Joan Rivers akitangaza kitabu chake cha kumi, Diary of a Mad Diva, mapema mwaka huu |
Mchekeshaji na mtangazaji wa televisheni Joan Rivers
ametolewa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na “amewekwa mahala tulivu” katika
chumba binafsi hospitalini.
Rivers, mwenye umri wa miaka 81, amekuwa akitumia mashine kupumua akiwa kwenye hospitali ya Mount Sinai tangu kupata maradhi ya moyo mjini New York wiki iliyopita.
Pumzi za mchekeshaji huyo zilisita wakati wa upasuaji wa mishipa yake ya sauti kwenye zahanati moja Alhamis iliyopita.
Binti yake, Melissa Rivers, alitoa taarifa kuthibitisha afya ya mama yake ikiimarika siku ya Jumatano.
“Mama yangu ametolewa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na kupelekwa chumba binafsi,” ilisema taarifa hiyo kutoka Melissa. “Ahsante kwa nyote mnaoendelea kunipa moyo.”
Joan Rivers amekuwa kwenye mashine za kupumulia kwa zaidi ya wiki moja. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu afya yake.
Muigizaji na mchekeshaji huyo anajulikana sana kwa kauli zake kali na za kuchoma, na hivi karibuni ameanza kuwananga watu mashuhuri wanohudhuria matamasaha makubwa wanopita kwa kile kiitwacho ‘red carepet’ kwenye kipindi chake cha Fashion Police.
No comments:
Post a Comment