Kuchukua mimba kwa niaba ni nini?
Ni pale
ambapo mwanamke anachukua ujauzito kwa nia ya kumkabidhi mtoto kwa mtu
mwengine baada ya kujifungua. Kwa kifupi, anabeba ujauzito kwa ajili ya
wazazi wasio na uwezo wa kuzaa – wanajulikana kama “wazazi
waliokusudiwa”.
Kuna aina mbili za kuchukua mimba kwaajili ya
familia nyingine. Kwa desturi, yai la mama anayebeba hiyo mimba ndilo
hutumika, ambapo hubaki kuwa mama aliye na asidi nasaba zake, yaani DNA.
Aina ya pili, ni pale ambapo yai linatolewa na mama ambaye anataka
msaada wa mtoto au mtu aliyejitolea. Yai linarutubishwa kupitia mchakato
ambao yai hurutubishwa na mbegu za kiume nje ya mwili wake yaani kwenye
maabara, IVF.
Ni halali?
Ina tofauti kutoka nchi hadi nchi
Nchi kama Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi na Bulgaria wanakataza kabisa mfumo wa aina wowote wa kubeba mimba.
|
Tukio la Gammy aliyezaliwa na mama aliyebeba ujauzito kwa niaba, limeleta utata Australia na Thailand |
Nchi
zikiwemo Uingereza, Ireland, Denmark, na Ubelgiji, ubebaji mimba kwa
niaba unaruhusiwa pale ambapo mama anayebeba mimba hiyo halipwi, au
hulipwa kwa matumizi maalum tu. Kumlipa mama posho (ijulikanayo kama
biashara ya ubebabji mimba) ni marufuku.
Biashara ya ubebaji mimba ni halali katika baadhi ya majimbo ya Marekani, na nchi kama India, Urusi na Ukraine.
Watu
wanaotaka kuwa wazazi huenda wakaenda nje ikiwa nchi zao za asili
haziruhusu mchakato huo wa ubebabji mimba kwa niaba, au kama
hawakufanikiwa kupata mwanamke anayeweza kuchukua mimba kwa niaba.
Hata
hivyo, hata Australia sheria hubadilika. Kwa mfano, baadhi ya majimbo
nchini humo ni kosa la jinai kwenda nchi nyingine kumtafuta mama
atayebeba mimba kwa niaba tena kibiashara, wakati wengine huruhusu.
Watu huenda wapi kupata wa kubeba mimba kwa niaba?
Wataalamu
wanasema nchi ambazo ni maarufu wa kuwa na akina mama walio tayari
kuchukua mimba kwa niaba ni Marekani, India, Thailand, Ukraine na Urusi.
Mexico, Nepal, Poland na Georgia pia ni miongoni mwa nchi zinazotajwa kuwa na uwezekano wa akina mama wa kutoa huduma hizo.
Gharama
zinatofautiana katika kila nchi, na pia iantegemea na idadi ya
mzunguzko wa IVF unaohitajika, na iwapo bima ya afya inahitajika.
|
India ni maarufu kwa kutoa huduma za mama wa kuchukua ujauzito kwa niaba |
Families Through Surrogacy, shirika la kimataifa la kuchukua mimba kwa niaba, limekadiria wastani wa gharama za huduma hiyo katika nchi mbalimbali.
- US - $100,000 (£60,000)
- India - $47,350
- Thailand - $52,000
- Ukraine - $49,950
- Georgia - $49,950
- Mexico - $45,000
Kuna utata gani?
Hakuna
sheria zilizokusudiwa na kutambuliwa kwa wanaobeba mimba kwa niaba,
kwahiyo wazazi wengi na watoto hubaki wakihaha na wengine hubaki bila
utaifa.
Huchukua miezi chungu nzima kumrejesha mtoto aliyetokana
na mama aliyebeba mimba kwa niaba, nyumbani kwao kwa asili, kwani huwa
hawatambuliki moja kwa moja kama wazazi wao halali.
"Huko
Thailand, mama wanaobeba mimba kwa niaba, wanaonekana kuwa mama halali,
kwahiyo iwapo wazazi watamwacha mtoto na mama, basi yeye kisheria ana
haki,” anasema Bi Scott.
"Huko India, wazazi waliokusudiwa
kukabidhiwa mtoto huonekana kuwa wazazi halali, ambapo kutokana na
sheria ya Uingereza, mama aliyebeba mimba kwa niaba, anatambulika kama
mama halali.
“Hii inamaanisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyebeba
mimba kwa niaba nchini India, kutokana na wazazi wa Uingereza, amezaliwa
bila utaifa, na lazima aombe uraia wa Uingereza.”
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu