Hisibati na Sayansi ni masomo
yasiowavutia sana watoto, lakini Tanzania mtazamo huo unabadilika. Ubongo kids
ni vibonzo vya elimu burudani,ya kwanza kwa Tanzania, inayofundisha watoto
hisabati na sayansi kwa njia ya wanyama wanaoimba. Kipindi kinatazamwa na zaidi
ya watoto milioni moja. Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasimulia.
Wednesday, 11 February 2015
WASHINDI IVORY COAST WAMWAGIWA FEDHA
Timu ya mpira ya Ivory Coast imezawadiwa
mamilioni ya dola na serikali ya nchi hiyo kwa kushinda Kombe la Mataifa ya
Afrika.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anampa kila mchezaji ambao jumla wako 23, nyumba yenye thamani ya dola 52,000 kila moja na pia pesa taslimu ya kiwango hicho hicho kwa kila mmoja, serikali hiyo ilisema.
Timu hiyo imeishinda Black Stars ya Ghana 9-8 kwa mikwaju wa penalti kwenye fainali ya shindano hilo Equatorial Guinea.
Shirikisho la Soka la nchi hiyo pia limepewa mamilioni ya fedha na wafanyakazi wengine wa timu hiyo.
Kwa jumla serikali hiyo imetoa zaidi ya dola milioni 3 kwa kusherehekea ushindi huo.
Timu ya Ghana nao hawakuachwa nyuma, licha ya kushindwa.
Kila mchezaji amepewa dola 25,000 na mfadhili wa timu hiyo, ambao ni shirika la mafuta la taifa Ghana (GNPC), kiwango ambacho waziri wa michezo wa Ghana ameona ni kidogo.
MAKERERE KUCHUNGUZA 'SHAHADA BANDIA'
Moja ya vyuo vikuu bora Uganda imeanza
uchunguzi wa madai kuwa wanafunzi wamekuwa wakituzwa shahada bandia.
Miongoni mwa wahitimu 12,000 kutoka chuo kikuu cha Makerere, takriban 600 hawakufikia viwango vinavyotakiwa, maafisa walisema.
Wanafunzi wote hao 600 wanaochunguzwa walikuwa wamehitimu masomo ya sayansi za jamii.
Makamu wa mkuu wa chuo Ernest Okello Ogwang aliiambia BBC kuwa alishuku matokeo ya mtihani yalibadilishwa kusudi.
William Tayeebwa, mkuu wa idara ya uandishi wa habari wa Makerere, aliiambia BBC kuwa mwanafunzi mmoja alifeli mtihani kwa 44%, mara matokeo yakabadilika na kuwa 71%.
Lakini wanafunzi saba kutoka idara ya uandishi wa habari ambao walikuwa na sifa zote na kuidhinishwa kuweza kuhitimu walikuja kugundua majina yao hayakuwepo katika orodha.
Bw Ogwang alikiri kuwa "huenda kuna udanganyifu". Alisema mashaka hayo ya udanganyifu unadhihirisha “udhaifu” katika mfumo wa chuo hicho ambapo “inabidi kuangaliwa kwa makini”.
WANAWAKE VINARA USAFIRI WA BODABODA
Zinaitwa bodaboda, kule Nigeria wanaziita okadas kwa jina jingine ni pikipiki. Hiki ni chombo cha usafiri ambacho katika miaka ya hivi karibuni kimeiteka miji mingi ya Afrika ikiwamo Tanzania.
Licha ya kutumika katika uhalifu, kusababisha vifo kwa kiasi kikubwa, utafiti uliofanywa na gazeti hili katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambako kuna matumizi makubwa ya bodaboda ulibaini kuwa usafiri huu unapendwa zaidi na wanawake.
Dereva wa bodaboda katika maeneo ya Tabata Relini, Ayubu Msigala anasema idadi kubwa ya abiria wake ni wanawake. Anasema wanawake wajawazito pia wanatumia usafiri huo kwa kiasi kikubwa.
“Zamani wanawake walikuwa wanaogopa bodaboda, lakini sasa hata wajawazito wanatumia zaidi, hawaogopi kama ilivyokuwa zamani,” anasema Msigalla.
