Tuesday, 10 February 2015
KANYE WEST ASEMA GRAMMYS 'HAZIHESHIMU SANAA'
Kanye West ameshutumu tuzo za Grammys kwa "kutoheshimu sanaa" baada ya kumpa ushindi Beck wa albamu bora ya mwaka badala ya Beyonce.
Alikuwa almanusra kuvamia jukwaa wakati Beck alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukran.
Ilionekana kama West alikuwa arudie tukio alilofanya dhidi ya Taylor Swift, alipovamia jukwaa mwaka 2009.
Hatahivyo, alipohojiwa kwenye kipindi cha E, baadae alisema aliamua kutabasamu na kukaa chini baada ya kumfikiria binti yake.
Msanii huyo wa miondoko ya hiphop alisema anaona Beck “angetakiwa kumpa Beyonce tuzo yake”.
"Ninachojua ni kuwa hizi tuzo za Grammys, kama wanataka wasanii wa kweli wawe wanarejea, wanatakiwa kuacha kutuchezea akili. Hatutoendelea kuzinguliwa nao." Alikiambia kipindi cha E, alipohojiwa akiwa na mkewe Kim Kardashian.
MBUNGE AUAWA NA AL-SHABAB SOMALIA
Mbunge mmoja wa Somalia amepigwa risasi na kufa mjini Mogadishu na wapiganaji wa al-Shabab, maafisa walisema.
Abdullahi Qayad Barre aliuawa karibu na kasri ya rais baada wa watu wenye silaha kumfyatulia risasi kwenye gari lake.
Msemaji wa al-Shabab alisema kundi hilo limehusika na shambulio hilo, na litalenga wabunge wengine.
Kifo cha Barre kimetokea huku kukiwa na ulinzi mkali wakati wabunge walipokusanyika kupiga kura ya kuidhinisha baraza jipya la mawaziri au la.
Ni mfululizo wa mauaji dhidi ya wanasiasa nchini humo.
Takriban wabunge watano waliuawa mwaka jana, lakini Barre ni wa kwanza kuuawa mwaka huu 2015.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na mwandishi wetu
Monday, 9 February 2015
MAMBO 5 YANAYOKWAMISHA BIASHARA
Wafanyabiashara wengi hukumbwa na changamoto nyingi katika uendeshaji wa shughuli zao za biashara. Changamoto hizi ndizo zinaweza pia kuwa utofauti wa biashara zinazokua na zile zinazokufa.
Makala hii inachambua mambo muhimu ambayo huwa ni mzigo mzito kwa wajasiriamali hata kufikia hatua ya kuathiri biashara zao, na pia makala hii inaonyesha baadhi ya njia za kukabiliana na changamoto hizo.
1. Mtaji
Kikwazo hiki hujitokeza katika mitazamo mitatu, kwanza wakati wa kutaka kuanzisha biashara, pili wakati biashara imeshaanza ila fedha hazitoshi kuendesha vema, na tatu pale mfanyabiashara anapokusudia kupanua biashara yake. Ili kukabiliana na kikwazo cha mtaji yafuatayo yanaweza kusaidia:-
Kuanza biashara kidogo kidogo: Hii namaanisha kuwa kufikiria namna ambazo unaweza kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo na wakati huo huo ukafanya kwa ufanisi. Hii inaweza kwa kuchunguza kwa umakini gharama zisizo za lazima, mambo ambayo unaweza fanya wewe mwenyewe au kusaidia na watu wengine bila kuajiri, pia chunguza aina ya bidhaa ambazo kweli ni za lazima kuanza nazo. Kutunza taarifa za biashara yako kwa ufasaha na kuwa na muundo bora wa uongozi, hii itakusaidia kuwa kutimiza masharti ya benki, na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha ambao wanaweza kukuongezea mtaji.
Zingatia pia kuwa na mali zisizohamishika, na pia kuna na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali kwani wao wanaweza kuwa vyanzo vya kukupatia mtaji.
2. Muundo wa biashara
IVORY COAST YASHINDA KOMBE LA AFRIKA 2015
Ivory Coast wameshinda taji la Kombe la Afrika mwaka 2015 kwa mikwaju 9 ya penati Ghana 8 |
Timu ya soka ya Ivory Coast imenyakuwa taji la Kombe la Afrika la mwaka 2015 kwa kuitandika timu ya Ghana kwa mikwaju ya penati.
