Mlipuko wa Ebola umeenea kwenye nchi tano Afrika Magharibi |
Zaidi ya watu 1,900 wamefariki dunia Afrika magharibi
kutokana na mlipuko wa Ebola, shirika la Afya duniani WHO limesema.
Kumeshathibitishwa kuwepo wagonjwa 3,500 nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia
Shirika hilo linakutana Alhamis kutathmini tiba gani bora na namna ya kujadili kufanyika vipimo vya haraka na uzalishaji wa dawa.
Wataalamu wa kudhibiti maradhi, watafiti wa tiba, maafisa kutoka nchi zilizoathirika, watawakilishwa kwenye mkutano Geneva.
Takriban dola za kimarekani milioni 600 zinahitajika kupambana na kirusi hicho, na zaidi ya watu 20,000 wanaweza kuambukizwa kabla ya mlipuko huo kudhibitiwa, WHO imeonya.
Mkuu wa WHO Margaret Chan ameelezea mlipuko huo “ni mkubwa, hatari na wenye utata mkubwa waliowahi kuuona”.
“Hakuna yeyote, hata wataalamu wa maradhi ya milipuko wenye uzoefu wa tangu mwaka 1976 hadi 1995, watu ambao walihusika moja kwa moja na milipuko hiyo, hakuna aliyeona kitu kama hicho,” alisema
Zaidi ya asilimia 40 ya vifo vimetokea katika kipindi cha wiki tatu kuelekea Septemba 3, WHO, ikiashiria kuwa ugonjwa huo unaongezeka kwa kasi kiasi cha kushindwa kuudhibiti.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment