Kinyeshi kupita kiasi na mikojo huachwa
ikijazana na wapanda mlima kwenye mlima Everest.
Jambo hilo linasababisha uchafuzi wa mazingira na
huenda ukaeneza maradhi, alisema mkuu wa jumuiya ya wapanda mlima wa Nepal.
Ang Tshering anataka serikali ya Nepal kuwaambia wageni wote kuhifadhi uchafu
huo
inavyostahili.
Alisema kinyesi na mikojo imekuwa “ikijazana” kwa miaka kadhaa maeneo ya
kambi nne zilizopo.
“Wapandaji milima huchimba shimo kwenye theluji kama vile choo na kuacha uchafu
huo hapo.”
Zaidi ya wapanda mlima 700 na wanaowaongoza hukaa takriban miezi miwili
mlimani humo kila msimu, ambapo huanza mwanzoni mwa mwezi Machi na kumalizika
mwezi Mei.
Baadhi ya wapanda milima hubeba mifuko maalum ya kuhifadhi uchafu huo kwenye
kambi za juu zaidi, alisema.
Kwenye kambi za chini kuna maturubali maalum ndio kama vyoo, ambapo ina njia
maalum ya kupitisha uchafu huo.
Serikali ya Nepal bado inatafuta suluhu ya tatizo hilo.
Sheria mpya zinamaanisha kuwa kila mpanda mlima lazima arudi na kilo 8 za
uchafu wanaporudi chini.
Hicho ni kiwango ambacho wataalamu wanaamini mpanda mlima hutoa akiwa
safarini.
Watu hao pia hulipa dola 4000, ambazo hawarudishiwi
kama watashindwa kutimiza masharti hayo.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu