Thursday, 18 September 2014

MEYA WA TORONTO APATA SARATANI YA 'KIPEKEE'



Rob Ford
Bw Ford alilazwa hospitali siku ya Alhamis na kukutwa na uvimbe tumboni

Meya wa Toronto Rob Ford amekutwa na saratani ambayo ni nadra mtu kupata “na ni ya hatari ”, madaktari wanaomtibu wamesema.
.
Bw Ford, mwenye umri wa miaka 45, ana saratani inayoweza kusambaa haraka kwenye tumbo lake

Anatarajia kuanza matibabu ya mionzi katika kipindi cha saa 48 zijazo.

Ana uvimbe wa sentimeta 12 kwa 12 kwenye tumbo na nyingine ndogo yenye sentimeta 2 kwenye tako lake la kushoto, ambapo inaaminiwa kukua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

“Nina matumaini makubwa kuhusu tiba hii,” alisema Dk Zane Cohen, ambaye anasimamia timu nzima inayomshughulikia meya huyo.

Bw Ford alijiengua kwenye kampeni za uchaguzi mpya baada ya kupatikana na uvimbe wa tumbo.

Meya huyo mwenye utata, aliyekiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine akiwa bado madarakani, bado ana wafuasi wengi licha ya wito wa kutaka ajiuzulu.

Pia aliwahi kuchukuliwa video akitishia kumwuua mtu asiyejulikana, na pia kutoa kauli chafu za ngono kwa waandishi wa habari.



Wednesday, 17 September 2014

UFAHAMU ZAIDI KUHUSU KURA YA MAONI YA USKOCHI

Alhamsi wananchi wa Uskochi watapiga kura ya maoni kuamua iwapo wajitenge na Uingereza au la. Wananchi watajua ikiwa Uskochi itajiondoa kutoka muungano na Uingereza, muungano ambao umedumu kwa miaka 307.

Hadi sasa kura ya maoni inaonyesha kuwa kuna ushindani mkubwa kati ya wanaotaka muungano kuvunjwa na wale wanaotaka muungano kusalia.

Peter Musembi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC anakufahamisha zaidi

CHUO CHA NIGERIA CHASHAMBULIWA

Security officers stand guard at the campus of Kano State Polytechnic on 30 July
Milio ya risasi na mlipuko umesikika katika chuo cha walimu cha mafunzo kwenye mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria.
Wanafunzi walionekana wakikimbia kutoka chuo hicho.
Mwanafunzi mmoja aliiambia BBC kuwa aliona miili 17 katika eneo hilo.
Haiko wazi nani anahusika na shambulio hilo, japokuwa hisia zitaelekea kwa kundi la Boko Haram, ambalo limekuwa likifanya mashambulio Nigeria tangu mwaka 2009.
Mwezi Julai mji huo ulikumbwa na mashambulio matano katika kipindi cha siku nne, moja likiwa limelengwa kwenye chuo kingine na kuua sita.
Mwezi Mei 2013, Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo ya kusini ya Borno, Yobe na Adamawa, akiahidi kuwamaliza wapiganaji hao.
Hatahivyo wapiganaji hao wameongeza mashambulio, na kuua zaidi ya raia 2,000 mwaka huu, kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu HRW.

WAAFRIKA KUSINI WENGI WAMEKUFA KANISA LA TB JOSHUA

Rescue workers carry a survivor into an ambulance in Lagos, Nigeria, on 13 September 2014.
Kupatikana kwa wengine walionusurika kulichochea harakati za msako kuendelea

Takriban raia 67 wa Afrika kusini walifariki dunia baada ya kanisa linalomilikiwa na mhubiri TB Joshua lilipoporomoka mjini Lagos wiki iliyopita, Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema.

Haijulikani ni idadi ya watu wangapi wamekufa kwa jumla, lakini idadi ya mwanzo iliyotolewa ni watu 60.

Ni tukio baya kabisa kuwahi kutokea lililohusisha raia wa Afrika kusini walio nje ya nchi "katika historia yetu", alisema Bw Zuma.

