UMEPATA kusikia jina la Dk. Asanterabi Malima?
Jambo
moja ambalo wanafunzi waliosoma naye nchini Tanzania hawabishani kuhusu
Malima ni ukweli kwamba alikuwa ni mwanafunzi mwenye akili nyingi
darasani.
Shafii Dauda ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha
kwanza katika Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam,
anamkumbuka Asanterabi kama mwanafunzi mwenye akili aliyefanya vizuri
sana katika masomo yake ya kumaliza kidato cha nne.
Shafii, ambaye
sasa ni miongoni mwa watangazaji na wachambuzi maarufu wa
mchezo wa
soka hapa nchini alikuwa kidato cha kwanza wakati Malima alikuwa kidato
cha nne.
Akili ile ya Malima imemfikisha nchini Marekani ambako
sasa amefanya ugunduzi wa kidude chenye saizi ya pini ndogo (milimita
0.250) kinachoweza kubaini magonjwa ya kuambukiza, kansa na moyo katika
hatua ya awali kabisa.
Mtafiti wa Kisayansi
Ugunduzi huu, utakapofika mwisho wake,
unaweza kuokoa maisha ya watu wengi duniani. Fikiria tu kwamba unakuwa
na kifaa ambacho mojawapo ya magonjwa hayo yakikuanza unaubaini mapema
na kwenda kutibiwa.
Mamilioni ya watu wataokolewa maisha yao na kijana huyu wa Kitanzania.
“Siku
zote nimekuwa na ndoto za kugundua kitu ambacho kitaweza kuokoa maisha
ya watu. Baba yangu alifariki kwa ugonjwa wa moyo ambao ungegundulika
mapema kama kungekuwa na kifaa kama hiki.
“Kwa sasa sitaweza
kuokoa maisha ya baba yangu lakini ninaweza kuokoa maisha ya wazazi au
watoto wa watu wengine kutokana na ugunduzi huu nilioufanya. Nafurahi
kwamba ndoto yangu imetimia.
“Kansa, baadhi ya magonjwa ya
kuambukizwa na magonjwa ya moyo huwa yanachelewa sana kugundulika. Watu
wengi hupoteza maisha, na kwa nchi zilizoendelea hutumia pesa nyingi
sana kuwatibu waathirika.
“Kifaa nilichogundua ni kidude cha
ukubwa wa pini (0.250mm) kinachoweza kupima na kugundua hayo magonjwa
mapema. Ili, yaweze kutibika kirahisi, kuokoa maisha na kupunguza
gharama,” anasema
Asanterabi katika mazungumzo yake na Raia Mwema
yaliyofanyika kwa njia ya mtandao juzi Jumatatu.
Asanterabi ni
mtoto wa aliyepata kuwa waziri wa fedha wa Tanzania, Profesa Kighoma Ali
Malima, aliyefariki dunia Agosti 6, 1995 jijini London, Uingereza,
katika mojawapo ya vifo vya kushtusha katika historia ya Tanzania.
Kifaa
alichokigundia kijana huyu wa Kitanzania kinafahamika kwa jina la
Biolom na ugunduzi huu aliufanya akishirikiana na wanafunzi wenzake
wawili wa Chuo Kikuu cha Northeastern kilichopo Boston; Cihan Yilmaz na
Jaydev Upponi.
Pamoja na udogo wake, kipini hicho kina jumla ya
maeneo manne –yote yenye kazi maalumu, na ubunifu huo tayari
umetambuliwa na Serikali ya Marekani.
Katika mazungumzo yake na
vyombo vya habari vya Marekani, Asanterabi alipata kusema kwamba vifaa
vingi vya kisasa hubaini magonjwa; kwa mfano kansa, katika wakati ambapo
ni vigumu mtu kupata tiba na kupona.
“Kazi yetu hii
itakapokamilika, tutaweza kubaini magonjwa haraka zaidi na mapema zaidi
na hivyo watu watapata tiba mapema na kuokoa maisha.
“Nchini
kwangu (Tanzania), akinamama wengi hufariki dunia kwa sababu ya kuugua
ugonjwa wa kansa ya kizazi, kifaa hiki kitaweza kusaidia watu wengi
kupona kutoka katika matatizo yao,” alisema.
Kidude hicho ni
kidogo sana kwa umbo na namuuliza kama wameamua iwapo mtu anaweza
kukinunua na kubaki nacho nyumbani akijitazama mwenyewe au ni lazima
aende hospitali.
“Dhamira yetu hapo ni kipimo kitumike mtu akienda
hospitali au kliniki (for annual check-up). Lakini japokuwa kinafanya
kazi, kupata ruhusa kwa kukiingiza kama pini ni vigumu. Tunafanya vipimo
(test) kwa kupima damu iliyotoka kwa mgonjwa,” anasema.
Elimu yake
Sunday, 28 September 2014
NYOTA WA FILAMU GEORGE CLOONEY AFUNGA NDOA
Nyota muigizaji wa Hollywood George Clooney amemwoa mwanasheria wa kutetea haki za binadamu Amal Alamuddin huko Venice, miongoni mwa matukio yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu zote.
Wenzake ambao ni maarufu pia kwenye tasnia ya uigizaji na uimbaji katika mji wa Italia walimiminika kushuhudia muungano huo wa kapera maarufu katika uwanda wa filamu, mwenye umri wa miaka 53, na Bi Alamuddin, mwenye umri wa miaka 36.
Shughuli hiyo ilisherehekewa katika hoteli iliyoelekea kwenye mfereji mkubwa wa Venice.
Wakala wa Clooney walitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.
Kulingana na shirika la habari la AP, hiyo ndio itakuwa taarifa pekee itakayotolewa kuhusu harusi hiyo.
Saturday, 27 September 2014
HUKUMU YA HOSNI MUBARAK KUTOLEWA KARIBUNI
![]() |
| Mubarak alisafirishwa kwa helikopta ya jeshi kufikishwa mahakamani siku ya Jumamosi |
Mahakama ya Misri inatarajia kutoa uamuzi kwenye kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak kwa makosa ya rushwa na kuua waandamanaji wakati wa ghasia za mwaka 2011.
Mubarak, mwenye umri wa miaka 86, anashtakiwa pamoja na watoto wake wa kiume na aliyekuwa waziri.
Alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2012, lakini hukumu hiyo baadae ilibadilishwa.
Mubarak aliiongoza Misri kwa takriban miaka 30 kabla ya ghasia kuibuka na kuondolewa.
Aliachia madaraka baada ya wiki kadhaa za vurugu zilizosababisha vifo vya mamia ya waandamanaji nchini humo.
Kesi hiyo mpya ilianza Aprili 2013, na imeahirishwa mara chungu nzima.
Wachambuzi wanasema Mubarak huenda akaachiwa huru, baada ya mashahidi wengi kubadilisha ushahidi wao na ukiegemea upande wake.
Mubarak tayari anatumikia miaka mitatu gerezani kwa ubadhirifu wa mali ya umma.
Alikutwa na hatia mwaka 2012 kwa mashtaka yanayohusiana na mauaji ya waandamanaji pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Habi al-Adly, na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Watoto wake wa kiume Alaa na Gamal nao kwa sasa wanatumikia kifungo cha miaka minne jela kwa ubadhirifu wa mali za serikali.
Pamoja na baba yao walitozwa faini $3m na kuamriwa kurejesha $17.6m waliotuhumiwa kuiba.
CHELSEA CLINTON AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE
![]() |
| Mtoto wa Chelsea ni mjukuu wa kwanza wa Bill na Hillary Clinton |
Chelsea Clinton, binti wa aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Hillary Clinton, amejifungua mtoto wa kike.
"Mimi na Marc tuna mapenzi, furaha na tunatoa shukran wakati tukisherehekea kuzaliwa kwa binti yetu, Charlote Clinton Mezvinsky, " Bi Clinton aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter.
Bi Clinton, mwenye umri wa miaka 34, aliolewa na Marc Mezvinsky mwaka 2010, na kutangaza kuwa mjamzito Aprili 2014.
Binti huyo anazaliwa huku Bi Hillary Clinton akiwa na nia ya kugombea urais mwaka 2016.
Anaonekana kuwa mgombea mkuu kupitia chama cha Democrat na mrithi wa Rais Barack Obama, na alisema atachukua uamuzi wa kugombea au la mwanzoni wa mwaka 2015.
Bill Clinton alikuwa rais wa 42 Marekani , kuanzia Januari 1993 hadi Januari 2001.
Chelsea Clinton, alisomea vyuo vikuu vya Stanford, Columbia na Oxford, anasimamia Wakfu wa Clinton akishirikiana na wazazi wake.
Bi Clinton aliacha kazi iliyokuwa ikimlipa $600,000 kwa mwaka kama mwandishi maalum wa habari wa NBC mwezi Agosti ili ashughulike na ujauzito wake.
WACHEZA KRIKETI WAWEKA REKODI MLIMA KILIMANJARO
![]() |
| Kupumua na kukimbia kuna uziyo kwenye sehemu hiyo ya juu |
Kundi la wacheza kriketi wa kimataifa wameweka rekodi mpya ya dunia kwa kucheza mechi kubwa kwenye kilele cha Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi Afrika, uliopo nchini Tanzania.
Timu hizo zinamhusisha mrusha mpira wa zamani wa Afrika Kusini Makhaya Ntini na mrusha mpira wa zamani wa England, Ashley Giles.
Mechi hiyo ilichezwa kwenye urefu wa mita 5,730 (futi 18,799) kwenye eneo lilinyooka chini kidogo ya kilele.
![]() |
| Kulikuwa na hali ya baridi na kuganda kwa barafu kwenye eneo hilo |
Hii kweli maajabu! Tunacheza kriketi kwenye kilele cha Afrika, Giles alituma ujumbe kwenye Twitter.
Rekodi ya hivi karibuni ya mechi kubwa ni ile mita 5,165, iliyochezwa kwenye milima ya Himalaya, kwenye kambi ya mlima Everest nchini Nepal mwaka 2009.
Chanzo: taarifa.co.tz
Friday, 26 September 2014
WENYE MATATIZO YA AKILI KUONGEZEKA, UGANDA
Wataalamu wametoa wito wa kushirikiana zaidi kwa huduma za watu wenye matatizo ya akili na huduma na tiba kwa walioathirika na Ukimwi na huduma ya afya kwa jumla.
Wito huo umetolewa baada ya idadi ya watu wenye matatizo ya akili kuongezeka nchini Uganda hasa watu wanaoishi na Ukimwi.
Dk Sheila Ndyanabangi, afisa mkuu wa tiba wa wenye matatizo ya akili katika wizara ya afya, alisema idadi ya watu wenye matatizo ya akili kuripotiwa imeongezeka kwa 17,000 kati ya mwaka 2009 hadi 2012.
Alisema idadi hiyo inatokana na migogoro ya hivi karibuni na kupanuka kwa miji iliyowalazimu watu wengi kujihusisha na kamari na kukopa mara kwa mara, pamoja na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
Takriban 56% ya Waganda wanaoishi na virusi vya HIV wana msongo wa mawazo, na dalili kama kulala kwa tabu, kutokuwa na hamu ya kula, na kusikia uchovu mara zote.
Dalili nyingine ni huzuni, na kuzongwa na mawazo yaliyojaa matatizo. Japo si jambo linalotokea sana, baadhi ya watu huzidiwa na msongo wa mawazo mpaka hutaka kujiua.
Chanzo: New vision, Uganda
Thursday, 25 September 2014
ASAMOAH GYAN AKANA KUMTOA RAFIKI YAKE 'KAFARA'

Kapteni wa Ghana Asamoah Gyan alisema madai kuwa alimwuua rafiki yake ambaye ni msanii wa miondoko ya hip-hop Castro kama sehemu ya kafara ni “ upuuzi mtupu”.
Msanii Castro, ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka , pamoja na rafiki yake Janet Bandu,mwezi Julai.
Walitoweka walipoenda likizo na familia ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Sunderland , Gyan katika mji wa Ada kwenye pwani ya Ghana.
Madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Ghana vinasema kutoweka huko kunaonyesha mazingira ya utata.
Castro na Bandu mara ya mwisho walionekana wakielekea kwenye pwani hiyo kwenye motokari ya majini ‘jet ski’ na baadae kutangazwa kuwa walizama.
Hakuna miili yoyote iliyoopolewa mpaka sasa na uvumi uliendelea kusambazwa mwezi huu baada ya kaka yake, Baffour Gyan, akidaiwa kuwa sehemu ya genge lililomshambulia mwandishi wa habari aliyemhoji mchezaji huyo kuhusu uvumi huo.
Kwa sasa hata hivyo, Baffour Gyan amefutiwa makosa yake.
Hisia hizo zilisababisha Gyan mwenye umri wa miaka 28 aliyejiunga na Al-Ain ya UAE mwaka 2011, kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Wakili wake Kissi Agyabeng alisema familia yake imepata "mshtuko" na wamebaki kimya mpaka sasa kwa kuwa hawakutaka kuingilia uchunguzi wa polisi.
"MBU WAZURI" KUPAMBANA NA DENGE - BRAZIL
Watafiti wa Brazil mjini Rio de Janeiro wamewatawanya maelfu ya mbu walio na bakteria anayefubaza homa ya dengu.
Matumaini ni kuwa watazaliana, na kuongezeka kwa wingi, hivyo kupunguza watu wanaopata ugonjwa huo.
Mchakato huo ni sehemu ya mradi unaofanyika pia Australia, Vietnam na Indonesia.
Bakteria huyo, Wolbachia, hawezi kuingiziwa kwa binadamu
Mradi huo ulianza mwaka 2012 alisema Luciano Moreira wa taasisi ya utafiti ya Brazil iitwayo Fiocruz, ambaye ndiye anasimamia utafiti huo.
Alisema maelfu ya mbu hao wataachiwa wazunguke wanapotaka kila mwezi kwa muda wa miezi minne, mwanzo wakianzia Tubiacanga, kaskazini mwa Rio.
Bakteria "Wazuri'
Bakteria Wolbachia anapatikana kwenye wadudu kwa 60%. Hufanya kazi kama kinga kwa mbu anayehifadhi denge, Aedes aegypti, akizuia virusi vya dengu kuzaliana mwilini.
Wolbachia pia ana athari yake kwenye uzalishaji. Ikatokea mbu dume aliye na virusi hivyo akarutubisha mayai ya jike bila ya bakteria hao, mayai hayo hayaingii kwenye hatua ya lava.
Iwapo wote jike na dume wakiwa na virusi hivyo au kama jike tu ndio ana bakteria, vizazi vyote vya siku za usoni vya mbu hao watakuwa na Wolbachia.
Kwa matokeo hayo, mbu wa Aedes ambao wana Wolbachia wanakuwa wengi bila hata watafiti kuendelea kuwasambaza wadudu walioathirika kila mara . Maradhi ya dengu yaliibuka upya Brazil mwaka 1981 baada ya kutoweka kabisa kwa zaidi ya miaka 20.
Baada ya miaka 30 iliyofuata, watu milioni saba waliripotiwa kuathirika.
Brazil inaongoza duniani kwa idadi ya watu walioathirika na denge, huku wakiwepo watu milioni 3.2 walioathirika na 800 kufariki kutokana na ugonjwa huo baina ya mwaka 2009 - 2014.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Matumaini ni kuwa watazaliana, na kuongezeka kwa wingi, hivyo kupunguza watu wanaopata ugonjwa huo.
Mchakato huo ni sehemu ya mradi unaofanyika pia Australia, Vietnam na Indonesia.
Bakteria huyo, Wolbachia, hawezi kuingiziwa kwa binadamu
Mradi huo ulianza mwaka 2012 alisema Luciano Moreira wa taasisi ya utafiti ya Brazil iitwayo Fiocruz, ambaye ndiye anasimamia utafiti huo.