Ivory Coast imeshinda kwa mikwaju 9 ya penati huku Ghana ikipata mikwaju 8.
Boubacar Barry, 35, ndiye aliyeibuka kidedea kwa kufunga penati ya mwisho baada ya mlinda mlango wa Ghana Razak Braimah kukosa penati.
Ghana walipata penati nane huku Ivory Coast wakishinda kwa penati tisa |
Mlinda mlango mkongwe wa Ivory Boubacar Barry ndiye nyota wa mchezo wa leo.
Mashindano hayo yalikuwa yanafanyika nchini Equatorial Guinea.
Chanzo: taarifa.co.tz
Sunday, 8 February 2015
MASHABIKI WA MPIRA WAZUA GHASIA, 14 WAFARIKI
Takriban watu 14 wamefariki dunia katika mapambano yaliyozuka baina ya mashabiki wa mpira na polisi nje ya uwanja wa mpira mjini Cairo, chombo cha habari cha taifa cha Misri kimeripoti.
Mashabiki wa klabu ya mpira ya Zamalek walijaribu kuingia uwanjani kutazama mechi bila tiketi, na kuchochea ghasia hizo, maafisa walisema.
Vurugu hizo zilianza kabla ya mechi baina ya pande za Zamalek na ENPPI.
Februari 2012, zaidi ya watu 70 walikufa katika ghasia zilizozuka baada ya mechi huko Port Said.
DEREVA ALIYEFUKUZWA AKUSUDIA KUUA 50
Polisi nchini Uganda walisema walimkamata dereva aliyejaribu kuligonga basi kwenye mto ulojaa mamba kwa nia ya kuua abiria 50 waliokuwa kwenye chombo hicho baada ya kufukuzwa kazi.
“Tulipojua kuhusu utekajinyara huo, tuliweka vizuizi kabla ya mto huo ..tulimvamia halafu tukamkamata.” Alisema Denis Namuwooza, mkuu wa polisi katika wilaya ya Kasese kusini-magharibi mwa Uganda.
Dereva huyo, ambaye polisi walisema alifukuzwa kutokana na ulevi, iliripotiwa alikusudia kulirusha basi hilo huko Kazinga, mto ambao aghlabu hujaa viboko, ambao huunganisha maziwa mawili makubwa katika mbuga ya wanyama ya Queen Elizabeth nchini Uganda.
Aliwaambia abiria "atakufa pamoja na wao kwa kulirusha basi Kazinga, “ alisema mmoja aliyenusurika, Dinah Mwagale Mudusu, akizungumza na chombo cha habari cha Uganda.
Chanzo: AFP
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
UCHAGUZI WA MWEZI HUU NIGERIA WAAHIRISHWA
Mapema Jumamosi, waandamanaji wengi wametoa wito wa uchaguzi kuendelea kama ilivyopangwa |
Upinzani wa Nigeria umesema hatua ya kuahirisha uchaguzi wa rais wa Februari 14 kwa wiki sita “una athari kubwa kwa demokrasia”.
Tume ya uchaguzi imesema imesogeza tarehe ya upigaji kura kwasababu majeshi yaliyotakiwa kufanya ulinzi kwenye vituo vya kupigia kura yamesambazwa kupambana na Boko Haram
Kuahirishwa kwa uchaguzi huo kumeifurahisha chama tawala, lakini Marekani imesema “imesikitishwa”
Nigeria imekuwa ikipambana na wapiganaji wa Boko Haram kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Maelfu ya watu wamekufa kutokana na mapigano ya wapiganaji hao katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Boko Haram pia imeanza kushambulia majirani wa Nigeria: siku ya Jumapili, kwa mara ya pili katika siku tatu, wapiganaji hao wameshambulia mji wa Diffa mpakani mwa Niger.
Takriban mtu mmoja alifariki dunia kwenye mlipuko katika soko la mji huo, huku baadhi ya walioshuhudia wakisema mtu aliyejitoa mhanga ndiye kahusika.
Subscribe to:
Posts (Atom)