Bw Joshua, mhubiri maarufu sana kutoka Nigeria, anajulikana Afrika nzima.

Bw Joshua alisema ndege ndogo ilikuwa ikizunguka juu ya jengo hilo kabla ya kuporomoka siku ya Ijumaa mchana, na kusema lilikuwa jaribio la kumwuua.

Hatahivyo, siku ya Jumanne, afisa wa uokoaji alisema inaonyesha sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo ni kuongeza ujenzi kwa juu kabla ya kuimarisha msingi.

Takriban watu 130, wakiwemo raia wengi wa kigeni, walitolewa kwenye kifusi.

Bw Joshua, ambaye pia anajulikana kama mtume, huwahubiriwa watu wengi sana katika makanisa makubwa wilaya ya Ikotuna mjini Lagos.

Wafuasi wake nchini Nigeria na nchi za nje wanaamini ana kipaji cha kuponya na utume.


BINTI ARIDHIKA LICHA YA KUWA NA NDEVU


 



Vimbwanga vya WhatsApp    

DAKIKA ZA MWISHO ZA KAMPENI USKOCHI



 Yes supporters at rally in George Square

Pande zote mbili katika mjadala juu ya kura za maoni za Uskochi wako katika dakika za lala salama kuwashawishi wapiga kura ikiwa ni siku ya mwisho ya kampeni.

Haya yanatokea huku matokeo ya maoni yaliyotolewa hivi karibuni yanaonyesha kura hizo zinakaribiana sana, ambapo kura ya “Hapana” (wasitengane) inaongoza kwa kiwango kidogo sana.

Waziri kiongozi wa Uskochi Alex Salmond amewaandikia wapiga kura akiwataka wapige kura ya “Ndio”, akisema “wakati ndio huu”.

People with vote No banners and balloons

Wanaoongoza kampeni ya kuunga mkono muungano waitwao ‘Better Together’ walikesha  kuwasahaiwshi wale wanaofanya kazi usiku, huku wale wanaopinga wakiwa na kauli mbiu ya “Love Scotland”.

Maoni mengine yaliyochapishwa na magazeti matatu, siku ya Jumanne, huku wale ambao hawajaamua bado kuchagua upande upi, yote yameonyesha kura ya “Hapana” inaongoza kwa 52% kwa 48%.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

 

Tuesday, 16 September 2014

AJIUA KWA KUJIRUSHA MDOMONI MWA MAMBA

This picture taken on 15 September 2014 shows crocodiles in and outside a pond at the farm where a woman killed herself in Samut Prakarn, outside Bangkok.
Bi Wanpen alijirusha kwenye eneo hili la kuhifadhia mamba Samut Prakarn

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Bangkok amejiua kwa kujirusha kwenye kundi la mamba eneo wanalofugwa karibu na mji mkuu, polisi walisema.

Walioshuhudia walimwona Wanpen Inyai akijirusha kwenye dimbwi la mamba hao, gazeti la Bangkok Post liliripoti.

Wafanyakazi wa eneo hilo walishindwa kumwokoa.

Polisi walisema waliambiwa na familia yake kuwa Bi Wanpen alionekana mwenye msongo wa mawazo kabla ya kifo chake.

Vivutio vya kitalii vya Thai inasemwa aghalabu huwa na sheria kali za kiusalama.

Kulingana na ripoti iliyotolewa, alivua viatu vyake kabla ya kujirusha katikati ya bwawa hilo lenye  kina cha mita 3 lililo na mamia ya mamba.

Wafanyakazi wa eneo hilo la kitalii walijaribu kutumia fimbo ndefu kuzuia mamba hao kumshambulia mama huyo, kulingana na Bangkok Post.

Mapema siku hiyo, familia ya Bi Wanpen ilijaribu kuripoti kuwa hajulikani alipo baada ya kuona alitoweka, lakini waliambiwa wasubiri hadi saa 24.

Kifo kama hicho kiliwahi kutokea mwaka  2002 katika eneo hilohilo, na mwengine pia alijiua hapohapo muongo mmoja uliopita.



WAFANYAKAZI WA KIGENI LA! SUDAN KUSINI

Men carry maize flour sacks during a food distribution by the Catholic Church to refugees and displaced people in Juba on 30 August 2014
Kuna wasiwasi hatua ya serikali hiyo itavuruga jitihada za kupambana na ukosefu wa chakula

Serikali ya Sudan kusini imetoa amri kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na makampuni binafsi kuwafukuza baadhi ya wafanyakazi wa kigeni ifikapo mwezi Oktoba.

Wizara ya kazi imesema kazi kama za mapokezi hadi wakurugenzi katika siku za usoni zifanywe na raia wa Sudan kusini.

Shirika la kutoa misaada la Oxfam limesema hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kwenye miradi hiyo ya misaada.

Takriban watu milioni mbili wamekimbia makazi yao tangu makundi mawili hasimu wa chama tawala kupigana mwezi Desemba.

Maelfu ya watu wamekufa kwenye mapambano hayo na mashirika ya kutoa misaada yamesema hadi watu milioni nne wako katika hatari ya kukosa chakula kutokana na mgogoro huo.

Kilichoanza kama ugomvi wa kisiasa baina ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa naibu wake Riek Machar uligeuka kuwa mapigano ya kikabila.


SEPP BLATTER APATA MPINZANI FIFA 2015


Jerome Champagne ametangaza nia ya kupambana na Sepp Blatter katika kuwania urais wa Fifa.
Jerome Champagne ametangaza nia ya kupambana na Sepp Blatter katika kuwania urais wa Fifa

Jerome Champagne ametangaza nia ya kupambana na Sepp Blatter katika kuwania urais wa Fifa.

Raia wa Ufaransa Jerome Champagne amethibitisha mipango yake kupambana na Sepp Blatter kwa ajili ya urais wa Fifa.

Blatter alitangaza nia yake ya kuwania muhula wa tano wiki iliyopita.

Mwanadiplomasia Champagne, 56, alifanya kazi Fifa kwa miaka 11 kama mkurugenzi kabla ya kuondoka 2010.

“Nimeshawaandikia Kamati ya Uchaguzi ya Fifa na rais wake, Bw Domenico Scala, kuthibitisha nia yangu ya kugombea urais wa Fifa,” aliandika mtandaoni.

Champagne anahitaji msaada wa wanachama watano wa Vyama vya Soka wa Fifa ila hawezi kutangaza ni wa kina nani mpaka tangazo rasmi litakapotolewa mwezi Januari.

Uchaguzi utafanyika kwenye mkutano wa Fifa mwezi Juni mwakani.
Chanzo: taarifa.co.tz

MBUNGE KEISSY AWAKERA WAZANZIBARI

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ally Juma Khatibu akizungumza baada ya kukerwa na kauli za Mjumbe mwenzake, Ally Keissy, bungeni Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ally Keissy jana alilazimika kusindikizwa na askari wa Bunge kuondoka katika viwanja vya eneo hili kumnusuru na hasira za wajumbe kutoka Zanzibar waliokerwa na mchango wake kuhusu masuala ya Muungano.

Kessy alisimama bungeni hapo saa 5:52 asubuhi kutoa mchango wake kuhusu Katiba akijikita zaidi katika suala la muundo wa Muungano na kusema kwamba Zanzibar inabebwa na Tanganyika.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanganyika inabeba mzigo mkubwa ambao haubebeki, hapa tunahudumia wabunge 83 kutoka Zanzibar ambao wanatibiwa wao na wake zao na watoto kwa gharama za Tanganyika wakati hawachangii,” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kwa Tanganyika kubeba mzigo mkubwa kama huo wakati katika Jimbo lake la Nkasi wananchi wanalia na shida ya maji.

Alisema katika Kamati yao Namba Moja, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu alitoa semina iliyoonyesha kuwa Zanzibar haichangii chochote kwenye Muungano na kuwa hata mishahara wakati mwingine wanategemea Tanganyika.

Keissy alisema wananchi wakilijua jambo hilo, wataikataa Katiba inayopendekezwa na kuitupilia mbali kwa kuwa inatoa upendeleo kwa Wazanzibari na kuikandamiza Tanganyika.

“Mimi naweza kuwa na wanawake sita, nikazaa nao lakini kila mtoto anaendelea kutunzwa na baba yangu, jambo kama hili halivumiliki hata kidogo japo najua kuwa ukweli unawauma,” alisema huku baadhi ya wajumbe wakipaza sauti wengine kumpinga na wengine kuomba mwongozo wa mwenyekiti.

Alipinga suala la rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa Muungano kwa maelezo kuwa katika mfumo wa vyama vingi jambo kama hilo haliwezekani na kuhoji itakuwaje awe makamu wa kwanza wa rais wakati hajachaguliwa na wananchi wa Tanzania Bara?

Monday, 15 September 2014

WAAFRIKA WATUMIA TAKRIBAN $7 BIL. KWA NYWELE BANDIA

 
Licha ya raslimali ndogo za fedha, Waafrika wanatumia takriban dola za kimarekani bilioni 7 kwenye nywele.

Kulingana na shirika la utafiti la kimataifa la Euromonitor, watu wa Afrika kusini, Nigeria na Cameroon pekee wanatumia takriban dola bilioni 1.1 kwenye bidhaa za nywele.

Hiyo ni pamoja na shampoo, mafuta ya nywele (lotion) na relaxer.

Kiwango cha pesa kinachopatikana kwa nywele bandia inazidi hata mafuta hayo ya nywele.

Inaripotiwa, faida inayopatikana kwa biashara ya nywele za kuongezea (weaves, wigs na extensions) ni takriban dola bilioni 6 kwa mwaka.

Biashara hiyo ya nywele barani Afrika imekua kiasi ambacho Unilever mjini Johannesburg inajitapa hasa.

L’Oreal nayo inafanya utafiti zaidi kwenye nywele za Kiafrika na ngozi ili kuongeza bidhaa zake za Dark And Lovely na nyinginezo.

"Ukuaji huu umetokea miaka 10 tu iliyopita, wanawake wana uthubutu inapokuja mitindo ya nywele", kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa L’Oreal Afrika Kusini.

Alisema ghafla sasa unaweza kutumia vifaa vya nywele ambavyo havikuwepo kabisa au vilikuwa ghali mno.

Nywele nyingi zinaouzwa barani Afrika hutoka Asia na hutengenezwa kwa bidhaa rahisi zaidi.


Nywele asili huuzwa pia, lakini hugharimu zaidi.

Chanzo: Africafrique.com
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

MALAYSIA YAWATUMIA GLOVU AFRIKA MAGHARIBI

 A medical worker in Kailahun, Sierra Leone washes their gloves in chlorine on 15 August 2014.
Malaysia ina mpango wa kutoa zaidi ya glovu za mpira milioni 20 za kujukinga katika nchi tano barani Afrika zilioathirika na mlipuko wa Ebola, serikali ya nchi hiyo imesema

Zitasambazwa kwa wahudumu wa afya nchini Liberia, Sierra Leone , Guinea, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Upungufu wa vifaa vya kujikinga imekuwa sababu moja ya kusambaa kwa virusi hivyo.

Maradhi  hayo yameua zaidi ya watu 2,400, wengi wao wakiwemo wahudumu wa afya, mwaka huu, katika mlipuko mbaya kutokea duniani.

Wahudumu wa afya hivi karibuni waligoma nchini Liberia, wakisema wanahitaji vifaa zaidi vya kujikinga.

Malaysia inaongoza kwa uzalishaji wa glovu za mpira, ikitengeneza 60% ya glovu hizo duniani.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

UMOJA WA MATAIFA WASHIKA HATAMU CAR

A local resident sits amid Congolese soldiers of the African-led International Support Mission to the Central African Republic (MISCA)
Majeshi ya Umoja wa Afrika ambayo tayari yapo yataanza kuvaa kofia za bluu

Umoja wa Mataifa unachukua udhibiti rasmi wa shughuli za usalama za Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ambapo takriban 25% ya watu eneo hilo wamekimbia makazi yao.