Alisema maelfu ya mbu hao wataachiwa wazunguke wanapotaka kila mwezi kwa muda wa miezi minne, mwanzo wakianzia Tubiacanga, kaskazini mwa Rio.
Bakteria "Wazuri'
Bakteria Wolbachia anapatikana kwenye wadudu kwa 60%. Hufanya kazi kama kinga kwa mbu anayehifadhi denge, Aedes aegypti, akizuia virusi vya dengu kuzaliana mwilini.
Wolbachia pia ana athari yake kwenye uzalishaji. Ikatokea mbu dume aliye na virusi hivyo akarutubisha mayai ya jike bila ya bakteria hao, mayai hayo hayaingii kwenye hatua ya lava.
Iwapo wote jike na dume wakiwa na virusi hivyo au kama jike tu ndio ana bakteria, vizazi vyote vya siku za usoni vya mbu hao watakuwa na Wolbachia.
Kwa matokeo hayo, mbu wa Aedes ambao wana Wolbachia wanakuwa wengi bila hata watafiti kuendelea kuwasambaza wadudu walioathirika kila mara . Maradhi ya dengu yaliibuka upya Brazil mwaka 1981 baada ya kutoweka kabisa kwa zaidi ya miaka 20.
Baada ya miaka 30 iliyofuata, watu milioni saba waliripotiwa kuathirika.
Brazil inaongoza duniani kwa idadi ya watu walioathirika na denge, huku wakiwepo watu milioni 3.2 walioathirika na 800 kufariki kutokana na ugonjwa huo baina ya mwaka 2009 - 2014.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Wednesday, 24 September 2014
BOKO HARAM WAJISALIMISHA, MKUU 'ADAIWA' KUUAWA
Jeshi la Nigeria limesema zaidi ya wapiganaji 260 wa Boko Haram wamejisalimisha kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji pia alisema jeshi limemwuua aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau.
Mohammed Bashir inasemekana alitokea kwenye video ikionyesha kundi hilo lakini anahisiwa kuwa si Shekau halisi.
Boko Haram limepoteza wapiganaji wengi katika wiki za hivi karibuni wakati jeshi la Nigeria likipambana nao karibu na makazi yao makuu Maiduguri, kaskazini -mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo lilisema wafuasi 135 wa Boko Haram walijisalimisha pamoja na silaha zao Biu, jimbo la Borno, siku ya Jumanne - na wengine 133 huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambapo kwa sasa wanahojiwa.
Mwandishi wa BBC Will Ross aliyopo Lagos alisema hatua kama hii haijawahi kutokea tangu vita vya kupambana na Boko Haram kuanza.
Licha ya kwamba ni vigumu kuthibitisha, jeshi linaona tukio hili kuwa jambo lenye umuhimu sana.
KIUMBE CHA AJABU KUIBUKA PEMBA
Katika
hali isiyo ya kawaida huko maeneo ya bahari ya Shamiani (kwa Gombe) jimbo la
kiwani mkoa wa kusini Pemba kumeibuka kiumbe kikubwa cha ajabu kutoka baharini
ambacho kimepwewa.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wakaazi wa maeneo ya jirani na eneo hilo
ambao wamefurika kwa wingi kwenda kuona kiumbe hicho wamesema kuwa ni mara ya
kwanza kuona kiumbe cha namna hicho kikiwa kimepwewa ndani ya bahari.
Baadhi
yao wameeleza kuwa huenda pengine kiumbe hicho cha ajabu chenye urefu takribani
mita 40 na upana zaidi ya mita 25 kikawa ni samaki aina ya nyangumi au
chongowe.
Katika
hali ya kushangaza ndani ya fukwe hizo za bahari ya kwa Gombe watu zaidi ya 200
kutoka maeneo jirani ya Likoni,mwambe na ngambu shamiani wamejitokeza kuona kiumbe
hicho cha ajabu ambacho tayari kimekufa.
