Wednesday, 31 December 2014

RAIS KENYATTA ATEUA INSPEKTA MPYA WA POLISI

 


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemteua Joseph Kipchirchir Boinet, kuwa Inspekta Jenerali mpya wa polisi nchini humo.

Amechukua nafasi ya , David Kimaiyo, aliyejiuzulu, kufuatia mauaji ya wachimba migodi 36 Mandera, kaskazini-mashariki mwa Kenya.

Boinet alijiunga na shirika la kijasusi mwaka 1998.

Bunge linatarajiwa kuidhinisha uteuzi wake kabla ya kupitishwa rasmi.




Tuesday, 30 December 2014

FURAHA KUONGEZEKA DUNIANI, AFRIKA KINARA



A handout picture taken by Prince Harry shows Lesothan children posing for a photograph at a herd boy school supported in Mokhotlong, Lesotho (December 2014)
Waliohojiwa Afrika ndio wenye furaha zaidi

Watu wenye furaha inaongezeka duniani, kulingana na utafiti wa mwisho wa mwaka wa watu  64,000 katika nchi 65.

Shirika lililofanya utafiti huo WIN/Gallup liligundua kuwa 70% ya waliohojiwa wameridhika na maisha yao – idadi iliyoongezeka kwa 10% kutoka mwaka jana.

Fiji ndilo taifa lenye furaha zaidi, huku 93% ya wakazi wakiwa na furaha na kuridhika, na Iraq ikiwa la mwisho lenye furaha kwa 31%.

Utafiti huo umeonyesha kuwa Afrika ni bara lenye furaha zaidi, huku 83% ya watu wakisema wana furaha au furaha sana.

Wakati huohuo, Ulaya ya Magharibi ilionekana eneo lenye watu wengi wasio na furaha, huku 11%  wakisema hawana furaha au hawana furaha hata kidogo.

Kwa takwimu za ulimwengu, 53% ya waliohojiwa walihisi mwaka 2015 utakuwa mzuri zaidi kuliko 2014.

Robo tatu ya waliohojiwa Afrika walikuwa na matumaini makubwa ya maisha kuimarika, ikilinganishwa na 26% ya waliopo Ulaya ya Magharibi.

Nigeria ndio nchi yenye hisia chanya kuliko zote, huku Lebanon ikiwa yenye hisia hasi kuliko zote.




Monday, 29 December 2014

MARUBANI WA AIR TANZANIA WAWAACHA ABIRIA 'MABOYA'


 map

Zaidi ya abiria 100 wamekwama katika uwanja wa ndege nchini Tanzania kufuatia marubani kushindwa kuripoti kazini baada ya mapumziko ya Krismasi, maafisa walisema. 

Walitaka wawe wamesafiri Desemba 27 kutoka Dar es Salaam hadi visiwa vya Comoro na maeneo mengine.

Abiria wenye hasira walililaumu shirika la ndege linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo, Air Tanzania, kwa kutowahudumia uzuri.

Msemaji wa Air Tanzania alisema shirika hilo halijui kwanini marubani hao hawakuripoti kazini.

Marubani hao walipewa nafasi ya kupumzika siku ya Krismasi na siku iliyofuata na kutarajiwa kurejea kazini Jumamosi.

"Tunahisi huenda kukawa na tatizo kwasababu hili si jambo la kawaida ," alisema msemaji huyo, Lily Fungamtama.

"Tunaomba radhi kwa abiria wetu wote kutokana na hali hii na tumefanya kila liwezekanalo kuwatafutia ndege mbadala," aliongeza.

Abiria mmoja aliiambia BBC hana uhakika tena kama anaweza kuliamini shirika hilo, kwani limekuwa mara kwa mara likivunja ahadi zake ya lini ndege hiyo itaondoka.

Abiria waliokuwa wasafiri kuelekea katika miji ya Kigoma, kaskazini- magharibi mwa nchi hiyo na 
 Mtwara uliopo kusini wamekwama, pamoja na wale waliokuwa wakielekea visiwa vya Comoro.

Mwandishi wa BBC alisema abiria, wakiwemo wanawake na watoto, wamepewa malazi katika hotel ndogo ndani na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam.

 

SOMALIA YAANZA KUTOA BIMA KWA 'MARA YA KWANZA'


 

Biashara ya kwanza ya Bima kwa zaidi ya miaka 20 imeanza kwenye mji mkuu Mogadishu nchini Somalia.

Kampuni hiyo (Somali Takaful and Re-Takaful) inayosema inafuata sharia za Kiislamu itaanza kwa kutoa bima za mota na mizigo ya majini.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mohamed Jesow alisema watu wengi Mogadishu hawajui hata bima ni nini, kwani nchi hiyo imekuwa uwanja wa vita tangu serikali kuu kuporomoka mwaka 1991.

Alisema wateja watakaolipwa fidia ni wale ambao mali zao ziliharibiwa kwa bomu na mashambulio mengine, ilimradi hawakulengwa wao moja kwa moja.

Ulinzi umeimarika Mogadishu katika miezi ya hivi karibuni, lakini kundi la al-Shabab na wengine mara nyingi hufanya mashambulio.



HISABATI KWELI ZINA WENYEWE

     

Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

GEORGE WEAH ASHINDA USENETA LIBERIA