Hakuna majeshi mapya yaliyosambazwa kuongeza majeshi 5000 ya Afrika na 2,000 ya Ufaransa ambayo tayari yalikuwepo.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema majeshi zaidi yanahitajika haraka iwezekanavyo kumaliza ghasia hizo.

CAR imekuwa katika mgogoro tangu kundi la waasi lenye Waislamu wengi zaidi lilipochukua madaraka kwenye nchi yenye Wakristo wengi Machi 2013.

Kiongozi wa waasi Michel Djotodia alijiuzulu mwezi Januari baada ya shinikizo kubwa la kidiplomasia lakini mauaji yameendelea.

Waislamu wamekimbia mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi yao, huku nchi hiyo ikiwa imegawanyika Waislamu wakiwa kaskazini na Wakristo wakiwa kusini.

NYANI/ KIMA AKIPIGA 'TIZI'

Vimbwanga vya WhatsApp

POLISI YAKAMATA 'MABOMU YA AL-SHABAB' UGANDA



Ugandan police stand guard outside a popular shopping mall in the capital Kampala - 14 September 2014

Polisi nchini Uganda wamesema wamekamata kiwango kikubwa cha mabomu wakati wa uvamizi eneo la washukiwa wa al-Shabab.

Mamlaka zinasema chumba cha magaidi hao kilikuwa kinapanga kufanya mashambulio kwenye mji mkuu Kampala.

Watu 19 wamekamatwa na kuhojiwa juu ya nia zao, msemaji wa polisi alisema.

Uganda imekuwa katika tahadhari ya hali ya juu tangu kiongozi wa al-Shabab, Ahmed Abdi Godane, alipouawa katika shambulio la anga nchini Somalia mapema mwezi huu.

Wiki iliyopita, ubalozi wa Marekani mjini Kampala ulionya kuwepo uwezekano wa mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya Wamarekani nchini humo kutokana na shambulio la anga walilofanya Septemba 2.

Siku ya Jumapili, Marekani ilifuta onyo hilo baada ya kusema inaamini “tishio la moja kwa moja la kushambuliwa na al-Shabab limekabiliwa vilivyo”.

Chanzo: BBC                     
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

WATAKA POSHO YA Sh500,000 KWA SIKU

 “Unajua kuna ‘presha’ kubwa kwamba Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwe imetoka Septemba 21, sasa hiyo inaifanya kamati hiyo kufanya kazi hadi usiku,”.PICHA|MAKTABA 

Mzimu wa posho umeibuka upya katika Bunge la Katiba, safari hii wajumbe wake wa Kamati ya Uandishi wakiomba walipwe posho maalumu ya Sh500,000 kwa siku kutokana na kazi ya kuandika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge zinasema kuwa tayari maoni ya wajumbe yamewasilishwa kwa uongozi kwa ajili ya uamuzi.

Wajumbe wa kamati hiyo kwa sasa wanalipwa posho maalumu ya Sh210,000 zaidi kwa siku, nje ya ile ya Sh300,000 kwa siku wanayolipwa wajumbe wote wa Bunge hilo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi-CCM inahusisha baadhi ya vigogo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Vigogo hao ni pamoja Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro, Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman aliyejiuzulu ujumbe wa kamati hiyo hivi karibuni kwa sababu ambazo hazijaelezwa.

Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad pamoja na kukiri kuwa kamati hiyo imeomba kuongezwa kiasi hicho cha posho, alisema Kamati ya Uongozi ambayo ndiyo huamua, haijayajadili maombi hayo na kuyatolea uamuzi.

Chenge hakupatikana jana kuzungumzia maombi hayo.