Aidha
makundi ya wananchi wanaendelea kukata minofu ya aina hiyo ya kiumbe huku
wengine wakijaza madumu yao mafuta yanayotiririka kutoka kwa kiumbe hicho.
Kwa
upande wake mtalamu wa viumbe vya bahari Zanzibar kwa masharti ya kutotajwa
jina amesema msimu huu viumbe vya bahari aina ya nyangumi hupita katika ukanda
wa bahari ya hindi.
“Inaonekana
baadhi ya watu huwapiga viumbe vya bahari vya aina hii ndio maana hufariki
dunia,hali hii inaitia nchi yetu jina baya kimataifa tunaonekana tunawaua kwa
makusudi’’aliongezea mtaalamu huyo.
Alieleza
kuwa kitengo chao kimeshatoa elimu sana ili wananchi waache tabia hii ya kuwaangamiza
viumbe hawa kwani dunia haikubali kwa sasa kwa vile ni viumbe adimu na
muhimu.
Aidha
alieleza alishauri wananchi wakiona kiumbe kama hicho kikiwa hai basi watoe
taarifa kwa wahusika ili aweze kurudishwa baharini.
Hali hii
ya kuonekana kiumbe cha ajabu ni mara ya kwanza kwa maeneo haya ambapo kumeibua
mshangao.
Chanzo: WhatsApp
ABU QATADA AFUTIWA MASHTAKA YA UGAIDI
![]() |
| Abu Qatada alishtakiwa kwa jaribio la kuwashambulia Waisraeli, Wamarekani na wengine wa nchi za magharibi |
Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali Abu Qatada amekutwa hana hatia ya makosa ya kigaidi na mahakama ya Jordan.
Jopo la majaji wa kiraia wa mahakama ya Amman wamemfutia mashtaka ya kuhusika katika jaribio la kufanya shambulio lililokusudiwa katika sherehe za millennia mwaka 2000.
Uamuzi huo unatolewa baada ya kufutiwa mashtaka mwezi Juni ya jaribio la kufanya shambulio kwa kutumia mabomu nchini Jordan mwaka 1998.
Abu Qatada alihamishwa kutoka Uingereza mwaka 2013.
Uamuzi huo unafuatia msuguano wa kisheria wa muda mrefu baina ya mawaziri nchini Uingereza kulazimisha mhubiri huyo kushtakiwa kwao Jordan.
Japo atakuwa huru siku za hivi karibuni, hatorejea London.
Mhubiri huyo, ambaye jina lake halisi ni Omar Othman, alipewa hifadhi Uingereza mwaka 1994, lakini shirika la usalama MI5 lilizidi kumwona tishio kwa usalama wa taifa.
WACHUNGAJI WALAWITI WATOTO, ARUSHA
Watoto sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Watoto sita waliobakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la Field Force, Kwamorombo jijini Arusha.
Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000 za kufungia mdomo.
“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’ alisema mwanafunzi mmoja.
Tuesday, 23 September 2014
SHAIRI - BINGWA AMETOKA KAPA
Alileta zake mbwebwe, Na mashabiki lukuki
Akasema hata Wembe, Ukiletwa hakatiki
Yeye anakula sembe, Wali kwake hashituki
Bingwa ametoka kapa, Aso bingwa hali gani?
Akaivaa na jezi, Ugani akajitosa
Na kuwaita Malezi, Wale walokula kasa
Kumbe vile hajiwezi, Ni lijoka la kipisa
Bingwa ametoka kapa, Aso bingwa hali gani?
Aliposhindwa ugani, La kusema alikosa
Kusingizia utani, Kumbe vile ni garasa
Walikwama wa maini, We utumbo ndo kabisa
Bingwa ametoka kapa, Aso bingwa hali gani?
Unapokwenda mechini, Muhimu ujizatiti
Usijitie kundini, Na kuleta tashtiti
Ukija bila plani, Utarudi umaiti
Bingwa ametoka kapa, Aso bingwa hali gani?
Shairi hili limeandikwa na Wazir Khamsin
Subscribe to:
Comments (Atom)






