Sunday, 4 January 2015

INDIA KUCHUNGUZA UTUMIAJI WA CHOO




Serikali ya India imetangaza kuwepo na mpango wa kitaifa wa kuangalia iwapo watu wanatumia vyoo.

Ni sehemu ya mpango wa taifa kufanya nchi hiyo iwe safi, uliozinduliwa na waziri mkuu mpya, Narendra Modi, miezi mitatu iliyopita.   

Wakaguzi wa usafi watafanya uchunguzi nyumba hadi nyumba wa namna watu wanavyotumia vyoo, na wakihifadhi matokeo kwenye simu za mkononi na vifaa vengine vya kiteknolojia.

Taarifa ya serikali ilisema hatua hiyo inaadhimisha utafiti wa awali ambao ulisimamia ujenzi wa vyoo.

Serikali hiyo ilisema imejenga vyoo nusu milioni tangu mwezi Oktoba.

Hatahivyo, Umoja wa Mataifa unaamini takriban nusu ya watu nchini India hawako radhi kutumia vyoo vya ndani, matokeo yake ni kuibuka kwa maradhi tele yanayohusu uchafu na vifo vya mapema.

Chanzo: Reuters na AFP


AINA NYINGI ZA SARATANI NI 'BAHATI MBAYA'


 Lung cancer cells

Aina nyingi za saratani zinaweza kusemwa kuwa ni bahati mbaya badala ya kutokana na hatari kama vile uvutaji sigara, utafiti umeonyesha.

Wataalamu Marekani walikuwa wakijaribu kueleza kwanini baadhi ya mkusanyiko wa seli mwilini zilikuwa rahisi kupata saratani kuliko nyingine.

Matokeo hayo, kwenye jarida la Sayansi, zimeonyesha theluthi mbili ya aina ya saratani zilizofanyiwa utafiti zilisababishwa kwa bahati mbaya tu na si mtindo wa maisha.

Hata hivyo, baadhi ya aina za saratani zinazojulikana sana na zinazoua zinatokana na mtindo wa maisha.

Kwahiyo, je ni muda wa kushusha pumzi, kunywa na kula chochote bila kuwa na wasiwasi?

Haitoshangaza likiwa jibu ni Hapana.

Utafiti unaonyesha theluthi mbili ya aina ya saratani ni kwa bahati mbaya.

Lakini theluthi inayobaki kwa kiasi kikubwa kinatokana na mitindo yetu ya maisha.

Kunywa pombe kupindukia, muda mwingi juani au unene sana zote zinaweza kusababisha saratani.

Ikumbukwe 20% ya sababu za kupata saratani duniani ni kwa uvutaji sigara.

Utafiti huu ni ukumbusho kuwa saratani aghlabu ni bahati mbaya na njia pekee kuikwepa ni kuitambua mapema

MFALME ABDULLAH WA SAUDI ARABIA AUGUA


In this Friday, June 27, 2014 file photo, Saudi King Abdullah speaks before a meeting with U.S. Secretary of State John Kerry at his private residence in the Red Sea city of in Jeddah, Saudi Arabia

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amepata maradhi ya mapafu 'Pneumonia'na amekuwa akipumua kwa kutumia mrija, maafisa wa nchi hiyo walisema.

Mfalme huyo, anayeaminiwa kuwa na umri wa miaka 90, alilazwa hospitalini siku ya Jumatano kwa  uangalizi.

Mfalme Abdullah, aliyeshika nafasi hiyo kuanzia mwaka 2005, amekuwa akiumwa mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Umri wake na afya yake umefanya wengi kujiuliza kuhusu urithi wa ufalme nchini humo.

Crown Prince Salman, mwenye umri wa miaka ya 70, ndiye anayefuata kwenye urithi wa ufalme, japo bado kuna maswali kuwa nani atachukua nafasi hiyo.

Ufalme huo umepita kwa watoto wa kiume wa muasisi na baba wa taifa wa Saudi Arabia Ibn Saud, lakini wachache sana bado wako hai.

Mwaka jana, Mfalme Abdullah alichukua hatua ya kuteua naibu, ambaye ni mdogo wake wa baba mmoja Prince Muqrin, kwa nia ya kujaribu kuweka hali ya kuwepo hali tulivu ya kurithishana.

Chanzo: AFP
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


MSANII WA HIP HOP PROF J KUWANIA UBUNGE MIKUMI

 

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, anatarajia kugombea Ubunge jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro mwaka huu.

Akizungumza na Tanzania Daima, rafiki yake wa karibu na Profesa Jay, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, alisema kwa sasa yupo Mikumi kwa ajili ya kumsaidia Profesa Jay katika maandalizi ya uchaguzi mkuu hapo mwakani.