Chanzo: Mwananchi, Tanzania

Sunday, 14 September 2014

'WAARABU WATOA MSAADA' WA KUPAMBANA NA IS



US Secretary of State John Kerry boards his plane at Cairo International Airport on 13 September 2014 as he leaves the Egyptian capital.
John Kerry amekuwa akisafiri Mashariki ya Kati kutaka kuungwa mkono kupamabana na IS

Nchi kadhaa za Kiarabu zimejitolea kufanya mashambulio ya anga dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq, maafisa wa Marekani wamesema.

Lakini hamna hatua yoyote itakayochukuliwa mpaka iidhinishwe na serikali ya Iraq, walisema.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesmea “ana imani kubwa” na ahadi zilizotolewa za misaada ya kijeshi za kupambana na kundi hilo.

Alizungumza mjini Paris baada ya ziara ya kasi Mashariki ya Kati kujaribu kushawishi nchi kadhaa kuwaunga mkono ili kupambana na IS.

Ufaransa ina mpango wa kufanya mkutano wa kimataifa kuzungumzia usalama wa Iraq na namna ya kupambana na IS siku ya Jumatatu.

Siku ya Jumamosi, kundi hilo lilitoa video ikionyesha kumkata kichwa mateka wa Uingereza David Haines. Kundi hilo limetishia kumwuua Mwingereza wa pili, Alan Henning, ambaye pia alitokea kwenye video hiyo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

BIBI KIZEE AMTIA ADABU MWIZI

The woman was attacked between Invicta Road (pictured) and Bellevue Road.
Eneo lilipotokea shambulio hilo

 Ajuza mwenye umri wa miaka 80 amempiga ngumi mwizi usoni, na kusababisha atimue mbio.

Bibi huyo alikuwa akimtembeza mbwa wake maeneo ya Whistable, Kent nchini Uingereza, na kujikuta akikamtwa na mtu aliyevaa nyeusi na kuvaa fulana yenye sehemu ya kufunika kichwa pia.

 Alimkimbiza mshambuliaji huyo kwa kumpiga ngumi mdomoni.

 Polisi wa Kent wamesema wanamtafuta mshukiwa aliyejeruhiwa usoni.


Inspekta polisi wa Kent alisema, "Inaonekana mshukiwa safari hii kakosea wa kumshambulia".


RAIS AWAFUKUZA MAAFISA 'WALIOONDOKA' LIBERIA

Food delivered in Monrovia, 12 Sept
Chakula cha msaada chagaiwa kwa maelfu ya walioathirika na Ebola, Liberia

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf amewafukuza kazi maafisa wa serikali 10 walio "nje ya nchi bila sababu yoyote", huku nchi hiyo ikiwa ina mgogoro wa taifa wa Ebola.

Alisema maafisa hao wameonyesha "kutojali janga letu la taifa na kuipiuuza serikali".

Viongozi hao walipewa makataa ya wiki moja zaidi ya mwezi mmoja uliopita warejee nyumbani.

Sierra Leone, Liberia na Guinea ni nchi zilizoathiriwa zaidi katika mlipuko wa ugonjwa huo uliouwa zaidi ya watu 2,400.

Zaidi ya nusu waliofariki dunia kutokana na virusi vya Ebola walikuwa Liberia.

Maafisa hao 10 ni pamoja na makamishna wawili, wasaidizi sita wa mawaziri na manaibu waziri wawili katika wizara ya sheria, Wheatonia Dixon-Barns na Victoria Sherman-Lang.

Maafisa wengine wanane nao wamepewa onyo kurejea nchini humo, na hawatolipwa mpaka warudi.

'ABAKWA HADI KUFA' NA WAKE ZAKE 5



 sex1
Mfanyabiashara mwenye uwezo mkubwa na mwenye wake sita- amefariki dunia baada ya kile kinachodaiwa kulazimishwa kufanya mapenzi kwa mkupuo na wake zake wenye ‘wivu’.

Uroko Unoja, raia wa Nigeria alikuwa akifanya mapenzi na mke mdogo ambapo inaripotiwa wake waliobaki wakamvamia na visu na fimbo – kutaka afanye nao mapenzi pia.

