Marcos Rojo amepewa kibali cha kazi na hivyo anatarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya QPR
|
Kijana mpya wa Manchester United Marcos Rojo ataonekana kwa mara ya
kwanza dhidi ya Queens Park Rangers kwenye uwanja wa Old Trafford
Septemba 14 baada ya kupewa kibali cha kufanya kazi.
Rojo alikwenda Ureno siku ya Alhamisi kwa ajili ya kukamilisha masuala yanayohusu kibali chake cha kazi.
Uwepo wake utakisaidia kikosi cha Louis van Gaal ambaye amekuwa na tatizo la ulinzi kwenye mechi za kwanza za msimu huu.
Rojo aliruhusiwa kufanya mazoezi Manchester United licha ya kutokuwa na kibali cha kazi |
Muargentina huyo, 24, hakuwahi kushtakiwa kwa tukio hilo, ambalo lilitokea mwaka 2010, ila bado lilikuwa likifanyiwa uchunguzi wa kinadharia baada ya kesi kufunguliwa upya mwezi Mei mwaka huu.
Chanzo: taarifa.co.tz
No comments:
Post a Comment