

Wajomba zake wawili binti huyo nao pia wamekamatwa kama sehemu ya uchunguzi.

                                                          

150 WAPEWA MIMBA NA WANAFUNZI WENZAO CHUONI



Wanafunzi 150 kati ya 1,000 waliojiunga na masomo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) mwaka jana wamebainika kuwa na ujauzito waliopewa na wenzao chuoni hapo.

Utafiti wa usawa na jinsia uliofanywa na chuo hicho kati ya Juni na Novemba mwaka jana umebaini kuwa wanafunzi wanaopata ujauzito ni wale wa mwaka wa kwanza.

Hayo yamebainishwa jana na Mratibu wa Masuala ya Jinsia wa chuo hicho, Dk Dativa Shilla katika warsha ya uchaguzi na uhusiano wa kijinsia iliyofanyika chuoni hapo.

Alisema hali hiyo inatokana na kuwapo kwa vitendo vya ukatili, manyanyaso na ubabe unaofanywa na wanachuo wa kiume dhidi ya wale wa kike na hivyo kuwalazimisha kufanya mapenzi bila hiyari yao.

“Kupitia utafiti huu tumeona hakuna usawa wa kijinsia wa kupata elimu baina ya mwanamke na mwanamume kwa sababu mwenye ujauzito hawezi kufanya vizuri katika masomo yake ukilinganisha na mhusika wa kiume,” alisema.

ASAMOAH GYAN KUCHEZA DHIDI YA SENEGAL?



 Asamoah Gyan

Kapteni wa Ghana Asamoah Gyan anaugua “malaria” na huenda asiweze kucheza dhidi ya Senegal siku ya Jumatatu.

Shirikisho la Mpira la Ghana lilisema mshambuliaji huyo alilazwa hospitalini huko Mongomo siku ya Jumamosi jioni na kutolewa Jumapili asubuhi.

Ugonjwa huo “uligunduliwa mapema” na Gyan anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Kiongozi wa timu ya Senegal Alain Giresse lazima aamue kuhusu afya ya Sadio Mane, ambaye amekuwa hachezi baada ya kujeruhiwa mguu.

Mchezaji huyo wa Southampton alijumuishwa kwenye timu hiyo licha ya klabu yake kusisitiza kuwa hatokuwa na afya nzuri ya kucheza.

Chanzo: BBC                                                

Sunday, 18 January 2015

KISWAHILI NI CHA WASIOJUA KIINGEREZA?



Katika nchi nyingi za Afrika, jamii imejigawa katika jamii ndogondogo ziitwazo makabila.

Kila kabila linakuwa na lugha inayotambulisha jamii ile. Kwa kuwa katika nchi makabila ni mengi na yanaongea lugha tofauti ambazo mara nyingi hata hazisikilizani, nchi huamua kuweka lugha moja rasmi kuwa lugha ya taifa.

Wenzetu katika nchi nyingine waliamua kuchukua lugha ya wale waliowatawala kuwa ndio lugha ya taifa. Hivyo kama walitawaliwa na Waingereza lugha ya taifa inakuwa Kiingereza, kama walitawaliwa na Wafaransa basi lugha ya taifa inakuwa Kifaransa. Tanzania ni nchi moja katika nchi chache sana katika Afrika ambazo zinatumia lugha ambazo siyo lugha za walio watawala. Sisi Tanzania tunatumia Kiswahili kama lugha ya taifa.

Mimi najivunia sana lugha hii, ninatamba mbele za walimwengu kwamba sisi tuna lugha ya Kiswahili inayotuunganisha kama taifa. Pamoja na kwamba sasa Kiswahili kimeenea sehemu nyingine za dunia hii hasa zile za Afrika Mashariki bado mimi naona hiyo ni lugha yetu sisi na wengine wamejifunza kama sisi tunavyojifunza lugha za watu wengine.

Ninaamini wapo wenye fikira kama hizi za kwangu lakini ninahisi pia wapo wanaoona lugha hii haiwahusu. Wengi wa hao ni watu wanaojua Kiingereza ambao wanaona Kiingereza ndiyo utambulisho wa usomi.

Hivyo hata kama Kiswahili kinadidimia hilo sio tatizo kwao kwani hiyo siyo lugha ya watu wenye hadhi; hata kama matumizi ya lugha hiyo ya Kiswahili siyo sahihi, hilo halijalishi kwani inakosewa lugha isiyo ya lazima kwao.

THAILAND KUITAMBUA JINSIA YA TATU?



 There's a perception that transgender people are well accepted in Thailand, due to the availability of gender reassignment surgery, as seen here in Bangkok. But challenges persist, says advocates.

Thailand, hivi karibuni inaweza kuanza kutambua jisnia ya tatu kwa mara ya kwanza kwenye katiba ya nchi hiyo.

"Ni haki ya binadamu kama ulizaliwa mwanamme au mwanamke na unataka kubadili jinsia yako au kuwa na maisha ya jinsia nyingine." Alisema Kamnoon Sittisamarn, msemaji wa kamati ya rasimu ya katiba, inayofanyia kazi rasimu mpya nchini humo.

"Watu wanatakiwa kuwa na uhuru wa kubadili jinsia na wanatakiwa kupata ulinzi sawa kutoka kwenye katiba na sheria na kupewa haki sawa."

Jinsia ya tatu inamaanisha kuwa mtu hatotakiwa kujitambulisha kama mwanamme au mwanamke, na kumpa haki ya kujitambulisha kivyake.

Iwapo itapitishwa , Thailand itajiunga na nchi kadhaa za bara la Asia, zikiwemo India, Pakistan na Nepal, ambazo hivi karibuni zimekubali kutambua jinsia ya tatu.


Chanzo: edition.cnn.com
 

 

Friday, 16 January 2015

MAFURIKO YAUA TAKRIBAN 170 MALAWI


Malawians displaced by floods

Serikali ya Malawi imesema takriban watu 170 wamefariki dunia kutokana na mafuriko – ongezeko kubwa sana.

Mvua kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita umevurumusha nyumba tele na kusababisha wakazi wengi kuhamia uwanda wa juu, wengine wakivuka mpaka hadi Msumbiji.

Makamu wa rais Saulos Chilima alisema zaidi ya watu 100,000 walihama makazi yao, hasa kusini.
Mapema wiki hii, serikali ilitangaza kuwa theluthi ya nchi hiyo ni eneo la majanga na kuomba msaada.

Mamlaka za Malawi zimekuwa zikitumia helikopta za kijeshi na boti kuwafikia baadhi ya watu waliokwama.

Lakini Bw Chilima alisema shughuli za uokoaji zinakwama kutokana na hali mbaya ya hewa katika siku chache zilizopita na ugumu wa kupata sehemu ya kutua kwa helikopta hizo.