Monday, 30 March 2015

UCHAGUZI NIGERIA: MATOKEO YA AWALI YATARAJIWA



An official of the Independent National Electoral Commission retrieves on March 29, 2015 documents from ballot boxes from the presidential election

Tume ya kusimamia uchaguzi Nigeria imesema inatarajia kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais siku ya Jumanne baada ya raia wa nchi hiyo kupiga kura Jumamosi.

Rais aliye madarakani Goodluck Jonathan anakabiliwa na changamoto nzito kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Muhammadu Buhari.

Umoja wa mataifa umeusifia upigaji kura huo licha ya kuwepo hitilafu za kiufundi, maandamano na ghasia yanayohusishwa na Boko Haram

Upigaji kura uliendelea mpaka siku ya pili katika baadhi ya sehemu nchini Nigeria baada ya kuwepo matatizo ya mfumo mpya wa kutumia kadi za kielektroniki.

 

Sunday, 29 March 2015

KINYESI KUPITA KIASI MLIMA EVEREST



 Mount Everest

Kinyeshi kupita kiasi na mikojo huachwa ikijazana na wapanda mlima kwenye mlima Everest.

Jambo hilo linasababisha uchafuzi wa mazingira na huenda ukaeneza maradhi, alisema mkuu wa jumuiya ya wapanda mlima wa Nepal.

Ang Tshering anataka serikali ya Nepal kuwaambia wageni wote kuhifadhi uchafu huo  inavyostahili.

Alisema kinyesi na mikojo imekuwa “ikijazana” kwa miaka kadhaa maeneo ya kambi nne zilizopo.

“Wapandaji milima huchimba shimo kwenye theluji kama vile choo na kuacha uchafu huo hapo.”

Zaidi ya wapanda mlima 700 na wanaowaongoza hukaa takriban miezi miwili mlimani humo kila msimu, ambapo huanza mwanzoni mwa mwezi Machi na kumalizika mwezi Mei.

Baadhi ya wapanda milima hubeba mifuko maalum ya kuhifadhi uchafu huo kwenye kambi za juu zaidi, alisema.

Kwenye kambi za chini kuna maturubali maalum ndio kama vyoo, ambapo ina njia maalum ya kupitisha uchafu huo.

Serikali ya Nepal bado inatafuta suluhu ya tatizo hilo.

Sheria mpya zinamaanisha kuwa kila mpanda mlima lazima arudi na kilo 8 za uchafu wanaporudi chini.

Hicho ni kiwango ambacho wataalamu wanaamini mpanda mlima hutoa akiwa safarini.

Watu hao pia hulipa dola 4000, ambazo hawarudishiwi  kama watashindwa kutimiza masharti hayo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

Friday, 27 March 2015

FILAMU KUHUSU ALBINO YAZINDULIWA LONDON

   
 Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la mauaji ya albino, hasa katika mataifa ya Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania na vile vile Burundi. Watu hao hulengwa kutokana na itikadi za kichawi kwa madai kuwa viungo vyao huleta utajiri, bahati na kuponyesha maradhi yoyote. Filamu moja inayoangazia mauaji ya albino Tanzania 'White Shadow' imezinduliwa London wiki hii, Zuhura Yunus wa BBC alihudhuria uzinduzi huo.

HIV: DHARURA YA KIAFYA KUTANGAZWA INDIANA



Computer artwork of the HIV virus

Gavana wa Indiana ametangaza dharura ya afya ya umma baada ya mlipuko wa HIV “kufikia kiwango cha kusambaa” sehemu ya jimbo hilo.

Kaunti ya Scott, eneo la kimaskini ambapo watumiaji wa dawa za kulevya kutumia sindano moja kwa pamoja si jambo la ajabu, ambapo katika wiki za hivi karibuni maambukizi mapya 79 yameongezeka kutoka wastani wa watu watano.

 Gavana Mike Pence ameidhinisha maafisa wa afya kutekeleza mradi wa kutoa elimu juu ya kubadilishana sindano – jambo alilowahi kukataa siku za nyuma.

HIV ni kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Aids.

Mlipuko huo mwanzo ulitambuliwa mwezi Januari mwishoni. Tangu wakati huo, maafisa wamegundua watu 79 wakiwa na ugonjwa huo – kutoka watu 26 tu mwezi uliopita.

Thursday, 26 March 2015

MAREKANI YAONYA KUWEPO SHAMBULIO KAMPALA



A crowded street in Kampala. File photo
Marekani yaonya kuwepo shambulio Kampala

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeonya kuwa raia kutoka nchi za kimagharibi – wakiwemo Wamarekani – huenda wakawa wamelengwa kwa mashambulio ya ugaidi katika mji mkuu Kampala.

Ulisema “umepata taarifa za uwezekano wa kuwepo vitisho” kwenye maeneo ya mijini ambapo aghlabu raia wa kigeni hujikusanya.

Shambulio “huenda likatokea hivi karibuni” ilisema, huku ikisema mikutano mengine iliyokuwa imepangwa kufanyika katika hoteli za Kampala imeahirishwa.

Ubalozi huo haujatoa taarifa zaidi. Uganda imeshawahi kushambuliwa siku za nyuma na wapiganji wa Kisomali wa al-Shabab.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

Wednesday, 25 March 2015

ALIYEKUWA RAIS WA LIBERIA KUFUNGWA UINGEREZA



 Charles Taylor in court (file photo)

Imetolewa amri kuwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles atatumikia kipindi chake chote cha gerezani Uingereza, baada ya kukataliwa kuhamishiwa Rwanda.

Alisema ananyimwa haki yake ya maisha na familia yake, kwasababu mke wake na watoto wake wamenyimwa viza ya Uingereza.

Majaji walikana kauli yake hiyo, wakisema hawakuomba viza hiyo inavyotakiwa.

Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilimtia hatiani juu ya uhalifu wa kivita kwa kuwaunga mkono waasi waliofanya ukatili Sierra Leone.


JEREMY CLARKSON ATOLEWA TOP GEAR YA BBC



Jeremy Clarkson

Mkataba wa Jeremy Clarkson hautoongezwa baada ya kufanya "shambulio lisilokuwa na uchochezi wowote” kwa msimamizi wa kipindi cha Top Gear, mkurugenzi mkuu wa BBC amethibitisha.

Tony Hall alisema “hakuchukua uamuzi huo kwa uwepesi” na alitambua “itagawanya maoni ya wengi”.

Hata hivyo, aliongeza “alivuka mpaka” na " hawezi kukubaliana na kilichofanyika katika tukio hilo".

Clarkson alisimamishwa kazi Machi 10, kwa kile kilichoitwa “ugomvi” na msimamizi wa Top Gear Oisin Tymon.

Ugomvi huo, uliotokea kwenye hoteli moja huko Yorkshire, inasemwa kuwa ilitokea kwasababu hapakuwepo na chakula cha moto baada ya kufanya kazi siku nzima.