Akizungumzia suala la wanawake kupenda bodaboda, Msigala anasema wanawake waliokuwa wakiziogopa bodaboda sasa ndiyo wanaozipanda kwa wingi huku wanawake wajasiriamali wakiongoza kuzitumia.
Anasema mamalishe, wauza nguo, vocha, hata wafanyakazi wa maofisini wamekuwa wapandaji wakubwa wa bodaboda.
Tuesday, 10 February 2015
BOBBI KRISTINA 'KUFA' SIKU MOJA NA WHITNEY

Familia ya Bobbi Kristina Brown watachomoa mashine yake ya kupumulia siku ya Jumatano ili Brown aweze kufa siku ileile aliyokufa mama yake Whitney Houston, gazeti la New York Post limeripoti.
Bibi yake Brown na mama yake Whitney, Cissy Houston, alipendekeza wazo hilo mwishoni mwa juma, kulingana na the Post.
Familia inapanga kuchomoa mashine ya Brown ya kupumulia usiku wa Jumanne kuingia Jumatano.
Brown, mwenye umri wa miaka 21, amepooza tangu alipokutwa kwenye bafu nyumbani kwake huko Georgia, Januari 31.
Polisi wanafanya uchunguzi, wakimfutailia zaidi mpenzi wake Nick Gordon, aliyemkuta kwenye bafu hilo.
Inaripotiwa Brown alikuwa na majeraha usoni alipokutwa.
Whitney Houston alifariki dunia Februari 11, 2012, baada ya kuzama kwenye bafu lililojaa maji na baadae mwili wake ukikutwa na dawa za kulevya.
Familia yake na marafiki, akiwemo baba yake Bobbi Kristina, Bobby Brown, wameandaa sala ikiambatana na mishumaa siku ya Jumatatu huko Riverdale.
WALIOBADILISHIWA WAZAZI UTOTONI WALIPWA

Wanawake wawili waliobadilishiwa watoto miaka 20 iliyopita wote wawili watapewa euro 400,000 euros ($451,760) kutokana na kosa hilo, kulingana na uamuzi wa mahakama moja kusini mwa Ufaransa.
Mahakama hiyo mjini Grasse nayo pia ilitoa amri kuwa zahanati hiyo binafsi iliyohusika na kuwachanganya watoto hao kulipa euro 300,000 kwa kila mmoja kwa wazazi watatu waliohusika, pamoja na euro 60,000 kwa kila kaka na dada walioathirika.
Mmoja miongoni mwa mama hao wawili aligundua kuwa mtoto wake si halisi baada ya kupima asidi nasaba mwaka 2004, miaka 10 baada ya binti huyo kuzaliwa.
Mabinti wote wawili walikuwa wakiumwa homa ya manjano walipozaliwa na kuwekwa kwewnye chombo kimoja cha kuhifadhi mtoto mjini Cannes.
Muuguzi aliwabidilisha watoto hao wakati wa kuwakabidhi mama zao. Wanawake hao walielezea wasiwasi wa kupewa watoto wasio wao wakati huo, lakini waliambiwa hakuna kosa lolote.
Chanzo: Reuters
Imetafsiriwa na mwandishi wetu
KANYE WEST ASEMA GRAMMYS 'HAZIHESHIMU SANAA'
Kanye West ameshutumu tuzo za Grammys kwa "kutoheshimu sanaa" baada ya kumpa ushindi Beck wa albamu bora ya mwaka badala ya Beyonce.
Alikuwa almanusra kuvamia jukwaa wakati Beck alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukran.
Ilionekana kama West alikuwa arudie tukio alilofanya dhidi ya Taylor Swift, alipovamia jukwaa mwaka 2009.
Hatahivyo, alipohojiwa kwenye kipindi cha E, baadae alisema aliamua kutabasamu na kukaa chini baada ya kumfikiria binti yake.
Msanii huyo wa miondoko ya hiphop alisema anaona Beck “angetakiwa kumpa Beyonce tuzo yake”.
"Ninachojua ni kuwa hizi tuzo za Grammys, kama wanataka wasanii wa kweli wawe wanarejea, wanatakiwa kuacha kutuchezea akili. Hatutoendelea kuzinguliwa nao." Alikiambia kipindi cha E, alipohojiwa akiwa na mkewe Kim Kardashian.
Subscribe to:
Comments (Atom)