Bw Onojo akafanya mapenzi na wake zake wanne mmoja baada ya mwengine, lakini akaacha kupumua baada ya mke wa tano kuelekea kupata zamu yake, kulingana na gazeti la Daily Post la Nigeria.

Wanawake wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo katika jimbo la Benue wiki iliyopita, ilisema ripoti hiyo, ikitumia sentensi ‘kubakwa hadi kufa’ kuelezea hatma ya mfanyabiashara huyo.



MAHARUSI WANAPOANGUA KICHEKO GHAFLA

Vimbwanga vya WhatsApp

'MAUAJI' MENGINE KUFANYWA NA IS YACHUNGUZWA

David Haines
Bw Haines alitekwanyara mwaka jana alipokuwa akitoa misaada Syria

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema " inafanya kazi haraka iwezekanavyo kuthibitisha"  video inayodai kuonyesha kukatwa kichwa kwa mateka ambaye ni raia wa Uingereza, David Haines.

Wizara hiyo imesema kama ni kweli ni "mauaji ya kukera", na wakati huohuo wanaendelea kushirikiana na familia ya Bw Haines.

Mfanyakazi wa shirika moja la kutoa misaada, mwenye umri wa miaka 44, kutoka Perth, alitekwa mwaka jana nchini Syria.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State IS tayari wamewakata vichwa waandishi wawili wa habari wa Marekani na kutishia kumwuua Bw Haines iwapo mashambulio ya anga ya Marekani nchini Iraq hayatositishwa.

Bw Haines, baba wa watoto wawili, alichukuliwa mateka katika kijiji cha Atmeh, jimbo la Idlib nchini Syria, mwezi Machi 2013.

Alikuwa akilisaidia shirika la Kifaransa la kutoa misaada Acted, baada ya kufanya hivyo hapo awali nchini Libya na Sudan kusini.

Tukio hilo limetokea saa chache baada ya familia yake kuliomba kundi la IS moja kwa moja kuwasiliana nao siku ya Ijumaa.

Video hiyo inaonyesha pia tishio la kumwuua mateka mwengine Mwingereza.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema tukio hilo "ni la kukera mno na la kutisha"

"Ni tukio la ukatili wa hali ya juu. Ninawapa pole familia ya David Haines walioonyesha ujasiri wa ajabu mpaka sasa na wakati wote tangu alipotekwa.

"Tutafanya kila liwezekanalo ndani ya uwezo wetu kuwasaka wauaji hawa na kuhakikisha haki inatendeka, hata iwe kwa muda gani," alisema.

Msemaji wa serikali ya Uingereza alisema waziri mkuu huyo ataitisha mkutano wa dharura baadae hii leo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

Saturday, 13 September 2014

UGANDA YATAHADHARISHWA JUU YA AL-SHABAB

Uganda's Entebbe Airport on 3 July 2014
Usalama uliimarishwa maeneo muhimu, ukiwemo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe

Serikali ya Uganda imegundua chumba cha magaidi inachoamini walikuwa wakijiandaa kufanya shambulio wakati wowote, ubalozi wa Marekani mjini Kampala ulisema.

Ubalozi huo umesema chumba hicho kinamilikiwa na kundi la Somalia la Al- Shabab, lakini hilo bado linatakiwa kuthibitishwa na polisi wa Uganda.

Awali ubalozi huo uliwaonya raia wa Marekani kubaki nyumbani wakati wa harakati za polisi za kukisaka chumba hicho.

Polisi Uganda walisema wameimarisha usalama kwenye maeneo ya umma mjini Kampala, na kukamata watu kadhaa.

Mapema wiki hii, ubalozi wa Marekani ulionya uwezekano wa kuwepo mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya Wamarekani yatakayofanywa na al-Shabab kufuatia shambulio la anga lililomwuua kiongozi wao Ahmed Abdi Godane, Septemba 2.

Washukiwa wanaaminiwa kuwa raia wa kigeni, amesema mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga.

Kundi hilo la al-Shabab, linalotaka kupindua serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa limemtaja Ahmad Umar kuwa kiongozi wao mpya.