“Nipo na Profesa tunawapigia kampeni wenyeviti wa mitaa na vitongoji katika uchaguzi unaoendelea, kwasababu tukiamini kwamba serikali na msingi mzuri wa uongozi inabidi uanzie chini.

Ina maana nyumba ambayo itakuwa na msingi mzuri ni nyumba bora zaidi. “Kwahiyo tupo hapa Mikumi tukijaaliwa uzima Profesa Jay mwakani ametangaza nia ya kugombea ubunge hapa nyumbani kwao.

Tumeanza kujenga mazingira kwenye uongozi wa chini ili mwakani Profesa akute kuna misingi imara na apate ubunge wa hapa Mikumi, kwahiyo yeye atagombea Mikumi na mimi nitagombea Morogoro mjini kwetu,” alisema.

Aliongeza kuwa, Mikumi ndipo kwao kabisa na Profesa Jay ambaye anatarajia kugombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), na wameamua kuingia kwenye siasa kwasababu wameshafanya sana nyimbo za kiharakati, wameshaongea mengi kupitia muziki wao lakini bahati mbaya viongozi wamekuwa na masikio magumu.

MSHUKIWA WA SHAMBULIO LA TZ NA KENYA AFARIKI



Anas Al-Liby shown in FBI photo
Anas al-Liby alikana kuhusika na ugaidi Marekani

Anayedaiwa kuwa kiongozi wa al-Qaeda amefariki dunia siku chache tu kabla ya kufikishwa mahakamani mjini New York kutokana na mashambulio ya mwaka 1998 barani Afrika kwenye mabalozi ya Marekani.

Abu Anas al-Liby, mwenye umri wa miaka 50, alikufa hospitalini siku ya Ijumaa, mke wake na wakili wake walisema.

Inaripotiwa alikuwa na saratani ya ini.

Bw Liby alikamatwa kwenye uvamizi uliofanywa na Marekani mjini Tripoli Oktoba 2013.

Alitakiwa kufikishwa mahakamani Januari 12 kutokana na mashambulio ya ubalozi mwaka 1998, yalioua zaidi ya watu 220 nchini Kenya na Tanzania.

Bw Liby, ambaye jina lake la ukweli ni Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, awali alikana mashtaka ya kuhusishwa na ugaidi.

Mke wake, Um Abdullah, aliishutumu serikali ya Marekani siku ya Jumamosi kwa “kumteka, kumfanyia mabaya na kumwuua mtu asiye na hatia,” kulingana na shirika la habari la AP.

UJAUZITO KWA NIABA - SURROGACY

Kuchukua mimba kwa niaba ni nini?

 Ni pale ambapo mwanamke anachukua ujauzito kwa nia ya kumkabidhi mtoto kwa mtu mwengine baada ya kujifungua. Kwa kifupi, anabeba ujauzito kwa ajili ya wazazi wasio na uwezo wa kuzaa – wanajulikana kama “wazazi waliokusudiwa”.

Kuna aina mbili za kuchukua mimba kwaajili ya familia nyingine. Kwa desturi, yai la mama anayebeba hiyo mimba ndilo hutumika, ambapo hubaki kuwa mama aliye na asidi nasaba zake, yaani DNA. Aina ya pili, ni pale ambapo yai linatolewa na mama ambaye anataka msaada wa mtoto au mtu aliyejitolea. Yai linarutubishwa kupitia mchakato ambao yai hurutubishwa na mbegu za kiume nje ya mwili wake yaani kwenye maabara, IVF.

Ni halali?
Ina tofauti kutoka nchi hadi nchi

Nchi kama Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi na Bulgaria wanakataza kabisa mfumo wa aina wowote wa kubeba mimba.
surrogate australia
Tukio la Gammy aliyezaliwa na mama aliyebeba ujauzito kwa niaba, limeleta utata Australia na Thailand
Nchi zikiwemo Uingereza, Ireland, Denmark, na Ubelgiji, ubebaji mimba kwa niaba unaruhusiwa pale ambapo mama anayebeba mimba hiyo halipwi, au hulipwa kwa matumizi maalum tu. Kumlipa mama posho (ijulikanayo kama biashara ya ubebabji mimba) ni marufuku.

Biashara ya ubebaji mimba ni halali katika baadhi ya majimbo ya Marekani, na nchi kama India, Urusi na Ukraine.

Watu wanaotaka kuwa wazazi huenda wakaenda nje ikiwa nchi zao za asili haziruhusu mchakato huo wa ubebabji mimba kwa niaba, au kama hawakufanikiwa kupata mwanamke anayeweza kuchukua mimba kwa niaba.

Hata hivyo, hata Australia sheria hubadilika. Kwa mfano, baadhi ya majimbo nchini humo ni kosa la jinai kwenda nchi nyingine kumtafuta mama atayebeba mimba kwa niaba tena kibiashara, wakati wengine huruhusu.

Watu huenda wapi kupata wa kubeba mimba kwa niaba?
Wataalamu wanasema nchi ambazo ni maarufu wa kuwa na akina mama walio tayari kuchukua mimba kwa niaba ni Marekani, India, Thailand, Ukraine na Urusi.

Mexico, Nepal, Poland na Georgia pia ni miongoni mwa nchi zinazotajwa kuwa na uwezekano wa akina mama wa kutoa huduma hizo.

Gharama zinatofautiana katika kila nchi, na pia iantegemea na idadi ya mzunguzko wa IVF unaohitajika, na iwapo bima ya afya inahitajika.
India ni maarufu kwa kutoa mama wa kuchukua ujauzito kwa niaba
India ni maarufu kwa kutoa huduma za mama wa kuchukua ujauzito kwa niaba
Families Through Surrogacy, shirika la kimataifa la kuchukua mimba kwa niaba, limekadiria wastani wa gharama za huduma hiyo katika nchi mbalimbali.
  • US - $100,000 (£60,000)
  • India - $47,350
  • Thailand - $52,000
  • Ukraine - $49,950
  • Georgia - $49,950
  • Mexico - $45,000
Kuna utata gani?
Hakuna sheria zilizokusudiwa na kutambuliwa kwa wanaobeba mimba kwa niaba, kwahiyo wazazi wengi na watoto hubaki wakihaha na wengine hubaki bila utaifa.

Huchukua miezi chungu nzima kumrejesha mtoto aliyetokana na mama aliyebeba mimba kwa niaba, nyumbani kwao kwa asili, kwani huwa hawatambuliki moja kwa moja kama wazazi wao halali.

"Huko Thailand, mama wanaobeba mimba kwa niaba, wanaonekana kuwa mama halali, kwahiyo iwapo wazazi watamwacha mtoto na mama, basi yeye kisheria ana haki,” anasema Bi Scott.

"Huko India, wazazi waliokusudiwa kukabidhiwa mtoto huonekana kuwa wazazi halali, ambapo kutokana na sheria ya Uingereza, mama aliyebeba mimba kwa niaba, anatambulika kama mama halali.

“Hii inamaanisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyebeba mimba kwa niaba nchini India, kutokana na wazazi wa Uingereza, amezaliwa bila utaifa, na lazima aombe uraia wa Uingereza.”


Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

ASKARI KUSEREBUKA



Vimbwanga vya WhatsApp

TUMIA DAMU YA WALIONUSURIKA - WHO

Bag of blood
Damu ya wagonjwa waliopona kutokana na Ebola inatakiwa kutumika kutibu wengine, Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza.

Afrika magharibi inakabiliwa na mlipuko mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya Ebola na zaidi ya watu 2,000 wamefariki dunia.

Kundi la wataalamu duniani wamekuwa wakikutana kutathmini tiba za majaribio zitakazoweza kutibu Ebola.

WHO pia imetangaza kuwa chanjo za Ebola zinaweza kutumika ifikapo mwezi Novemba.

Dawa ya damu               
 
Watu hutengeneza kinga kwenye damukatika jaribio la kupambana na maambukizi ya Ebola

Kinadharia, kinga hizi (antibodies) zinaweza kuhamishwa kutoka mtu aliyenusurika kwa mtu mgonjwa ili kuipa nguvu mfumo wao wa kinga.

Hatahivyo, takwimu za kutosha za ubora wa tiba hiyo hazipo.

Utafiti uliofanyika katika mlipuko wa mwaka 1995 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilionyesha watu saba kati ya nane walipona baada ya kupewa tiba ya aina hiyo.




SCHUMACHER AREJEA NYUMBANI

 

Michael Schumacher ameondoka hospitali ili kuendelea na matibabu akiwa nyumbani, lakini aliyekuwa mshindi wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga Formula One anakabiliwa na "safari ngumu na ndefu siku za usoni" baada ya ajali mwaka jana, kulingana na meneja wake.

"Hivyo, kurejesha hali yake ya kawaida itafanyika nyumbani kwake. Ukizingatia majareha mazito aliyoyapata, kumekuwa na maendeleao mazuri katika kipindi cha wiki na miezi kadhaa," ilisema taarifa fupi iliyotolewa na meneja wake Sabine Kehm.

Msemaji wa hospitali ya chuo kikuu huko Lausanne amethibitisha kuwa Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45, mshindi wa dunia mara saba, aliondoka.

Schumacher alipata majeraha makubwa ya kichwa baada ya kupata ajali kwenye mchezo wa utelezi wa barafu (skii) nchini Ufaransa mwezi Desemba na akahamishiwa Lausanne mwezi Juni baada ya kuibuka kufuatia kupooza.

Alipatiwa matibabu kurejesha hisia zake.

Chanzo: Al-Jazeera
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu